Hongera Lowassa, Hongera CCM kwa kukata ngebe

Ewassa ni jembe la ukweli la kuzolea mavi:crying:

Ha ha haaaaa, nimechekajeeeeee! Hili kweli jembe la kuzolea mavi! Huyu mtu hasafishiki hata kwa nini. Aje kifua mbele na atuambie Dowans / Richmond ni akina nani? Ni mwizi tu huyu, hafai hata kido, Nyerere alimkataa kabisa huyu, bora Dhaifu aliambia muda wake bado!
 
Mwee!
Mungu naye anapanga mengi, mpaka wanasiasa kuwa wa-NEC!
Tena wanasiasa wenyewe wa kile chama chetu cha mitikasi, mikakati na mizengwe; na ikipasa hata kutoleana bastola. Basi huyo mungu anaombwa awageukiye wale akinana wajawazito wanaolazwa mzungu wa nne kule hospitali mwananyama na kwingeneko.
Tafadhali asiwasahau wale watoto waloko kwenye majengo -wanasiasa wanayaita madarasa lakini hawana wa kuwafundisha, wala zana za maabara.
Vipi kwenye maji safi na salama -pia awakumbuke watazania wasokuwa na maji safi na salama ya kunywa.
Akawatembelee wagonjwa waloko mahospitalini ambao madaktari wanashindwa kuwahudimia kwa kukosa gloves, bandage nk.

Ewe Mungu, tafadhali geuza macho yako, achana na hao wachumia tumbo (wao wanajiita wanasiasa), geuka uwatizame walala hoi, ulowawakea madini ndani ya ardhi yao, ukaweka twiga na wengineo ktk mapori yao, lakini wachumia tumbo wameamua kugenisha kila kitu (wanaiita kubinafsisha).
 
Nina wasiwasi na kiwango chako cha kufikiria,hv kama una akili timamu unaweza kumfagilia mtu kama lowasa? nafikiri kuna haja ya kusali sana ili watu kama wewe mungu awape mwanga kwenye akili zao.
 
Tatizo lako wewe Pasco aka Pasc...wa Ma..... ni kuyakimbia maneno yako ambayo umewahi kuyaandika hapa siku za nyuma. Aliyeandika hapa kwamba Lowassa akiingia Ikulu labda nawe utapata japo kidogo mafuta uzuri si mwingine ni wewe.
Mkuu BAK, kiukweli, sijawahi kulipwa hata senti tano kumpigia debe EL, lakini kwa vile kuna watu wanaolazimisha lazima nalipwa, basi mimi huwajibu "ndiyo nalipwa" ili wajiridhishe!.

Naomba nikiri wazi kuwa mimi ni masikini na kuna kipindi nalala njaa kwa umasikini wangu, ila pamoja na umasikini huu, siendekezi njaa wala siuvalii kibwebwe umasikini huu ili nipate chochote!, mimi ni masikini jeuri, nalala njaa with smilling face!. Kwa vile kuna watu wamejiaminisha nautafuta U-DC, kiukweli kabisa toka ndani ya moyo wangu, sio tuu siuzimii U-DC, sijawahi hata kuutamani!.Ila watu wakilazimisha sana, huishia kuwapatia watakacho!.

Vivyo hivyo kwa EL, wale wanaolazimisha nayafanya haya kwa maslahi binafsi na sio maslahi ya taifa, then nawakubalia yaishe!.

Umewahi kuona ile scenario, mtoto anavunja glasi kwa bahati mbaya, mama kwa hasira, anamwambia "endelea kuvunja mpaka umalize zote!", vivyo hivyo wale wote mnaoamini mimi ni gamba, endeleeni kuamini mpaka pale mnakapo thibitisha, au kuamini vinginevyo!.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
TB Joshua yule mchawi aneyewachezea wajinga kwa mazingaumbwe ya mafuta ya mizaituni basi mnafurika kwenda kuangalia maigizo.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Kama ni kweli kama usemavyo, na unaamini hivyo, kwanini na wewe usitumie hayo mafuta kufanya mazingaombwe ili upate utajiri wa kutisha hata wa kumzidi Lowasa! Wacha talalila! Usichokiamini wewe, usimlazimishe na wengine kuwa wajinga kama wewe.Halafu kwa taarifa yako, TB Joshua hajawahi kutumia mafuta hata siku moja kwenye ibada zake. Inaonekana hata hujawahi kumwangalia, unamsikia tu!
 
Moja kati ya wachangiaji wanaonivutia JF ni pamoja na ndugu ya Pasco,huwa anachangia vizuri na ni moja kati ya active members wa JF,kingine kinachonivutia kwa huyu mwanajf ni kuamini SANA katika mawazo yake(of coz ni haki yake kikatiba),hv sasa anataka kutuaminisha kwamba katika CCM na TZ kwa ujumla hakuna chaguo bora na sahihi zaidi ya Mh. EL,kitu ambacho mimi sidhani kama ni SAHIHI.Kwangu mimi EL sio chaguo sahihi kwa sababu zifuatazo
  • Kutajwa kwake katika LIST OF SHAME na Dr.Slaa,tatizo langu mimi sio yeye kutaja,tatizo langu ni yeye kutokuchukua hatua zozote kukanusha tuhuma hizo ili kujisafisha cha fedheha hii ukichukulia heshima yake aliyoijenga kwa zaidi ya robo karne,hivyo basi kukaa kwake kimya wengi tunaamini tuhuma hizi ni UKWELI MTUPU hasa kwa heshima na umakini wa mtoa hiyo list...
  • Kutokuwa muumini wa DEMOKRASIA,.wote tunajua ya kwamba CCM imekuja na kauli mbiu/kauli mkakati ya KILIMO kwanza,kwa maana ndio maamuzi sahihi ya CCM hata kama yanaupungufu..nilitegemea kama kuna kasoro yoyote angepinga kwa hoja kwa vikao na sio kutoka hadharani,na kama hayo ndio yalikuwa ndio maamuzi ya wengi anatakiwa aheshimu,ndio demokrasia hiyo au AJITOE chamani,
  • Hakufanya jitihada za dhati kuzuia kashfa ya RICHMOND..Kwa mujibu wa ripoti ya Dr.Mwakyembe ni kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa wazi wa taratibu wakati wa mchakato wa zabuni,ilijitahidi vp kuzuia,ok anasema alimweleza mkubwa wake,lakini maamuzi yalibaki vilevile,je alichukua hatua gani kulipinga hilo,maana bila kelele za wananchi na kamati ya Mwakyembe ile ndio ilikuwa imetoka.....
Mwisho,hata ikitokea EL amekuwa Rais wa Tz,ni kwa kuwa waTz wengi wanauelewa mdogo juu ya elimu ya urais+nguvu ya fedha na dola ya CCM,ila sio kwamba yy ni BORA!
Nawasilisha
 
Mkuu Sophist, hadithi yako ilibaki kidogo tuu ifanane na ukweli kama usingegaribu na cooked data za bilioni 4 per day ya scratch vouchers!. Tanzania ina watu milioni 40 na kati ya hao wenye simu ni milioni 10 tuu wakigawana makampuni 7-Airtel, Tigo, Voda, Zentel, TTCL, Sasatel na BOL!. Alphatel ni moja kati ya 5 Super dealers wa Voda wakiongozwa na Shivacom!, sasa hao wateja wa vouchers wa wa ku roll 4bln per day kwa umasikini tulio nao wako wapi?.

Japo jina langu ndilo la kwanza kwenye ile payroll pale ofisini na kiukweli nimejitahidi sana ku recriut angalia sasa anavyong'arishwa!,Kwa nini wewe unataka kumpaka masizi?!.
Tafuta uongo mwingine!.
P .

Hello Pasco!
  1. Kazi ni kazi; hongera!
  2. Waulize wahasibu watakueleza, mauzo (sales turnover) siyo faida (markup/margin).
  3. Kama sales turnover ya Alphatel siyo 4/- billion ni ngapi?
 
Mkuu Pasco unajua siku hizi kuna viswahili vingi sana. Hebu fafanua ulipoandika hapa jamvini kwamba fisadi Lowassa akiingia Ikulu basi unaweza kuambulia kurushiwa mafuta uzuri ulikuwa una maana gani!?

Kwanini unampigia debe la nguvu mchafu fisadi Lowassa badala ya wale uliowasema ni wasafi ndani ya magamba akama akina Mwakyembe na Nahodha!?

Halafu tatizo lako weye hujibu maswali maana uliandika heri ya mwizi anayeleta maendeleo. Nikakuliiza katika wezi waliowahi kuingia Ikulu ni yupi aliyeleta maendeleo!? na maendeleo hayo yalipatikana katika nyanja (z)ipi!? (uchumi, afya, elimu, usafiri, huduma muhimu n.k.) lakini hadi sasa unalipotezea swali langu. Kama huna jibu si useme tu kwamba huna jibu badala ya kulipotezea!?


Mkuu BAK, kiukweli, sijawahi kulipwa hata senti tano kumpigia debe EL, lakini kwa vile kuna watu wanaolazimisha lazima nalipwa, basi mimi huwajibu "ndiyo nalipwa" ili wajiridhishe!.

Naomba nikiri wazi kuwa mimi ni masikini na kuna kipindi nalala njaa kwa umasikini wangu, ila pamoja na umasikini huu, siendekezi njaa wala siuvalii kibwebwe umasikini huu ili nipate chochote!, mimi ni masikini jeuri, nalala njaa with smilling face!. Kwa vile kuna watu wamejiaminisha nautafuta U-DC, kiukweli kabisa toka ndani ya moyo wangu, sio tuu siuzimii U-DC, sijawahi hata kuutamani!.Ila watu wakilazimisha sana, huishia kuwapatia watakacho!.

Vivyo hivyo kwa EL, wale wanaolazimisha nayafanya haya kwa maslahi binafsi na sio maslahi ya taifa, then nawakubalia yaishe!.

Umewahi kuona ile scenario, mtoto anavunja glasi kwa bahati mbaya, mama kwa hasira, anamwambia "endelea kuvunja mpaka umalize zote!", vivyo hivyo wale wote mnaoamini mimi ni gamba, endeleeni kuamini mpaka pale mnakapo thibitisha, au kuamini vinginevyo!.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom