Hongera mama Ananilea Nkya kwa tuzo ya mwanamke jasiri 2010

Zion Daughter

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
8,921
4,235
Unastahili tuzo(Tuzo ya mwanamke jasiri 2010-toka USA) hiyo kwa kuwa umekuwa mstahili wa mbele kutetea haki za waTZ ikiwa ni pamoja na wanawake kwa ujumla.
Ni wachache sana wanaweza fanya uliyofanya.
Mungu akubariki sana na akupe nguvu zaidi ufanye makuu zaidi.
Tupo nyuma yako kwenye harakati hizi na tunasema Hatutadanganyika.
 
hongera zako mama!umekuwa ICON nzuri kwa charity mwaka 2010
 
hongera zako mama!umekuwa ICON nzuri kwa charity mwaka 2010
Kweli yani.Halafu yule mama siyo manafiki kabisa,Ndicho nampendea.
Natoa wito kwa wanawake wote kama akina Sophia Simba na wengineo tuige mfano wake.
 
Hongera sana mama Ananilea Nkya!! Ninafurahishwa sana na mchango wako kwa taifa hili and top of all unajiamini maana una uhakika na unachokifanya!! Again, keep it up mom!
 
hivi mwaka 2010 si ndo umeanza tu? anyway hongera mama, ni kweli huyu mama hu-call a spade, a spade and i love that.
 
hivi mwaka 2010 si ndo umeanza tu? anyway hongera mama, ni kweli huyu mama hu-call a spade, a spade and i love that.
Mwezi wa tatu huu dadake stuka.Robo ya mwaka tushaikata tayari.Lakni nadhani assesment yao huwa inabase mwaka uliopita.Kama yeye labda aliyofanya kwa mwaka 2009.
 
hongera sana mama, wewe ni mfano bora kwa wanawake wa Afrika kwa ujumla. nashauri wanawake tuige mfano wake KWA MAENDELEO YA WANAWAKE NA TAIFA KWA UJUMLA
 
Just curious.Atampongezaje?kwenye TV au kumpa uongozi?

Precisely, Betty mkwasa alipopata CCN Multichoice award, akapongezwa kwa u-DC.

But ukikaa na huyu mama umsikie comments zake kuhusu wanaume.....!!!! you can comment about her otherwise.
 
Precisely, Betty mkwasa alipopata CCN Multichoice award, akapongezwa kwa u-DC.

But ukikaa na huyu mama umsikie comments zake kuhusu wanaume.....!!!! you can comment about her otherwise.


Kwani vipi ndugu yetu, tufahamishe.
 
Hongera sana Mama Nkya! You surely deserve the prize for your struggle and commitment for the betterment of our beloved country. Tunaomba tu hiyo tuzo iwe changamoto ya kukufanya uendeleze mapambano na isiwe tuzo la kukufanya uridhike na kurudi nyuma. Yu wapi Mama Kijo mbona hasikiki sana siku hizi? Mama Kilango naye baada ya kupata tuzo mwaka naona kama ameanza kulegeza uzi wa mapambano! This last sentence will 'cost' me. Peace! Ha ha haaaa!
 
who is this good mama? What she does?

huyu ni mwnaharakati wa kutetea haki za binadamu (si wanawake tu kama wengi tunavyofikiri)

if am not mistaken anajihusisha sana na watu wa media and works with tamwa.

I stand out to be corrected!!!
 
[/SIZE]

Hata mpongeza kwa sababu Ananilea si mwanasiasa na nadhani si mwanachama wa CCM.
Jana kwenye kipindi cha pambanua channel 10, kuna mtazamaji aliuliza kama yeye (na wenzio waliokuwemo kwenye interview ile) atagombea ubunge...

akasema kuwa anaamini Mungu kampa kila mmoja karama na yeye karama anaamini anafanya vizuri kwenye karama aliyotunukiwa kwa hivo jibu ni kuwa hata gombea ubunge (or even be in politcs in a way).
 
Yu wapi Mama Kijo mbona hasikiki sana siku hizi?
Mkuu mama Hellen Kijo-Bisimba yupo Uingereza anako kula nondoz ya udaktari wa falsafa (shahada ya uzamifu) wa masuala ya haki za binadamu. Kwa mara ya mwisho alionekana hapa bongo mwishoni mwa mwaka jana alipokuwa nakusanya data za utafiti wake kwenye wilaya za nyanda za juu kusini na kanda ya ziwa. Mama Kijo-Bisimba hasikiki sana siku hizi kwasababu amekuwa mwanafunzi muda mwingi yupo maktaba mkuu wangu
 
Back
Top Bottom