Hongera Mh. Dr. Jakaya Mrisho kwa kuwakilisha vema Nchi yetu!!

Nzilo

Senior Member
Nov 24, 2013
180
58
Kwa mara nyingine nimeamini kuwa bado tuna hazina kubwa ya wanadiplomaisia!!. Na ulimwengu unajua sasa kuwa Tanzania ina nafasi gani na mchango gani katika kupigania Uhuru wa Waafrika wenzetu hususani Uhuru wa ndugu zetu wa Afrika kusini.... Zaidi nimefurahishwa na hotuba yako Mh. JK umetuwakilisha vema watanzania wenzako... haya ndiyo mafanikio tunayoyahitaji na umeonesha wazi kuwa huutwi Rais kwa kubahatisha ni pamoja na kufanya vizuri kimataifa.... Hongera sana Mh. Dk. Jakaya!!!
 
Kutokana na utendaji mbovu wa baraza hilo maarufu kama baraza la maswahiba rais huyo ameshinikizwa kuwatimua maswahiba wachovu katika baraza lake na kuzidi kudhoofisha chama pamoja na sirikali katika kutumikia wananchi.
Ukirudi nyumbani useme na wananchi kwa staili ya africa kusini
 
wazee amebaki kaunda. jk umepata nafasi ya kusikia hekima yake..love ua neighbour as you love uaself. Do what you wanna people do 2u. Maneno mazito tunapoelekea kwenye katiba ya nchi. Remember we are all God's image
 
kwa mara nyingine nimeamini kuwa bado tuna hazina kubwa ya wanadiplomaisia!!. Na ulimwengu unajua sasa kuwa tanzania ina nafasi gani na mchango gani katika kupigania uhuru wa waafrika wenzetu hususani uhuru wa ndugu zetu wa afrika kusini.... Zaidi nimefurahishwa na hotuba yako mh. Jk umetuwakilisha vema watanzania wenzako... Haya ndiyo mafanikio tunayoyahitaji na umeonesha wazi kuwa huutwi rais kwa kubahatisha ni pamoja na kufanya vizuri kimataifa.... Hongera sana mh. Dk. Jakaya!!!

mbona kuna uzi humu katoa data za uongo? Au mliandaliawa kumsifu kabla ya hotuba yenyewe?
 
Sidhani km kusifia jambo jema lililofanywa na Kiongozi yeyote wa nchi kuwa ni kuandaliwa kufanya hivyo.....!!! kimsingi nimefuatilia tukio hilo mwanzo mwisho TBC... Andrew kwangu mimi kusifia jambo jema ndiyo desturi yangu.
 
Last edited by a moderator:
Siyo siri, speech ile imenigusa na ninahisi imemgusa kila mtu aliyefuatilia tukio hilo, hasa alipokuwa anasimulia kile kipindi Mandela alichokuja Tanzania 1960s...
 
Back
Top Bottom