Hongera Lowassa, Hongera UKAWA

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Hongera Lowassa, Hongera UKAWA. Pole sana CCM.
Nimesoma post nyingi sana za kukatisha tamaa kwenye jukwaa hili na kwingineko. Wengi wenu mnafikiri safari ya ukombozi ni sawa na kutembea kwa mguu toka Karimjee kwenda Ikulu. Wengine wananichekesha kuanza kudai ati ?sitapiga kura tena.? We mwehu au umetumwa!!! Sasa usipopiga kura ndio utakuwa unawakomoa usiowapenda? Wendawazimu wakubwa ni wale waoipongeza CCM kwa kushinda uchaguzi. Yaani, unaweza kumpongeza Magufuli kwa jambo moja tu, ?kufanikiwa kukanyaga Ikulu akiitwa rais. Huwezi kumpongeza kwa jambo lolote lingine. Mwenye kustahili pongezi katika uchaguzi huu ni Lowassa na UKAWA.

Wapo wana CCM wanaomcheka Lowassa kwa kuhama CCM na kugombea kupitia CHADEMA na mwisho kutangazwa amekuwa wa pili. Tume ya uchaguzi imempa Lowassa kura milioni sita. Wewe unayemkebehi Lowassa umewahi kushiriki uchaguzi wowote na kupata japo kura elfu mbili tu? Acha ujinga. Lowassa ameonesha kuwa anakubalika kuliko mtu mwingine yoyote Tanzania, na kauli yake inaogopewa sana, na ndio maana jeshi la polisi limeandikisha polisi wengi kuliko idadi. Wanaogopa. Neno moja tu la Lowassa linaweza kusababisha hata huyo mteule wa tume asiweze kuapishwa. Neno moja alilosema Lowassa, ?msifanye fujo na kuwapa sababu.? Ndio maana nasema hongera Lowassa.

UKAWA je, kwanini hongera? Kudadadeki! Hapo ndipo nasema HONGERA tena kwa herufi kubwa zaidi. Pamoja na waasisi kukimbia, UKAWA kamwe haijageuka kuwa ukiwa kama kiongozi mkuu wa CCM alivyosema katika moja ya mikutano. Kama unayesoma ujumbe huu ni mkazi wa Dar es salaam, basi kuna uwezekano kwa asilimia kubwa diwani wako ni UKAWA. Manispaa yako itaongozwa na UKAWA na hata Jiji la Dar es salaam huenda likabadilishwa jina na kuwa UKAWA CITY. Hakuna mwenye uwezo wa kuzuia jambo hilo. Pombe ataongoza toka Magogoni na kando yake tu, pale Karimjee; BENDERA za vyama vinavyounda UKAWA zitakuwa zinapepea, kando ya ile ya taifa au ya jiji. Hapo atakuwepo ?rais? wa Dar akimaliza kero za wananchi. Sasa unategemea wanaukawa waingiwe ukiwa kwa ushindi mkubwa kama huu? Nendeni Dodoma mkaipige hiyo minyimbo yenu ya TOT; kwani hapo Dar nani kaisoma namba? Na hata huko Dodoma, baadhi yao wamepisha siti ili UKAWA waweze kukaa; yaani kama vile mtoto wa shule anavyompisha siti mkubwa wake kwenye daladala. UKAWA anakaa na CCM anashika bomba, kisha atashuka tu kituo kinachofuata.

Ndugu zangu msiweke tena post za kusema pole au kukata tamaa. Wapeni pole hao waliopoteza dira. Unajua mabadiliko sio kuvuka kijito. Ni kuvuka mito, mabonde na bahari. Hapa safari ilipofika sio padogo na tafu ya Ngoyayi haikuwa haba. Wekeni sasa post za mikakati ya sasa na malengo ya kusonga mbele. Na hata kwenye uzi huu ningependa usiweke maneno mengi zaidi ya kusema HONGERA LOWASSA, HONGERA UKAWA.
 
Hongera Lowasa, kura milioni 6 si utani. Inaonyesha jinsi alivyokubalika na kuaminika.
Hivyo Slaa uchaguzi wa 2010 alifikisha kura ngapi?
 
Eti Lowassa anaogopwa, aogopwe na nani kwa utajiri wake au!
 
Hongera Ukawa. hongera Luwasa.hongera Mbowe. hongera Mbatia. hongera Maalimu Seif. Hongra NLD familia ya Makaidi pokeeni hongera kwa niaba Baba. hongera mleta mada. Mungu yupamoja nasi.
 
Mimi kura yangu haijapotea.Nina Diwani,Nina Kubenea,Thanks to Ngoyai.Hongera mimi, hongera CDM, hongera UKAWA.Pipoooooooooooooozzzz
 
Hongera Lowasa, kura milioni 6 si utani. Inaonyesha jinsi alivyokubalika na kuaminika.Hivyo Slaa uchaguzi wa 2010 alifikisha kura ngapi?
Teh teh! Endeleeni kijitekenya...
Uchaguzi mkuu 2010 Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa akitetea Kiti cha URAIS kwa kipindi cha pili alifikisha kura 5,276,827.Who know tena baada ya kuijongeza
 
Hongera Lowasa, kura milioni 6 si utani. Inaonyesha jinsi alivyokubalika na kuaminika.Hivyo Slaa uchaguzi wa 2010 alifikisha kura ngapi?
Slaa 2010 alipata kura 2,271, 941. Roughly in Kama Lowassa anakubalika mara Tatu zaidi ya Slaa.
 
Lowasa amepata kura milioni kumi. NEC imempa magufuli. Wabung wetu wengi sana wameshinda. NEC kwa maelekezo ya mkapa na kikwete wakiongozwa na makamba, wamezigawa kura zetu kwa ccm

CCm haijashina uchaguzi ila imelazimisha kututawala kwa mabavu. Liwalo na liwe.
 
bado zimeibiwa nyingi lakini amepata 6,000,000. Tulipwaya sana nakujiamani kupita kiasi ndio maana ikawa rahisi kutumia nguvu ya dola kutumaliza. Hapo ndio tulipo jisahau tu.
 
Lowasa amepata kura milioni kumi. NEC imempa magufuli. Wabung wetu wengi sana wameshinda. NEC kwa maelekezo ya mkapa na kikwete wakiongozwa na makamba, wamezigawa kura zetu kwa ccm

CCm haijashina uchaguzi ila imelazimisha kututawala kwa mabavu. Liwalo na liwe.
Haya ndiyo yalikuwa malengo ya Lowassa? Mbona ujasema waliojiandikisha wakati wa JK walikuwa watu wangapi na sasa hivi watu wangapi.
 
Haya ndiyo yalikuwa malengo ya Lowassa? Mbona ujasema waliojiandikisha wakati wa JK walikuwa watu wangapi na sasa hivi watu wangapi.


Mkapa, kikwete na makamba ni mahaini wamepindua nchi kwa kujitangazia utawala wa mabavu. Wanastahili kuondolewa kwa namna yoyote.
 
hongera mzee Lowasa Hongera ukawa. nawashukuru mmedumisha amani. Kura m6 na ushee si haba ukizingatia kuwa lazima kwenye ushindani apatikane mshindi
 
Back
Top Bottom