Hongera Lowassa, Hongera CCM kwa kukata ngebe

Pasco,Nafahamu kuwa wewe ni mshauri (consultant) wa siasa na habari wa Edward Lowasa. Ila mwambie kuwa Mkuchika, Kinana, Bagenda na wengineo, rika lake la kisiasa waliokuwa wote ofisi ndogo ya makao makuu ya Tanu, wamekwishakusanya ushahidi dhidi ya Lowasa, ikiwa ni pamoja majumba yaliyokuwa ya Msajili wa Majumba aliyojimilikisha kila mkoa alipokuwa waziri wa ardhi ma maendeleo mijini (kwa sasa 'maendeleo ya makazi'). Katika hili, Richmond ni cha mtoto. Aidha kuna ushahidi (nakala ya minutes ipo kibindoni) wa Edward Lowasa kujimilikisha jengo la ofisi ya TANU katika mkoa fulani hapa nchini. Kama si taulo alilotupiwa na marehemu Sokoine tungekuwa tumemsahau Edward Lowasa zamani sana, katika siasa za Tanzania. Vilevile tunajua kuwa Edward Lowasa, kupitia kampuni yake binafsi ya Alfatel, anaingiza zaidi ya shilingi bilion 4 kwa siku kutokana na mauzo ya scratch vouchers za vodacom; mapato hayo hayalipiwi kodi. Pesa hizi ndizo zinazotumika kununua njia yake kupitia CCM kuelekea Ikulu. Tusubiri muda tu, tutamalizania naye. Hakikisha huachi arrears katika malipo yako vinginevyo unaweza kuwa miongoni mwa watakaokumbwa na kimbunga cha Lowasa bye-bye na kusaga meno siku zijazo (si nyingi).
Mkuu Sophist, hadithi yako ilibaki kidogo tuu ifanane na ukweli kama usingegaribu na cooked data za bilioni 4 per day ya scratch vouchers!. Tanzania ina watu milioni 40 na kati ya hao wenye simu ni milioni 10 tuu wakigawana makampuni 7-Airtel, Tigo, Voda, Zentel, TTCL, Sasatel na BOL!. Alphatel ni moja kati ya 5 Super dealers wa Voda wakiongozwa na Shivacom!, sasa hao wateja wa vouchers wa wa ku roll 4bln per day kwa umasikini tulio nao wako wapi?.

Japo jina langu ndilo la kwanza kwenye ile payroll pale ofisini na kiukweli nimejitahidi sana ku recriut angalia sasa anavyong'arishwa!,Kwa nini wewe unataka kumpaka masizi?!.
Tafuta uongo mwingine!.
P .
 
Mkuu Mwakyomwango, ni kweli EL ana mali nyingi kwa kiwango cha Mwalimu by then. Je, utapenda nikuorodheshee mali walizonazo hao viongoozi wa baada ya Mwalimu ili tuzilinganishe?.

Una taarifa by the time Mr. Clean anaondoka, Mwalimu angekuwepo, angeozea Segerea? Unazijua mali za Rukhsa? Au nikutajie mpaka mali za Dhaifu?.

Kwa kigezo cha mali CCM hakuna msafi. Uchafu valid ni wa Richmond ila hilo ni zigo la mtu tuu, yeye ni mbebaji tu, muda muafaka ukifika, atalitua zigo hilo na mtamtambua mwenye zigo lake.

P.

Mkuu hapo kwenye RED ni sababu tosha ya kutokuwa rais!

Lakini kwetu hasa Afrika tusivyojali siwezi shangaa lolote!
 
Kwani EL anakosa gani? Mimi ninachojua EL ndiye Raisi 2015.

Gazeti la SAUTI la 26/9/2012 limeeleza kuwa Mbowe na Slaa waanza kuhujumiana kwa kile kilichoelezwa kuusaka urais,zitto naye yuko kivyake,tena wabunge wameanza kugawanyika,soma gazeti la sauti la 26/9/2012 toleo la 210,kwaninin EL asiwapige bao? cdm nao bana.
 
wewe unachekesha kweli. wewe unaishi nchi gani?? kwa akili yako bado unashabikia hiki chama cha magamba na mafisadi wake?? ohhh Lowasa ohhh.. sijui takataka gani.... to hell.. watz tuna matatizo kibao.. tunateswa na ufuisadi waliousababisha wao.

badala ya kushabiia ujinga hebu jiulize nini chanzo cha umasikini tulionao

je??? baada ya miaka 50 ya uhuru

1.wewe unapata maji safi ya bomba kila siku?

2.watoto wako au ndugu yako jirani yako wanapata elimu bora au wnasoma shule ya kata?

3.barabara ya mtaani kwako ni ya rami??

4.hospitali unayotibiwa wewe ndugu yako jirani yako inatoa hudum stahiki??

5.unaishi kwenye nyumba bora anayostahili kuishi binadamu?? au uko kwenye mahema mabwepande??

6. una kipato hali kinachokutosheleza we na fmilia yako??

ukiisha kujiuliza hayo huwezi kuwashabikia hao jamaa zako na chama chao kwa jambo lolote wanalofanya.tunasubiri muda wao ufike waondoke tu
 
Mbona unaanza kuzua maneno ambayo mie sikuyaandika? Ni wapi nilipoaandika kwamba tumtafute mtakatifu atupeleke Watanzania peponi!? Hata Mwalimu hakuwa mtakatifu lakini uongozi wake kwa asilimia kubwa unakubalika na Watanzania wengi waliopata bahati ya kumfahamu na hata Walimwengu wengi walioomfahamu katika nchi mbali mbali duniani wanamkubali kwamba alikuwa kiongozi mzuri pamoja na kuwa hakuwa mtakatifu.

Katika mafisadi wote ndani ya magamba akiwemo fisadi Lowassa ni yupi ambaye ameweza kudeliver kwa vitendo!? maendeleo hayo yalikuwa delivered katika nyanja ipi? uchumi, afya, elimu, usafiri, huduma bora n.k.?

Mie naona madudu tu sioni maendeleo yoyote yale kama unavyodai wewe, kama kungekuwa na maendeleo Kikwete asingeitwa MSANII/DHAIFU. Yule fisadi Mkapa naye alikuwa busy kufanya biashara akiwa Ikulu na kujiuzia nyumba za Serikali, kujimilikisha migodi kwa njia za wizi, kuhusika katika kusaini mikataba ya uchimbaji wa madini yetu ambayo haina maslahi kwa Watanzania, kuhusika na wizi katika ununuzi wa rada na pia wizi mkubwa wa EPA uliofanywa akiwa mdarakani na kuuza mashirika mbali mbali nchini kwa bei ya kutupa. Yule Mwinyi naye hakufanya lolote la maana zaidi ya kujihusisha na udisadi. Sasa hayo maendeleo unayoyazungumzia yaliyoletwa na mwizi ni mwizi yupi huyo kati ya hao niliowataja hapo juu!?

Elimu yetu ni hovyo, afya nayo ni hovyo, uchumi nao ndio, umeme mwaka wa 20 sasa bado hauna ukakika, rasilimali zetu ikiwemo gas, dhahabu, almasi n.k. zinawaneemesha mafisadi Serikalini na wageni miaka nenda miaka rudi, sasa sijui wewe mwenzetu hayo maendeleo unayaona katika nyanja ipi hasa?

Tunamuona fisadi Lowassa akiwa amekazana kukimbia sakata la Richmond kwamba pamoja na kujiuzulu uwaziri mkuu lakini yeye hahusiki lakini yuko kimya kabisa kuonyesha msimamo wake kama anaunga mkono Richmond/Dowans wanastahili kulipwa $95 millioni. Yuko kimya kabisa kuhusu mikataba ya rasilimali zetu ambayo haina maslahi kwa Watanzania. Yuko kimya kabisa kuhusiana na wizi wa EPA, Meremeta, Kagoda.

Miaka yote aliyokuwa ndani ya Serikali hakufanya chochote kile kinachoonyesha kwamba anastahili kuiongoza nchi. Wizara zote alizowahi kushika utendaji wake ulikuwa ni wa kulegalega na hata alipokuwa Waziri Mkuu pia. Eti akathubutu kuita "wataalamu" toka Thailand waje kututengenezea mvua!!!!

Ukibahatika kumuona mwambie Watanzania wengi tungependa kumuuliza yafuatayo.

1. Je, utajiri wake ni wa halali? Alifanya biashara zipi zilizomuwezesha kuwa bilionea? kuanzia lini?
2. Mbona anakuwa kimya kupita kiasi kwenye mambo mbali mbali ambayo yanatukera mno Watanzania kama mikataba isiyo na maslahi, mafisadi ndani ya Serikali ambao sheria zinapindishwa na hivyo kutochukuliwa hatua zozote zile za kisheria.
3. Anaunga mkono Dowans walipwe $95 million au la?
4. Ana maoni gani kuhusiana na mafisadi mbali mbali wakiwemo wa EPA, Meremeta, Kagoda, Rada, Kiwira Coal Mining wakiwemo Mkapa na Chenge kutopandishwa kizimbani ili kujibu tuhuma za ufisadi dhidi yao?
5. Kwanini anang'ang'ania kuwa Rais 2015?

Achana na mambo ya kuwa mcheza sinema na kuja kuwapamba mafisadi, kuwarembaremba na kuwasifia bila kuangalia mabaya yao mbali mbali ili wakifanikiwa tu basi wakurushie nawe mafuta uzuri ili unukie.

Kauli zako zinabadilika kama kinyonga. Mara mie Mtanzania sina chama sasa hivi nimeamua kuweka mbele maslahi ya nchi yangu, siku chache baadaye unarudi hapa jamvini kuendeleza ucheza sinema wako wa kumsifia mfalme wako, kumpamba, kumrembaremba n.k. katika juhudi za kumfanya mfalme wako fisadi Lowassa achekelee.

Lowassa ni fisadi hafai kabisa kukabidhiwa nchi 2015. Makosa yaliyofanyika kwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete ndiyo yanaiangamiza nchi yetu sasa hivi kamwe tusikubali kuyarudia makosa yale. Hivyo ni lazima tuwe tayari kuuliza maswali mazito na kuonyesha misimamo yetu thabiti ili fisadi mwingine asiingie Ikulu 2015 na hivyo kuendeleza kuiangamiza nchi.



Mkuu BAK, kwani tunamtafuta rais mtakatifu atuendeshee ibada ili Watanzania wote twende peponi?, au tunatafuta rais mwenye uwezo wa kuongoza vita dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi?!. Kwani ufisadi is a big problem?!.

Kama ni utakatifu angekuwa Nyerere!, mpaka sasa ndio kwanza tuko kwenye mchakato wa kuntangaza "Mwenye Heri", mpaka aje kuwa Mtakatifu ni leo?!.

CCM are all devils, but between the two devils, choose the lesser!. Hivi kati ya mwizi anaye deliver development kwa vitendo na mtakatifu anaye hubiri development kwa maneno matupu, utamchagua nani?. Hivi ni nani afadhali kati ya EL ameiba ila ametumia proceeds za huo wizi kufanya mambo!, ama dhaifu aliyeisanehe mijizi ya EPA kwa kiini macho cha kurejesha walichokwiba and nothing was done?!.
 
hivi kwa ccm hakuna mtu mwingine kijana msafi mwenye nguvu, mbunifu anayekubalika ambaye mnaweza kumuandaa kugombea urais 2015 zaidi ya mzee Lowassa? Lakini huenda yanatimia maana mkisukumwa na ulevi tu ulevi wa madaraka na rushwa mkamuweka Lowassa kuwa mgombea utabiri wa Anguko la ccm utatimia maana wananchi wanamjua lowassa fika kwa kashfa ya Richmond hatauzika hivo chadema njia itakuwa rahisi mno!!!
CCM inawenyewe, panga pangua, piga ua wao wamo. Lowasa, Riz1, Chenge. Salma
 
CCM inawenyewe, panga pangua, piga ua wao wamo. Lowasa, Riz1, Chenge. Salma

ndio walimuingiza vasco madarakani(chenge na lowassa) hawezi kuwafanya kitu! salma ni mke akifanya chochote nyumbani kutachimbika, na riz 1 ndio mrithi wa kitu cha ufalme(crowned prince)!!
 
Lowasa ndiyo CCM yenyewe bila yeye hamna CCM pale.

Ni mawazo yangu tu lakini manake nape anaweza kuniponda mawe.
 
hivi kwa ccm hakuna mtu mwingine kijana msafi mwenye nguvu, mbunifu anayekubalika ambaye mnaweza kumuandaa kugombea urais 2015 zaidi ya mzee Lowassa?
Jamaa wameishiwa, utawasikia wale wale tu, kifupi hawana jipya!!!
 
Kwani kupitishwa kugombea U-NEC ndo kunamfanya asiwe fisadi? Jizi ni jizi tu hata likipitishwa kugombea U-CCM.
 
Mkuu Mwakyomwango, ni kweli EL ana mali nyingi kwa kiwango cha Mwalimu by then. Je, utapenda nikuorodheshee mali walizonazo hao viongoozi wa baada ya Mwalimu ili tuzilinganishe?.

Una taarifa by the time Mr. Clean anaondoka,walimuangekuwepo, angeozea Segerea? Unazijua mali za Rukhsa? Au nikutajie mpaka mali za Dhaifu?.

Kwa kigezo cha mali CCM hakuna msafi. Uchafu valid ni wa Richmond ila hilo ni zigo la mtu tuu, yeye ni mbebaji tu, muda muafaka ukifika, atalitua zigo hilo na mtamtambua mwenye zigo lake.

P.

Na ndio maana hawafai wote akiwemo Lowasa, Sita, Mwakyembe, Asha Rose migiro na wengine wote. Yaani nmtu yeyote kutoka ccm ni choo cha Rushwa.
 
hatulinganishi ni mwanaccm gani amejilimbikizia kiasi gani bali je kuna mtu msafi aliyebaki ndani ya ccm?
 
Mimi sina Jazba naomba unijibu hiki
Ni nini kilimuondoa Mbowe katika kinyang`anyilo cha uraisi mapema 2010?
Ni nini kilimuondo Zitto katika kinyang`anyilo cha uwenyekiti wa CDM?
Ukijibu kwa ufasaha nitakujibu vizuri.
Dah! Nimegundua tuko viwango tofauti mno kwenye masuala haya. CHADEMA ilimsimamisha Dr Slaa kama mgombea wao wa URAIS 2010. Sio Mbowe. Zitto aliondoa jina lake mwenyewe baada ya kushauriana na wazee wa chama chake. Nijibu swali langu sasa.
 
Dah! Nimegundua tuko viwango tofauti mno kwenye masuala haya. CHADEMA ilimsimamisha Dr Slaa kama mgombea wao wa URAIS 2010. Sio Mbowe. Zitto aliondoa jina lake mwenyewe baada ya kushauriana na wazee wa chama chake. Nijibu swali langu sasa.

Tatizo lako hupitii comment check juu nimeshakujibu vizuri.
 
Ninachojua kimoja tu EL Raisi 2015 nyie pigeni kelele tu.

Mpaka sasa ninaamini kabisa kuwa Mkweree na genge lake hawana ubavu wa kumzuia fisadi papa yeyote kupeperusha bendera ya ccm 2015; ingawa hatashinda urais hata kwa kuchakachua!!
 
Mkuu Mwakyomwango, ni kweli EL ana mali nyingi kwa kiwango cha Mwalimu by then. Je, utapenda nikuorodheshee mali walizonazo hao viongoozi wa baada ya Mwalimu ili tuzilinganishe?.

Una taarifa by the time Mr. Clean anaondoka, Mwalimu angekuwepo, angeozea Segerea? Unazijua mali za Rukhsa? Au nikutajie mpaka mali za Dhaifu?.

Kwa kigezo cha mali CCM hakuna msafi. Uchafu valid ni wa Richmond ila hilo ni zigo la mtu tuu, yeye ni mbebaji tu, muda muafaka ukifika, atalitua zigo hilo na mtamtambua mwenye zigo lake.

P.
Acheni kupiga mayowe mwizi wa kuku ni yule aliyekamatwa na kuku,jamaa yenu "maamuzi magumu" hasafishiki hata kwa dodoki la chuma,mwizi mkubwa na NEC ataisiki kwenye bomba kwa taarifa za kiinntelijensia atasambaratishwa kama watu wake ambaomajina yao hayakurudi kwenye hatua hii mnayopongezana yeye "kupitishwa"
 
TB Joshua yule mchawi aneyewachezea wajinga kwa mazingaumbwe ya mafuta ya mizaituni basi mnafurika kwenda kuangalia maigizo.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums


"WAJINGA NDIO WALIWAO", hata yule bibi Joyce Banda wa Malawi nae anamuabudu mchawi wa mazingaombwe yule!!
 
Jazba ya nini acha ukali kitu gani kimekukasilisha? Pole pole.

1. Kumbuka wagombea uraisi wakati huo walikuwa wanapendekezwa from Usalama wa Taifa.
2. Mtei walihitirafiana na Nyerere katika masuala fulani fulani na mtei akaamua kuachia ngazi,vilevile kwa Lowassa ilikuwa ni personal interest ya Nyerere wakati ule kuwa Kikwete awe raisi lakini kwa sababu UWT walikuwa wamemuandaa Mkapa basi mkapa akiteuliwa kugombea. Nadhani unanielewa mpaka hapo. Kumbuka wakati ule Lowassa alikuwa yuko ndani ya CCM na Nyerere akiwamo. Kama angekuwa Lowassa Mchafu so angeondolewa kwenye chama na Nyerere mwenyewe.

Isitoshe Lowassa alikuwa na cheo kikubwa tu ndani ya chama na serikali. Mimi ninajiuliza watu wanapokomalia hili hawatumii hata akili kidogo.

Mfano akina Kambona waliondolewa kwenye chama kabisa.
Lowassa ni Matunda mazuri ya Nyerere yaliyopikwa yakaiva. wameiva kisiasa wanaujuzi na nchi yetu.
Mbona umeongopa sana kama hili ndilo jibu! Ni kama vile hauna unachokifahamu kwa siasa za TANZANIA.
 
Mbona umeongopa sana kama hili ndilo jibu! Ni kama vile hauna unachokifahamu kwa siasa za TANZANIA.

Basi kaa vivyo lakini ujue kuwa Lowassa 2015 ni raisi. Is the best than any one in our country.
 
Back
Top Bottom