don-oba
JF-Expert Member
- Dec 8, 2011
- 1,387
- 677
Pamoja na kwamba umeshika nafasi ya pili, umeonesha uwezo mkubwa wa kujieleza na kujibu maswali ya wabunge. Kumbuka mfumo dume bado umetawala sana ktk nyanja za kiungozi. Kura ulizopata ni ushindi tosha. Hongera sana Mh Leticia Nyerere.
Kulikuwa na uchaguzi wa Muwakilishi wa Bunge la Tanzania katika jumuiya ya SADC, sasa mmoja wa wagombea hao alikuwa ni LETICIA NYERERE. Ni miongoni ama yawezekana ndiye aliyeweza kujieleza vyema zaidi na amejipambanua kuwa bora kabisa miongoni mwa wagombea. Sasa kutokana na mfumo dume katika politiki zetu, na uchama KURA ZA NDIYO kwa LETICIA NYERERE hazikutosha kumpa nafasi hiyo ya uwakilishi. Ndiyo msingi wa mleta uzi kumtia moyo kwamba bado yeye ni MSHINDI japo sanduku la kura halikumbeba. Nawasilisha !!
Kwa ufupi, leo bungeni ulikuwa na uchaguzi wa mwakilishi wa bunge la Tanzania katika SADC Parliamentary Forum (SADC PF), na wabunge waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ni Selemani Jafo (Kisarawe-CCM), Laurencia Bukwimba (Busanda-CCM), na Leticia Nyerere (Viti Maalum-CHADEMA). Lugha ya kujieleza na kuomba kura ilikuwa ni Kiingereza. Akaanza Selemani Jafo, akaanza kuongea vizuri lakini kadiri muda ulivyokuwa unaendelea akawa anapoteza muelekeo na lugha ikawa inachangia kumpoteza kwani 'the, the, the' zikawa nyingi na hata kuonekana kweli kiingereza ni tatizo. Akafuata Leticia Nyerere, na wakati akienda wabunge wakawa wanaanza kucheka, bila shaka wakiwa wanaifahamu lafudhi yake, sasa sijui kwa kiingereza itakuwaje (hata mimi nilikuwa najua sasa dada anaumbuka). Heee! Mambo yakawa tofauti kabisa alipoanza kujieleza, yaani Leticia ameongea vizuri tena kwa lafudhi ya London, akajinadi, akaomba kura na akajibu maswali matatu kwa umahiri kabisa. Hapa hadi wabunge wa CUF niliona wanamshangilia! Ndipo akamalizia dada Lolensia Bukwimba. Huyu ndio aliyempa credit Leticia. Bukwimba alikuwa anaongea kiingereza kibovu au tuseme cha wastani kisichokuwa professional, chenye tasfiri ya moja kwa moja kutoka kiswahili kwenda kiingereza (siyo ya kimantiki), na alifunga kazi kwa kutojibu swali aliloulizwa badala yake akatoa maelezo yaliyo general kuhusu SADC.
Kama upigaji kura ungekuwa fair kuzingatia uelewa wa SADC PF na kujieleza, basi binafsi ningetoa hivi:
Leticia Nyerere 45%, Selemani Jafo 35% na Lorensia Bukwimba 20%.
Lakini kwa kuwa wanaopiga kura hawazingatii hayo, niliondoka kabla sijasikia matokeo, lakini nilikuwa najua Leticia hatachaguliwa kutokana na chama chake, Lorensia hatachaguliwa kutokana na kushindwa kujieleza, na nilijua Jafo atashinda kwani ndiye aliyebaki wa wastani hivi