Hongera kwa kufaulu karibu chuo kikuu

mwanakijiji lugusi

Senior Member
Apr 13, 2016
128
225
HONGERA KWA KUFAULU! KARIBU CHUO KIKUU.

(Fikisha ujumbe huu kwa wadogo zetu 1year watarajiwa.)

Karibu Chuo Kikuu mdogo wangu!
Hiki ndio kile chuo ulichokua ukikitamani siku zote...hongera na karibu sana.
SI ULISIKIA KUNA BATA!?

Hili ndilo eneo pekee wanafunzi wanaingia darasani Kwa kupenda kwani hamna fimbo..karibu sana mdogo wangu..
Hili ndilo eneo pekee penzi hununua taaluma,nakutia moyo utashinda mdogo wangu

Hili ndilo eneo pekee watu wanapochagua kusoma vitu virahisi hata kama viko nje ya ndoto zao ilimradi ni virahisi tu watasoma..usijali wapotezee
Hili ndilo eneo pekee wanafunzi wanaruhusiwa kuoana watakavyo.karibu sana mdogo wangu jisikie uko batani.

Hili ndilo eneo pekee watu huja na Biblia/Quran kwenye beg alafu baada ya wiki mbili vitabu hivyo huhifadhiwa kabatini na begi huwekwa condom za kutosha kazi. Ni maamuzi yako mdogo wangu jisikie uko batani.

Hili ndilo eneo pekee kunakua na show nyingi za Bongofleva na dada zetu huingia bure ili wawe wengi huku kaka zetu wakitoa kiingilio Kwa niaba yao...karibu sana mdogo wangu jisikie uko batani.

Hili ndilo eneo pekee wadada wengi wanakuja weusi wanatoka weupe pasina shaka ni kiwanda cha rangi mdogo wangu.

Hili ndilo eneo pekee watu huwaacha wapenzi wao wa zamani kisa wamepata wasomi wenzao,usijali mdogo wangu jisikie uko batani.

Hili ndilo eneo pekee wanafunzi hawataki kupima damu na uzito lakini hupima mipini na vibamia eti kujua vina tofauti gani,utaelewa tu mdogo wangu.
Hili ndilo eneo pekee wazazi watakuamini sana mdogo wangu wakijua wewe ni msomi hata kama ni kichomi.

Sikukatishi tamaa mdogo wangu lakini wapenzi wa huku wengi wanakua na mafiga matatu na zaidi (eti ndio ujanja) karibu mdogo wangu jisikie uko batani.

Hili ndilo eneo pekee ambalo watu wengi ni waimbaji wa Bongo fleva yaani hamna talent nyingine.karibu sana mdogo wangu jisikie uko batani.

Hili ndilo eneo pekee watu wengi wanaitegemea serikali iwape ajira hata kama hamna watajiandaa cha ajabu anayesomea ualimu anavaa kama MC.karibu sana mdogo wangu.

Mdogo wangu wakati naandika haya nalia kwani siamini sisi tunaotegemewa na wazazi na Taifa tumekua hivi! Anyway!

Nikukumbushe tu mdogo wangu pamoja na hayo yote wapo watu wazuri wasiohusika na lolote kati ya hayo lakini nikutahadharishe kwamba ni vigumu sana kuwatambua hawa wazuri kwani ni wachache,unahitaji muda na utulivu kuwajua.

Vilevile kumbuka kuwa marafiki wanaathiri zaidi maisha yako kuliko waalimu wako..usikosee kuwachagua mdogo wangu.

Usisahau kuwa umri wako unakuruhusu kuwa na mpenzi lakini kuwa makini kuchagua wengine sio wapenzi ni washenzi.

Najua unamwamini Mungu mdogo wangu, lakini huku hiyo sio fashion sana,tafadhali usiiache ibada kwani kila hatua unayopiga shetani naye anatafuta mbinu ya kukukwamisha!

Mdogo wangu kitu chochote kisije kikakufanya ukawasahau wazazi wako kwani hakuna wakuichukua nafasi yao moyoni mwako!

Najua umemzidi baba/mama elimu lakini chunga usije ukaitumia elimu yako kuwadanganya na kuwadharau.Kumbuka wale ni wazazi wako.

Najua uliambiwa chuo kikuu bata lakini nikukumbushe bata huyu pia anashubiri kama SUP, Carry, na Disc.

Najua utawaambia marafiki zako maneno haya machungu kama ndimu lakini matamu kama asali,usijali waambie wenzako maneno haya huku nawe ukiyaishi.
Asante sana.
Ubarikiwe sana mdogo wangu, karibu chuo Kikuu na masomo mema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom