Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,502
- 4,408
Binafsi nimeshangazwa na ukimya wa wapinzani baada ya tukio la kuungua moto soko la Karume. Sijasikia pole yoyote kutoka kwa upinzani si CHADEMA wala ACT walioneshwa kusikitishwa na jambo hilo. Ni kimya kikuu kimetanda.
Ni wapinzani hawa hawa ambao polisi wakidhibiti mikusanyiko yao haramu wanapiga kelele na pengine hao waliounguliwa wakiwashawishi kushiriki lakini walipounguliwa soko wapo kimya. Kwa nini?
Kinachonishangaza, Mwenyekiti wa CCM alipoonesha yupo pamoja nao wamejazwa mitandaoni kuonesha hakuwa pamoja nao toka mwanzo kitu ambacho si kweli.
Je, kulikuwa na mpango gani uliopangwa na kuungua kwa soko la karume? Je, ni kwa nini maamuzi ya Mwenyekiti wa CCM yameonesha kuwakera wapinzani? Je, ni kwa nini hawajaonesha kusikitishwa na kuungua kwa soko la karume?
Wapinzani walikuwa wanataka sababu ya kusema wamekosa. Wapinzani walitengenezea jamii mtazamo hasi juu ya kuungua kwa masoko kwamba ni kazi ya 'kupangwa kutokea ndani' ili kuwaondosha. Wapinzani walisambaza taarifa za uzushi na uongo kwamba karume amepewa mwekezaji.
Wapinzani walifanya hayo yote kwa mtazamo wa kutengeneza chuki. Walitaka wasikie taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wetu kwamba wamachinga hawatakiwi tena karume lakini haikuwa hivyo.
Walifurahi kuona wakiandamana lakini haikuwa hivyo, ukimya wa upinzani ulikuwa na mengi yasiyoelezeka ila yote kwa yote Mungu amemjalia hekima Rais wetu kwa kuamua kwa utashi.
Tunampongeza sana Rais wetu kwa maamuzi ya hekima na busara iliyotumika kufika muafaka. Ameonesha kuwa ni mfariji katika mengi. Ametufariji na kututia moyo.