Hongera Mathew Kilama kwa Kuteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma

Kugosola

Senior Member
Aug 7, 2021
191
258
Ndugu Mathew Kilama, Wakati nakupongeza kwa kuteuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ningependa kukupa angalizo kuhusiana na utendaji usioridhisha wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Ningekushauli utafute threads humu JF kuhusu malalamiko lukuki ya utendaji mbovu wa Tume. Watu wameilalamikia sana Tume kuhusu kupoka na kuhujumu haki za watumishi wa umma wanaokata rufaa Tume kwa kushirikiana na waajiri. Watumishi wamekuwa wahanga kwenye hiyo Tume wakati wakitafuta haki yao.

Wafanyakazi wa Tume wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea bila kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma, wanajifanyia wanavyotaka wao na sio Kanuni za Utumishi wa Umma.

Hebu waangalie sana washauli ambao umewakuta wasije wakakupotosha.

Na mwisho nakushauli kuwa, TENDA HAKI na Mungu atakuinua na kukupeleka juu zaidi!!
 
kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
5,843
7,127
Na waajiriwa wanafanya makosa kwa kiburi kudhani Tume itawarudisha kazini! Mfano unajua kuwa kukosekana kazini kwa muda wa siku 5 mfululizo bila ruhusa ni kujifukuzisha kazi?
 
Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,908
6,459

Tulia wewe mamalia wa Tume mbona hilo kosa linajulikana? acheni tabia zenu za kushirikiana na waajiri kukandamiza haki za waajiriwa.
 
Admin1988

JF-Expert Member
Mar 30, 2017
1,454
1,541
Huyu jamaa ndiye aliye RUHUSU niandikiwe barua moja utumishi kuhamishiwa wizara nyingine.
BIG UP
 
PrN-kazi

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
2,900
440
Alafuuu!!, hivi maamuzi yalitolewa na Tume uwa yanawafikia walengwa baada ya muda gani????.

Kuna sintofahamu, nakutana na wahanga mitaani wakiwa wanalalamika kwamba waliambiwa kesi zao zilishatolewa uamuzi na Tume wakaambiwa wasubirie barua zao mpaka sasa inaelekea kufika miezi miwili barua hawajazipata, wanajiuliza barua zinaandaliwa kwa muda gani!!!!?
 
theWarrior1

New Member
Jan 11, 2022
1
0

Ni huzuni sana, pia wengine tulitaarifiwa kuwa rufaa zetu zilifanyiwa uamuzi toka kikao kilichopita kilichoisha Mwezi wa 11, ila mpaka leo hatujapokea Barua unaelekea Mwezi wa 3 huu toka kikao kilipokwisha. Hao waliolalamika vipi mpaka sasa wameshapokea Barua zao?
 
Kugosola

Senior Member
Aug 7, 2021
191
258
Ni huzuni sana, pia wengine tulitaarifiwa kuwa rufaa zetu zilifanyiwa uamuzi toka kikao kilichopita kilichoisha Mwezi wa 11, ila mpaka leo hatujapokea Barua unaelekea Mwezi wa 3 huu toka kikao kilipokwisha. Hao waliolalamika vipi mpaka sasa wameshapokea Barua zao?
Pole sana ndugu yangu.

Eti kuna kilaza mmoja ofisi ya Tume tena ni senior official kabisa anajitetea kwamba eti Tume inavunja Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma kwa kuchelewa kutoa maamuzi ya rufaa za watumishi wa umma kwasababu eti maofisa wa Tume ni wachache, this is hopeless to the maximum.

Tume inaminya haki za watumishi at the expense ya uchache wao maofisa wa Tume!
 
Precise Pangolin

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
12,908
6,459
Ni huzuni sana, pia wengine tulitaarifiwa kuwa rufaa zetu zilifanyiwa uamuzi toka kikao kilichopita kilichoisha Mwezi wa 11, ila mpaka leo hatujapokea Barua unaelekea Mwezi wa 3 huu toka kikao kilipokwisha. Hao waliolalamika vipi mpaka sasa wameshapokea Barua zao?
Kuna ndugu yangu ni mhanga wa tume mpaka leo mwezi wa sita hajapata barua yake ya maamuzi
 
Salhat

Senior Member
Oct 14, 2018
182
410
Imefika miez sita ssa hawashughulik na rufaa Wala malalamiko kisa mwenyekiti kastaafu ingekuwa bandar wangekaa mdaa mrefu hvyo bila kufanya teuzi au kwasab hiki kitengo hakiwaingizii fedha dah
 
Kugosola

Senior Member
Aug 7, 2021
191
258
Imefika miez sita ssa hawashughulik na rufaa Wala malalamiko kisa mwenyekiti kastaafu ingekuwa bandar wangekaa mdaa mrefu hvyo bila kufanya teuzi au kwasab hiki kitengo hakiwaingizii fedha dah
The Banana Republic!!😆😆😆😆

Kuna thesis ya mtahiniwa mmoja kichwa cha habari kimeandikwa hivi; "The Tanzania Civil Servants Appeal Authorities Surprisingly" kwa maana ya kwamba utendaji kazi wake ni wa hovyo kabisa, haki za watumishi zinadhurumiwa kwa makusudi kabisa.

Mh. Rais Samia Suluhu Hassan hebu siku kilio hicho.
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
65,159
69,227
Ndugu Mathew Kilama, Wakati nakupongeza kwa kuteuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ningependa kukupa angalizo kuhusiana na utendaji usioridhisha wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Ningekushauli utafute threads humu JF kuhusu malalamiko lukuki ya utendaji mbovu wa Tume. Watu wameilalamikia sana Tume kuhusu kupoka na kuhujumu haki za watumishi wa umma wanaokata rufaa Tume kwa kushirikiana na waajiri. Watumishi wamekuwa wahanga kwenye hiyo Tume wakati wakitafuta haki yao.

Wafanyakazi wa Tume wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea bila kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma, wanajifanyia wanavyotaka wao na sio Kanuni za Utumishi wa Umma.

Hebu waangalie sana washauli ambao umewakuta wasije wakakupotosha.

Na mwisho nakushauli kuwa, TENDA HAKI na Mungu atakuinua na kukupeleka juu zaidi!!
Jitahidi matumizi ya R&L
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom