Hongera Mh. Rais la uchaguzi huru na haki lakini mbona zilongwa mbali na zintendwa mbali

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
1,476
Points
2,000

sammosses

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
1,476 2,000
Kila Mtanzania mwenye akili timamu ana amini kuwa Watanzania tuna haki sawa mbele ya sheria. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977.

Katiba kwa Kulijua hilo imetoa haki ya kuchaguliwa na kuchagua viongozi tuwatakao kwa mujibu wa sheria na katiba hii.

Nichukue fursa hii kumpongeza rais Magufuli kwa tamko lake la hivi karibuni kuwa uchaguzi utakuwa wa haki, huru na uwazi, big up sana.

Pamoja na pongezi hizi, tamko lako bado lina ukakasi kutokana na maagizo ya awali kuwa, utamshangaa sana mkurugenzi ambaye kwa sasa mnamwita msimamizi msaidizi wa uchaguzi, akimtangaza mpinzani kuwa ameshinda, kwa kuwa ameajiriwa na serikali ya CCM, amepewa gari, nyumba nakadhalika.

Nachelea kusema hivi kutokana na Rais kutokutoa tamko la kukanusha kauli hii ndani ya serikali na nje ya serikali, kwa maana ya chama chake.

Lakini nimkumbushe kuwa ameshindwa kutengua kauli ya kuufuta upinzani aliyoitoa Feb 2016 huko Singida,kauli iliyo ambatana na kuzuiwa kwa siasa za hadharani mpaka 2020.

Pamoja na kuwa mwaka 2020 ndo tulionao, bado tamko lake limesimama bila kutenguliwa kwa kauli yake mwenyewe, kwa kuwa wapinzani wake wa kisiasa bado wanasumbuliwa na kukamatwa ama kuzuia kufanya siasa za wazi.

Maanake nini, ni kuzuia wapinzani kunadi sera zao angalau kwa muda huu mfupi wakati yeye na chama chake wakiendelea kufanya siasa kwa miaka yote 5 bila kusumbuliwa.

Hii ina ondoa adhima ya tamko na nia yake kama kweli ni kauli thabiti.

Wakati wa sherehe za kuazimisha miaka 58 ya uhuru Kiongozi wa upinzani bungeni (KUB),alishauri na kutaka maridhiano ya kitaifa, alizungumza bila kupepesa macho kwa tashwishi mbele ya halaiki ya Watanzania jijini Mwanza umuhimu wa maridhiano.

Tukio lile lilipokelewa kwa hisia kali na kila mpenda maendeleo nchini mwenye akili timamu. Japo wapo waliobeza kwa utashi wao wakiamini kwa jinsi tulivyo wana neemeka kupitia misuguano hii.

Hatujasikia tamko la Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM na Amiri jeshi mkuu kuhusiana na ujumbe aliopewa na mh. Mbowe, wala juhudi zozote za maridhiano zikifanyika.

Lakini ndani ya kizungumkuti hicho kuna ibuka tamko la uchaguzi huru WA haki, amani na uwazi. Kama si zilongwa mbali nazintendwa mbali ni nini!!!

Utakuwaje na uchaguzi wa huru, amani na haki ikiwa hatuna tume huru ya uchaguzi ambayo ni shirikishi angalau kama ile iliyo kuwa chini ya Jecha baada ya muafaka wa zanzibar (Zanzibar accord) , japo aliamua kuvuruga kwa amri toka juu.

Mazingira ya uchaguzi si salama, hayatoi uhuru wa kufanya uchaguzi huru na haki.

Rais kuwaaminisha Watanzania kwa maneno ni kuwatega kwa mtego wa kuku, kumtupia mahindi na kumkamata.

Watanzania wanataka tume huru iliyo shirikishi itakayo weza kusimamia maamuzi sahihi ya Watanzania bila kuingiliwa na mamlaka yeyote.

Hapo ndipo tutakuwa tumetibu sintofahamu za chaguzi zote zilizo pita.

Tukiendelea na matamko yasiyo na uhalisia na kujitangaza kuwa umeshinda kwa 98% wakati hukuwa na mshindani, uchaguzi haukuwepo, utakuwa unapalia vuguvugu la joto la kisiasa kila kukuchapo.

Ni vizuri wadau wa uchaguzi, viongozi wa dini asasi za kiraia, taasisi za haki za binadam washirikishwe kabla ya kukimbilia uchaguzi, vinginevyo mchelea mwana kulia hulia yeye.

Tujifunze kwa wenzetu waliopita tulipo na walipofikia walipo ili tuboreshe zaidi kwa maslahi mapana ya nchi.

Hatuendi kumteua mfalme kwa kuwa hii si monarchy state,tuna kwenda kuwachagua viongozi wa wananchi kwa matakwa ya wananchi,na kwa kuwa kilio kikubwa ni tume huru hatuna budi kama taifa kujitafakari upya kwa mustskabali wa amani.

Kubeza kuwa watu wanalilia tume huru wakati hawana wapiga kura hakuleti tija hasa kwa maneno ya khanga kutamkwa na msomi nguli.

Wapiga kura ni Watanzania, vyama ni vya Watanzania, kukiona chama chako kina haki kuliko vyama vingine ni kuwagawa Watanzania katika misingi ya haki na usawa.

Tukiendekeza hii kasumba tutaingiza nchi kwenye janga la machafuko makubwa, kwani nchi takribani zote zilizoingia kwenye machafuko sababu kubwa ni uchaguzi.

Tuachane na tume ya uchaguzi ya watawala yenye kuwanufaisha watawala, tuna taka tume ya uchaguzi ya wananchi kwa maslahi mapana ya nchi itakayo simamia haki na kutimiza wajibu wake.

Tume iliyo teuliwa na rais kuanzia Mwenyekiti, mkurugenzi na wasimamizi wasaidizi kwa maana ya wakurugenzi watendaji wa halmashauri ambao ni makada wa CCM atakaye thubutu kushiriki atakuwa ni mwendawazimu mwenye kubariki dhuluma dhidi ya haki.

Ni viase vyama vya siasa kama wadau wa uchaguzi, ngoma ikipigwa Sana mwisho hupasuka, tusisubiri ngoma ipasuke ndipo tutafute ngozi ya kuwamba ngoma.

Tumieni umoja wenu wa vyama vya siasa pamoja na changamoto za upendeleo wa wazi toka kwa msajili wa vyama vya siasa aliyeteuliwa na mwenyekiti wa chama, kuhakikisha muafaka na maridhiano yatasababisha Watanzania tupate tume huru.

Niwasihii viongozi wa CCM wanao toa kejeli kuhusu tume huru, kuwa kauli zao zina mpotosha mwenyekiti wenu, ifike mahali mshaurini kwa hekima kwa kumsaidia kuliko kumpotosha na mkumbuke nje ya mwenyekiti ni Rais wa Watanzania.

Viongozi wa vyama mbadala kulalamika hakuwezi kuisaidia nchi, mko kisheria matamko yasiyo na tija hayawasaidi wananchi, pambaneni kwa hoja ili maridhiano yawe ya wananchi. Hali tete kwa wananchi kwa sasa.

Msitugawanye kwa umoja wetu kwa itikadi za kivyama ila msirudi nyuma kupambania haki, kwa kuwa haki huinua taifa ni haki yenu kwa mujibu wa katiba kutafuta mamlaka ya kiutawala ili kutonyesha madhaifu ya waliopo madarakani.

Tusibaguane kwa Utanzania wetu, katiba imetoa mamlaka na haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi bila kuanisha ni wa itikadi gani.

Katiba imewataka Watanzania watekeleze haki hiyo, mizengwe ya nini!!!

Mungu ibariki Tanzania
 

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
12,797
Points
2,000

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
12,797 2,000
Ukirefer uchaguzi wa serikali za mitaa ukiofanyika hivi majuzi nchini, kauli ya Rais ina umbali wa kutoka hapa duniani na kwenda mbinguni!
 

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Messages
1,476
Points
2,000

sammosses

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2011
1,476 2,000
Mbona Viongozi wa CCM tena wa ngazi za juu wanausifia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa eti ulikuwa Huru na Haki isije ikawa hata huu 2020 ndio utakavyokuwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Maandalizi mengine ya uchaguzi kama wa TAMISEMI, unajua nchi hii tuna tabia ya kupimana, ukiona hakuna impact kwa ujinga uliofanya kwa negativity response una fanya mwendelezo huo huo ukiamini utafanikiwa hii imetuweka pabaya sana kama nchi.

Tuendeshwa Kama train kwa kufuata mwelekeo yote uoga.
 

Forum statistics

Threads 1,391,690
Members 528,449
Posts 34,086,839
Top