Hongera Leticia Nyerere...

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,387
677
Pamoja na kwamba umeshika nafasi ya pili, umeonesha uwezo mkubwa wa kujieleza na kujibu maswali ya wabunge. Kumbuka mfumo dume bado umetawala sana ktk nyanja za kiungozi. Kura ulizopata ni ushindi tosha. Hongera sana Mh Leticia Nyerere.

Kulikuwa na uchaguzi wa Muwakilishi wa Bunge la Tanzania katika jumuiya ya SADC, sasa mmoja wa wagombea hao alikuwa ni LETICIA NYERERE. Ni miongoni ama yawezekana ndiye aliyeweza kujieleza vyema zaidi na amejipambanua kuwa bora kabisa miongoni mwa wagombea. Sasa kutokana na mfumo dume katika politiki zetu, na uchama KURA ZA NDIYO kwa LETICIA NYERERE hazikutosha kumpa nafasi hiyo ya uwakilishi. Ndiyo msingi wa mleta uzi kumtia moyo kwamba bado yeye ni MSHINDI japo sanduku la kura halikumbeba. Nawasilisha !!
Kwa ufupi, leo bungeni ulikuwa na uchaguzi wa mwakilishi wa bunge la Tanzania katika SADC Parliamentary Forum (SADC PF), na wabunge waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ni Selemani Jafo (Kisarawe-CCM), Laurencia Bukwimba (Busanda-CCM), na Leticia Nyerere (Viti Maalum-CHADEMA). Lugha ya kujieleza na kuomba kura ilikuwa ni Kiingereza. Akaanza Selemani Jafo, akaanza kuongea vizuri lakini kadiri muda ulivyokuwa unaendelea akawa anapoteza muelekeo na lugha ikawa inachangia kumpoteza kwani 'the, the, the' zikawa nyingi na hata kuonekana kweli kiingereza ni tatizo. Akafuata Leticia Nyerere, na wakati akienda wabunge wakawa wanaanza kucheka, bila shaka wakiwa wanaifahamu lafudhi yake, sasa sijui kwa kiingereza itakuwaje (hata mimi nilikuwa najua sasa dada anaumbuka). Heee! Mambo yakawa tofauti kabisa alipoanza kujieleza, yaani Leticia ameongea vizuri tena kwa lafudhi ya London, akajinadi, akaomba kura na akajibu maswali matatu kwa umahiri kabisa. Hapa hadi wabunge wa CUF niliona wanamshangilia! Ndipo akamalizia dada Lolensia Bukwimba. Huyu ndio aliyempa credit Leticia. Bukwimba alikuwa anaongea kiingereza kibovu au tuseme cha wastani kisichokuwa professional, chenye tasfiri ya moja kwa moja kutoka kiswahili kwenda kiingereza (siyo ya kimantiki), na alifunga kazi kwa kutojibu swali aliloulizwa badala yake akatoa maelezo yaliyo general kuhusu SADC.

Kama upigaji kura ungekuwa fair kuzingatia uelewa wa SADC PF na kujieleza, basi binafsi ningetoa hivi:
Leticia Nyerere 45%, Selemani Jafo 35% na Lorensia Bukwimba 20%.
Lakini kwa kuwa wanaopiga kura hawazingatii hayo, niliondoka kabla sijasikia matokeo, lakini nilikuwa najua Leticia hatachaguliwa kutokana na chama chake, Lorensia hatachaguliwa kutokana na kushindwa kujieleza, na nilijua Jafo atashinda kwani ndiye aliyebaki wa wastani hivi
 
nami nimeona - zaidi ya mfumo dume bila shaka UCHAMA zaidi. Huyu angeunguruma kule na ulimwengu ukajua Mtanzania kaingia
 
Pamoja na kwamba umeshika nafasi ya pili, umeonesha uwezo mkubwa wa kujieleza na kujibu maswali ya wabunge. Kumbuka mfumo dume bado umetawala sana ktk nyanja za kiungozi. Kura ulizopata ni ushindi tosha. Hongera sana Mh Leticia Nyerere.

Ndugu don-oba hapo hujafanya mawasiliano yeyote na sisi wengine. Una assume tulikuwa wote sasa unatoa maoni yako!!!! Very bad.

.
 
Last edited by a moderator:
nami nimeona - zaidi ya mfumo dume bila shaka UCHAMA zaidi. Huyu angeunguruma kule na ulimwengu ukajua Mtanzania kaingia

Mkuu, mpaka kufikia hapa tulipo ni hatua kubwa... hicho chama kiko mguu mmoja nje na siku ya ulimwengu kuona ukweli iko karibu sana.
Hongera sana Leticia Nyerere!
 
Kwa kweli amejitahidi sana kama siyo ukiritimba wa wabunge wa nyinyim ilikuwa ni nafasi yake
 
kwani alikuwa anagombea nini na wapi? embu mwenye habari iliyonyooka atudadavulie hapa
 
Bora thread ifutwe kuna wengine hatukufuatilia tukio hilo, haina maana kabisa kuleta taarifa nusunusu kama kwamba wote tulikuwa tunaangalia bunge.
 
kashika nafasi ya pili wapi?

toeni habari iliyokamilika ndo malengo ya jukwaa hili na si nusunusu kama ulivyofanya.
 
Pamoja na kwamba umeshika nafasi ya pili, umeonesha uwezo mkubwa wa kujieleza na kujibu maswali ya wabunge. Kumbuka mfumo dume bado umetawala sana ktk nyanja za kiungozi. Kura ulizopata ni ushindi tosha. Hongera sana Mh Leticia Nyerere.
Ujinga huu, unadhani JF inapatikana kariakoo na manzese peke yake? hivi una uelewa wowote wa Public relation? unaamini kabisa hapa umehabarisha umma? hovyooo!!
 
Ujinga huu, unadhani JF inapatikana kariakoo na manzese peke yake? hivi una uelewa wowote wa Public relation? unaamini kabisa hapa umehabarisha umma? hovyooo!!

Tusimlaumu sana hebu ngoja tuone kama ata respond atujuze, asiporudi hapa ujue alikuwa amelala.
 
Pamoja na kwamba umeshika nafasi ya pili, umeonesha uwezo mkubwa wa kujieleza na kujibu maswali ya wabunge. Kumbuka mfumo dume bado umetawala sana ktk nyanja za kiungozi. Kura ulizopata ni ushindi tosha. Hongera sana Mh Leticia Nyerere.

Ndio hapo Mnapofanya MAKOSA; Mnahisi na kuifanya JAMII FORUMS kama ni LOCAL entity... kila MMOJA wetu anaisoma na kuona MATUKIO MBALIMBALI NCHINI... Mmesahau kua JAMII FORUMS ni GLOBAL entity...

Kuna wanachama wako kona zote duniani... na HABARI yako FUPI na isiyoeleweke MODS wanaiacha kuzidi kutuchanganya; lakini tungekuwa ni sisi tunachangia habari pamoja na kuwa mbali... Tunapata Treatments tofuati

OMBI; Jaribu kuweka habri kamili ili wote tunufaike; Kama Umeshindwa basi USIANDIKE...
 
Kulikuwa na uchaguzi wa Muwakilishi wa Bunge la Tanzania katika jumuiya ya SADC, sasa mmoja wa wagombea hao alikuwa ni LETICIA NYERERE. Ni miongoni ama yawezekana ndiye aliyeweza kujieleza vyema zaidi na amejipambanua kuwa bora kabisa miongoni mwa wagombea. Sasa kutokana na mfumo dume katika politiki zetu, na uchama KURA ZA NDIYO kwa LETICIA NYERERE hazikutosha kumpa nafasi hiyo ya uwakilishi. Ndiyo msingi wa mleta uzi kumtia moyo kwamba bado yeye ni MSHINDI japo sanduku la kura halikumbeba. Nawasilisha !!
 
mkoritho umejitahidi kuelezea ila bado hujatuma nyma kamili, na nani alichukua nafasi ya kwanza, maana mleta mada kakimbilia kupost ili awe wa kwanza akizani yupo shule.
 
Back
Top Bottom