Hongera Lowassa, Hongera CCM kwa kukata ngebe

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Nimekuwa nikifuatilia sana siasa za ndani ya nchi yetu. Katika kipindi hiki hadi tarehe 12-11-2012 siku ambayo itakuwa ni mwisho wa uchaguzi wa ndani wa CCM(kama ratiba inavyoonesha), mengi yamesemwa juu ya hatma ya CCM na baadhi ya wagombea.

Kama kuna mgombea aliyesemwa sana katika mchakato huu, si mwingine bali ni mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa. Wapo waliokuwa wanasema, mabadiliko ya katiba ya CCM yalikuwa na lengo la kumwondoa/ kumzibia njia Lowassa. Waswahili wana msemo wao wa busara kabisa kuwa "wa mbili ni wa mbili, havai moja" na wengine husema "lililopangwa na Mungu, binadamu hawezi kulipangua" na pia "asiyekuwemo haingii, na aliyemo hatoki". Kusemwa kwa Lowasa ni muendelezo wa siasa za CCM kuelekea 2015. Binafsi hajaweka wazi kama atagombea urais 2015, na kila anapoulizwa husema "tutavuka daraja pindi tutakapoufikia mto"

Vikao vya uamuzi vya CCM vimemalizika. Jina la Lowassa limepitishwa kugombea nafasi ya U-NEC kupitia wilaya yake ya Monduli. Pamoja nae wapo Dr Salash Toure na kijana Nanai Konani. Mi si mtabiri wa kujua nani atafanikiwa kuwa M-NEC kutoka Monduli, ila ninachoweza kusema ni kuwa CCM wamekata ngebe za watu waliokuwa wanavumisha taarifa za uongo kuwa mwisho wa Lowasa katika siasa za CCM umefikia, kwa kuwa hataruhusiwa kugombea ujumbe wa NEC. Wapo wanaosema kuwa CCM imekata majina ya wagombea U-NEC wengi waliokuwa wanamtandao wa Lowasa. Inawezekana habari hii ikawa kweli, maana wanaojua ni CCM wenyewe. Ila tukumbuke kuwa: KAMA IPO, IPO TU

Nimalizie kusema kuwa "chochote tulicho nacho, hatujapata kwa ujanja wetu, bali ni makusudi ya Mungu". Kama Mungu amepanga Lowasa kuwa M-NEC atakuwa tu. Na kama amepanga Lowasa kuwa Rais, atakuwa tu. Hakuna wa kuzuia mipango ya Mungu.
 
hivi kwa ccm hakuna mtu mwingine kijana msafi mwenye nguvu, mbunifu anayekubalika ambaye mnaweza kumuandaa kugombea urais 2015 zaidi ya mzee Lowassa? Lakini huenda yanatimia maana mkisukumwa na ulevi tu ulevi wa madaraka na rushwa mkamuweka Lowassa kuwa mgombea utabiri wa Anguko la ccm utatimia maana wananchi wanamjua lowassa fika kwa kashfa ya Richmond hatauzika hivo chadema njia itakuwa rahisi mno!!!
 
Sababu za lowa hasa kukataliwa na Nyerere mwaka 1995 hazijapitwa na wakati. Moja kati ya sababu hizo ni pamoja na kujilimbikizia mali za walala hoi ambazo alishindwa kueleza jinsi alivyozipata. ukumbuke vilivile mzimu wa rich monduli bado unamwandama huyo lowa hasa wako. Kama wewe ni mshauri wake, mwambie asipoteze muda wake kugombea urais kwani yeye ni mchafu na hasafishiki kwa sabuni iwayo yoyote ile.
 
Ole wao walitajalo jina la bwana Mungu bure....
Mungu yupi unayemsema...??? Ana haki kugombea ila si kwa maelezo yako haya.....
Another ROTTEN MINDS & LIVING NIGHTMARE.....
 
alisha waeleza mwenye ushahidi wa jambo lolote lile atoke mbele,wapi hakuna mtu aliyejitokeza,mwacheni mzee wa monduli atumie nafasi yake kikatiba
 
Mkuu Mwakyomwango, ni kweli EL ana mali nyingi kwa kiwango cha Mwalimu by then. Je, utapenda nikuorodheshee mali walizonazo hao viongoozi wa baada ya Mwalimu ili tuzilinganishe?.

Una taarifa by the time Mr. Clean anaondoka, Mwalimu angekuwepo, angeozea Segerea? Unazijua mali za Rukhsa? Au nikutajie mpaka mali za Dhaifu?.

Kwa kigezo cha mali CCM hakuna msafi. Uchafu valid ni wa Richmond ila hilo ni zigo la mtu tuu, yeye ni mbebaji tu, muda muafaka ukifika, atalitua zigo hilo na mtamtambua mwenye zigo lake.

P.
 
Lowasa na chama cha mapinduzi atakuwa rais au watatwaa rais baada ya hiki kizazi kupita ,ufisadi wa ccm hauvumiliki tena! Na hii tz ingekuwa kama nchi za kiarabu ungekuta tunaongea memgine sisi tuna Amani ya kijinga!
 
Lowasa na chama cha mapinduzi atakuwa rais au watatwaa rais baada ya hiki kizazi kupita ,ufisadi wa ccm hauvumiliki tena! Na hii tz ingekuwa kama nchi za kiarabu ungekuta tunaongea memgine sisi tuna Amani ya kijinga!
Ninachojua kimoja tu EL Raisi 2015 nyie pigeni kelele tu.
 
Mkuu Mwakyomwango, ni kweli EL ana mali nyingi kwa kiwango cha Mwalimu by then!. Jee utapenda nikuorodheshee mali walizonazo hao viongoozi wa baada ya Mwalimu ili tuzilinganishe?!. Una taarifa by the time Mr. Clean anaondoka, Mwalimu angekuwepo, angeozea Segerea?!. Unazijua amali za Rukhsa?. Au nikutajie mpaka mali za Dhaifu?!.

Kwa kigezo cha mali CCM hakuna msafi!. Uchafu valid ni wa Richmond ila hilo ni zigo la mtu tuu, yeye ni mbebaji tuu!, muda muafaka ukifika, atalitua zigo hilo na mtamtambua mwenye zigo lake!.
P.
acheni kutuzuga muda gani anangoja kama mzigo si wake si na aseme sasa hivi?ccm wote wezi tu !
 
TB Joshua unamuingizaje huku, wewe ni nani unayemuhukumu Mtumishi wa Mungu, unajua nini wewe kuhusu Mungu wa kweli na nguvu za Mungu, Mungu unayemjua na kumuamini wewe ni Mungu yupi? Unajua nini wewe kuhusu TB Joshua Ministry (SCOAN)?.
TB Joshua yule mchawi aneyewachezea wajinga kwa mazingaumbwe ya mafuta ya mizaituni basi mnafurika kwenda kuangalia maigizo.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
PASCO hebu tutajie bana tuone hizo nyeti ulizo nazo kuhusu viongozi wetu! Au na wewe unatishia kama MWEPESI?
 
Back
Top Bottom