Hongera Kitwanga kuthibiti Rushwa kwa wawinda rushwa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Kumekuweko tabia ya baadhi ya wabunge na vyombo vya habari kuwinda rushwa kwa kujitia kuibua kashfa wakiwinda wapewe rushwa ili wasiseme bungeni au kuandika magazetini.Waziri Kitwanga kawadhibiti.Wamepiga kelele weee hela ya rushwa haitoki wameandika wee hela haitoki.

Nikiwaangalia wanavyoongelea kila wakisimama mfano swala la Lugumi nacheka hadi basi najua wanachowinda.Safari hii imekula kwenu.

Kuna wabunge wakipanua midomo kubwata bungeni na waandishi wa habari wanavyoandika kwa nguvu kurasa za mbele unaweza dhani wazalendo kweli kumbe hamna kitu.Kuna kitu wanawinda.Rejea jinsi walivyopanua midomo kubwata bungeni na kuandika swala la Lowasa bungeni na kurasa za mbele kuwa ni fisadi na baadaye wakaufyata wakaanza kumsifia na kumwandika vizuri.


Mawaziri wote komaeni safari hii hahongwi mtu na muwaambie kabisa wabunge na vyombo vya habari vya wale wawinda rushwa.Kama wanawatishia waambieni lipukeni ila hakuna hata shilingi ya rushwa mtapewa.
 
Kuna mheshimiw mmoja yeye dili lake lilikuwa mifuko ya hifadhi ya jamii tu lkn kwa utawala huu imekula kwao, naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom