Hongera Mh. Hamis Kagasheki; Lakini ninaomba unijubu maswali yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Mh. Hamis Kagasheki; Lakini ninaomba unijubu maswali yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kichenchele, Aug 14, 2012.

 1. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Kufuatia sakata la kusafirishwa kwa wanyama hai akiwemo twiga na wanyama wengine kwenda nje ya nchi kwa njia zisizohalali kulikofanywa na watu wenye tamaa na kukosa huruma kwa watanzania wenzao. jana Waziri wa wizara husika aliweza kuutangazia umma juu ya kuwapa karipio baadhi ya wahusika, kuwashusha vyeo na wengine kuwafukuza kazi tena kwa kuwatangaza majina yao hadharani, kwa hili mm ninakupongeza sana, lakini ninaomba tu pamoja na pongezi hizi nakuomba unipe majibu ya maswali yangu machache yafuatayo.

  1: Mh. Kagasheki, kuna habari njema za kurejea kwa mjusi mkubwa aina ya Dinosaur aliyechukuliwa toka nchini na kupelekwa nchi fulani na kuwanufaisha wao; je kuna jitihada zozote za kuwarejesha hawa wanyama waliopakiwa kwenye ndege tena wakiwa hai?

  2: kuna sababu zipi za msingi zilizopelekea baadhi wa wahusika wa sakata hili kupewa karipio, na kuwashusha vyeo badala ya kuwawajibisha kwa kuwafukuza kazi na kuwataja kwa majina ili umma uwatambue kama ulivyofanya kwa hawa uliowataja jana?

  3: kuna mkakati gani wa kuhakikisha hasara iliyosababishwa na hawa wahusika inakuwa covered?

  4: unaweza kuujulisha umma kampuni ya ndege iliyohusika na usafirishaji wa wanyama hawa, kwani naamini hata kama ni ndege ya mtu binafsi tunavyo vyombo vya ulinzi vinavyoweza kutambua kuingia na kutoka kwa hivi vyombo vya angani.

  NAOMBA KUWASILISHA. AHSANTE NA KAZI NJEMA.
   
 2. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nitamsaidia kujibu hili moja sisi serekalini hatuna kawaida ya kushughulikiana kidhati zaidi tunajitahidi kubabaisha ili mtuone tunafanya kazi kumbe sio.halafu hao niliowakaripia hawagusiki moja kwa moja kwa sababu ntahatarisha kibarua changu.hata hao ambao tumekutangazia tumewafukuza tutawatafutia hata vikazi au vimiradi vya siri vya kujishikiza.umeelewa kijana na bahati yako na wenzako mnaficha id zenu hampajui mabwepande ninyi au mnafikiri tutakosea tena kama tulivyomkosa yule mpumbavu we subirini tu.na tutawatawala hata kama tumeshindwa kuongoza.
   
 3. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  ahsante sana kwa majibu yako,
   
 4. u

  upendom Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndege iliyotumika ni katar
   
Loading...