Elections 2015 Hongera Lowassa: Wewe ni bingwa wa siasa za Tanzania

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Nimeamini Lowassa ni bingwa wa siasa za Tanzania, na anastahili heshima,huyu mtu anajua kucheza na siasa zetu hadi maadui zake anawageuza na kuwafanya wafuasi wake watiifu.

Nani alitegemea Toka kashifa ya Richmond baada ya miaka nane Lowassa angekuja kuwa mkuu wa siasa za upinzani Tanzania, Mkuu wa wanasiasa wa upinzani Tanzania , Mkuu wa vyama vya upinzani Tanzania , Mkuu wa wale makamanda hatari wa kupiga vita ufisadi Tanzania ,Mbaya zaidi mgombea wao pekee na aliepita Bila kupingwa.?

Nani alitegemea leo Mbowe, Msigwa, Mdee na Lema wangepangiwa cha kuongea kwenye majukwaa ya kisiasa na Lowassa, nani alitegemea angetoa amri wafunge midomo kuhusu ufisadi na wakatii Bila shuruti, kwa hili Lowassa anastahili heshima ya kipekee hapa nchini.

Amewafanya maadui zake wamwombe radhi, wamsafishe , wamsujudu, wamtetemekee kiasi kwamba akitoa kauli inakuwa ndio sheria,na wanatiii Bila shuruti.

Hakuna heshima kubwa kama kumgeuza adui yako mkuu awe mfuasi wako mtiifu na mwaminifu kwako.

Naamini Lowassa alivyokatwa Dodoma alikata tamaa kabisa na siasa za Tanzania hasa kwenye URAIS,

Ila swala moja lilikuwa linamuumiza ni vipi atasafisha Jina Lake kupitia upinzani hasa Chadema ya Mbowe na Dr.Slaa, ili atakavyotulia kwenye ranch zake anakula mafao na wajukuu zake zisiwepo kelele za kumghasi.

Ndipo akajitoa mzima mzima kwenda Chadema kwa gharama zake na jamaa zake ambao amekuwa akichafuliwa nao siku zote. Lengo kumsafisha yeye na binafsi na jamaa zake hasa Rostam , Chenge, Karamagi nk.

Na kwa hilo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, japo itamuuma sana kumkosa mpiganaji namba moja wa ufisadi Tanzania Dr.Slaa, na huyu ndio lilikuwa lengo lake kuu, hakika Dr. Slaa angenasa kwenye mtego huu Lowassa angekua na amani maisha yake yote yaliyobaki duniani bahati mbaya Dr.slaa akashituka mapema.

Ila kwa sasa Lowassa ni kama ameteka kambi nzima ya maadui, ila kiongozi mkuu wa waasi Dr.Slaa ametoroka dakika za mwisho.

Baada ya Octoba 25 Lowassa atastaafu siasa na kwenda kupumuzika kwenye ranch zake na mahoteli yaliyoenea nchi nzima, huku akiwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kulipa kisasi na kuacha majeraha makubwa ndani ya Chadema na siasa za upinzani kwa ujumla.

Hongera Lowassa, Hatimaye sasa utapumzika kwa amani Bila bugudha, huku siasa za upinzani hasa Chadema zikiendelea kukupigia magoti kwa maumivu makali ya kutoaminika tena kwa wananchi hasa wapenda mabadiliko ya ukweli.!
 
IMG_20150513_192204 copy.jpg
 
Hujui ulichoandika eti baada ya kukatwa dodoma lowassa alikata tamaa. Kama ni mfuatiliaji wa siasa kwenye magazeti na humu jamvini mkakati wa lowassa kujiunga upinzani endapo angekatwa ulianza toka nyuma ya 2014. Inaelekea umemjua kwenye kutangaza nia ccm
 
Naona unatamani kuibadilisha bahari kua nchi kavu.. Kitu ambacho sio chakufikirika kirahic.. Aliekutuma mwambie watanzania wajana sio wa Leo
 
Na sasa hivi atakuwa MKUU WA NCHI....

Asante kwa mada yako ndefu, tuma salamu!
Ndoto ni ile ya usiku ila ya Mchana ni maruweruwe, vumilia kamanda Lowassa alikuja Chadema kwa kazi maalum na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom