Hongera Kishimba, Bila kufanya haya Elimu yetu itaendelea kuwa mzigo kwa Taifa

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,732
7,611
Elimu ya kumkomboa masikini ni Serikali kuwekeza kwenye elimu ya ufundi kuanzia Msingi hii itafanyaTanzania yenye Nguvu ki Uchumi katika Elimu inayogusa jamii ya watu wenye kipato cha chini ambao ni wengi.

Elimu ya msingi imebeba kundi kubwa la vijana wadogo ambao wengi wao huishia darasa la saba na kupoteza matumaini na kuishi maisha yasiyoeleweka katika jamii.

MFUMO WA ELIMU YENYE MSAADA YA DARASA LA SABA (VII)
Kama tunataka kufikia Taifa lenye Maendeleo ya kati haina budi kufanya haya ili tuitengeneze nguvu kazi yenye ujuzi, na utaalamu wa kufanya kazi Viwandani, Mashambani, Majumbani na kila sehemu inakohitajika nguvu kazi ya vijana kwa Maendeleo ya Jamii na Uchumi wa Taifa kwa ujumla.

1. Ufundi mbalimbali kwa wanafunzi wote wa kuanzia darasa la Tano hii itasaidia wale ambao hawataendelea na elimu ya Sekondari kuingia katika soko la ajira kujipatia kipato kusaidia familia zao na kukuza Uchumi wa pato la taifa Pia hata watakao maliza Elimu ya Sekondari na Elimu nyingine hawakupata ajira watajiajiri katika ufundi kwa sababu tayali wanao uzoefu na Utaalamu wa kutoka Shule ya msingi itaongeza tija kupunguza wasio na ajira na kuliongezea pato la kiuchumi taifa na kupunguza mzigo kwa Serikali kubeba kuhudumia kundi kubwa la wasiojiweza.

2. Kilimo Bustani: mboga mboga, matunda, maua, mazao kwa wanafunzi kuanzia darasa la Sita hususani kwa Shule za vijijini hii itasaidia kwa wale ambao hawataendelea na Elimu ya Sekondari au hata watakaokosa ajira kwa ngazi za Elimu watakazofikia maana watakuwa na utaalamu huo anglau wa kilimo watajiajiri mashambani kuongeza kipato kwa familia zao na kukuza pato la Uchumi wa Taifa

3. Kupulizia dawa za viuwatilifu (fumigation) majumbani na mashambani, bustanini kwa wanafunzi wa Darasa la Saba (Vll) hii itasaidia kwa wale ambao hawataendelea na Elimu ya Sekondari au hata watakaokosa ajira kwa ngazi za Elimu watakazofikia maana watakuwa na utaalamu huo anglau watajiajiri huko mashambani na majumbani kupulizia madawa kuua wadudu na kuongeza kipato kwa familia zao na kukuza pato la Uchumi wa Taifa
Na kutokomeza malaria

4. Kutengeneza Viatu, Sabuni kuogea na kufulia, kusafishia na Mafuta ya kupaka kwa wanafunzi wa Darasa la Saba (Vll) hii itasaidia kwa wale ambao hawataendelea na Elimu ya Sekondari au hata watakaokosa ajira kwa ngazi za Elimu watakazofikia maana watakuwa na utaalamu huo anglau walioupata mwanzo katka elimu ya Msingi watajiajiri na kuongeza kipato kwa familia zao na kukuza pato la Uchumi wa Taifa

5. Ufugaji wa Sungura, Bata, kuku wa mayai na nyama kuku wa kienyeji kwa wanafunzi wa Darasa la Saba (Vll) hii itasaidia kwa wale ambao hawataendelea na Elimu ya Sekondari au hata watakaokosa ajira kwa ngazi za Elimu watakazofikia maana watakuwa na utaalamu huo anglau watajiajiri na kuongeza kipato kwa familia zao na kukuza pato la Uchumi wa Taifa

AINA ZA UFUNDI, KILIMO,KUPULIZA MADAWA, KUTENGENEZA SABUNI,RANGI
1. Uashi
2. Uselemara
3. Fundi Bomba
4. Kutengeneza viatu
5. Kutengeneza sabuni
6. Kutengeneza Mabatiki
7. Kutengeneza mafuta ya kupaka
8. Ufundi Rangi majengo
9. Kilimo cha mashambani
10. Kilimo cha Bustani mboga mboga
11. Kilimo cha matunda
12. Kilimo cha Bustani maua na miti ya kupandwa
13. Upuliziaji madawa mashambani kuua magugu na wadudu waharibifu wa mimea
14. Upuliziaji madawa majumbani na katika mifugo kuua wadudu mchwa,viroboto na mende, mbu
15. Ufugaji kuku wa kienyeji
16.Kilimo cha kisasa
17.Kuchora picha na usanifu

WALIMU WA KUFUNDISHA
Serikali imeweza kutoa semina kwa Walimu Wakuu na Walimu wa Fedha, inchi nzima tangu Serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani jinsi ya kufanya manunuzi na usimamizi wa fedha inayotolewa na Serikali pamoja na wahisani.

Vivyo hivyo inaweza ikawapa semina waalimu wote kwa hizi fani ambazo hazihitaji utaalamu wa hali ya juu, na hizi fani zenye uhitaji wa wakufunzi wabobevu wakatafutwa waalimu wa Ufundi husika kulingana na uchaguzi wa kinachotakiwa kufunzwa katika shule kulingana na jinsi itakavyopangwa na wahusika.

PENDEKEZO: Serikali ianzishe mfuko wa kusaidia jamii vijiji, mitaa inchi nzima ili hawa vijana wapate mikopo ya mbegu na vifaa kazi kwa wahitimu watakao kuwa wamehitimu kuelekea kujitegemea.

MAHITAJI YA VIFAA VYA KUFUNDISHIA NA WAALIMU UPATIKANAJI PESA ZA UNUNUZI WA VIFAA
VIFAA vya kufundishia kwa vitendo na nadharia vichangiwe na wazazi wa Wanafunzi na 50% na Serikali ichangie 50%

WAALIMU Serikali iajiri Waalimu wa Ufundi na kuwapeleka Semina walimu waliokuwepo mashuleni kwa vitu ambavyo havihitaji utaalamu wa hali ya juu.

ANGALIZO:

Wasomi wengi waliopo katika nafasi nzuri zenye mafanikio wamekuwa wabinafsi ambao hawana huruma kwa wanyonge na hawakumbuki walikotoka ndiyo wamekuwa chanzo cha Ufisadi na unyonyaji wasichofahamu ni kuwa kodi za wanyonge ndiyo zinawalipa mishahara.

Hatuwezi kufikia mafanikio kama hatuwezi kuinua Elimu na kipato cha jamii ya wanyonge walio wengi

Mungu bariki Rais wetu wa JMT J.P.Magufuli

Mungu Ibariki Tanzania
 
jamaa ameona mbali... mfumo mzuri elimu ya awali ya msingi iwe mwisho darasa la 5(hapa mwanafunzi atasoma writting and reading skills pamoja na historia na technical theory) elimu ya juu ya msingi iwe miaka miwili( hapa mwanafunzi atajifunza all technical skills) baada ya hapo mwanafunzi atafanya mtihani wa kwenda shule za sekondari .
 
Mfumo wa kidunia uko hivyo umesetiwa kwa makusudi ili uendelee kama nchi lazima uwe foreign currencies siyo local currencies sasa kuzipata foreign or forrex lazima utafute kitu cha kuwavutia wageni waje na dollar!

Mbunge wangu Kishimba aliongea bungeni watu wote waliona point sana kuhusu elimu wewe ukibadirisha mfumo wa elimu mpaka upate endorsement ya wakubwa kupitia UNESCO la sivyo dunia inakutenga unatoka inje ya universal ndo universities doctor aliesomea Mhimbili ,Bugando,Udom ,anatakumburika kama doctor of medicine duniani alipo zote professionals zinatamburika duniani sasa wewe waka mfumo wako wakila mwaka umehitimu madarasa mawili unatengwa na dunia kama North Korea na nk unaruhusiwa kubadili lugha tu
 
Kishimba Kuna sehemu alinichekesha katika moja ya mchango wake bungeni alisema Ana watoto sita wamemaliza digrii zao hawana kazi serikali itoe ajira.

Nilicheka sababu yeye ni mfanyabiashara mkubwa Sana kashindwa kuwapa ajira wanae kwenye biashara na kampuni zake? Tunaona matajiri wafanyabiashara akina Mengi,dewji,manji, Bakhresa,wahindi,wapemba wakiajiri watoto wao ndani ya biashara zao wamalizapo digrii zao.

Kwa Hilo kishimba kanishangaza ina maana hizo biashara zake hataki kushirikisha watoto!!!!!Matajiri Kama kishimba na aina ya kishimba Ni moja ya wanaochangia tatizo la ajira nchini sababu hao watoto wake angewaajiri kwake tatizo la ajira lingepungua kwa kiasi.

Kishimba ajiri hao Watoto wako wenye digrii kwenye biashara na kampuni zako.
 
Kishimba Kuna sehemu alinichekesha katika moja ya mchango wake bungeni alisema Ana watoto sita wamemaliza digrii zao hawana kazi serikali itoe ajira.Nilicheka sababu yeye...
mkuu wasukuma na wanyantuzu hawashirikishi watoto wa nje ya ndoa kwenye biashara zao, hao itakuwa alizaa na vimada, ukifanya hivyo unakula sumu fasta.

Pili watoto wakiwa wengi kila mmoja atajitahidi kuiba kwa hofu kuwa mzee akienda ghafla atazurumika, wahindi na wachagga wanakuwa na wototo wachache, sana sana hawazidi watano lakini wengi wao ni wawili au watatu hivyo huona utajiri wa baba yao ni wao.

Halafu wahindi na waarabu mtoto wa nje si sehemu ya familia na hana chake na ni mara chache kukuta mhindi ana mtoto wa nje.
 
Mfumo wa kidunia uko hivyo umesetiwa kwa makusudi ili uendelee kama nchi lazima uwe foreign currencies siyo local currencies sasa kuzipata foreign or forrex lazima utafute kitu cha kuwavutia wageni waje na dollar...
kwani hao wahitimu wataenda kuajiriwa huko duniani? kwanini tusiwe na mfumo rafiki unaoendana na mazindira ya kwetu, pili kwani lazima tuwe na mtaala mmoja nchi nzima? kama tuna Swahili media, English media, kwanini tusiwe na technical media?

French media, Spanish media? ukweli ukienda gereji za vijiweni kuna vivulana vidogo vinasogeza jeck na kumpatia fundi spana na stick za kuchomea, sasa kwanini tusiwe na technical school za kuanzia darasa la kwanza hadi la saba?
 
mkuu wasukuma na wanyantuzu hawashirikishi watoto wa nje ya ndoa kwenye biashara zao, hao itakuwa alizaa na vimada, ukifanya hivyo unakula sumu fasta, pili watoto wakiwa wengi kila mmoja atajitahidi kuiba kwa hofu kuwa mzee akienda ghafla atazurumika, wahindi na wachagga wanakuwa na wototo wachache, sana sana hawazidi watano lakini wengi wao ni wawili au watatu hivyo huona utajiri wa baba yao ni wao. Halafu wahindi na waarabu mtoto wa nje si sehemu ya familia na hana chake na ni mara chache kukuta mhindi ana mtoto wa nje.
Huoni pia huko kuzaa nje kwa matajiri wa kisukuma na kinyatzu ambao hawana mpango wa kuwaajiri kwenye biashara na kampuni zao huoni kuwa ni kuongeza tatizo la ajira? Nashauri watoto wa nje wa matajiri wa kisukuma na kinyatzu waende mahakamani kudai mitaji au sehemu ya biashara za baba zao.wakiwa hai hao baba zao
 
Huoni pia huko kuzaa nje kwa matajiri wa kisukuma na kinyatzu ambao hawana mpango wa kuwaajiri kwenye biashara na kampuni zao huoni kuwa ni kuongeza tatizo la ajira? Nashauri watoto wa nje wa matajiri wa kisukuma na kinyatzu waende mahakamani kudai mitaji au sehemu ya biashara za baba zao.wakiwa hai hao baba zao
huwa wanapewa basic needs kama kusomeshwa shule lakini sio kuwa sehemu ya familia, pia inategemea na akili ya mtoto, kama ana akili za utafutaji anaweza pewa mtaji lakini lazima aonyeshe juhudi binafsi kwanza,
 
kwani hao wahitimu wataenda kuajiriwa huko duniani? kwanini tusiwe na mfumo rafiki unaoendana na mazindira ya kwetu, pili kwani lazima tuwe na mtaala mmoja nchi nzima? kama tuna Swahili media, English media, kwanini tusiwe na technical media? French media, Spanish media? ukweli ukienda gereji za vijiweni kuna vivulana vidogo vinasogeza jeck na kumpatia fundi spana na stick za kuchomea, sasa kwanini tusiwe na technical school za kuanzia darasa la kwanza hadi la saba?
Hili wazo zuri Sana.Sasa hivi kunahitajika tuwe hata na Chinese medium schools zinazotumia syllabus ya China au Germany medium schools zinazotumia syllabus ya ujerumani nk . Tuachie sekta binafsi iingie kazini.Mishule yetu ya msingi ianze kuwa na michepuo mfano ya michepuo ya kilimo ,ufundi nk toka darasa la kwanza au chekechea .Hii mishule ya elimu ya msingi general hii Ni useless.Mjerumani alikuwa na Trade schools primary na zilisaidia Sana mtu akimaliza alikuwa anajua Cha kufanya.
 
huwa wanapewa basic needs kama kusomeshwa shule lakini sio kuwa sehemu ya familia, pia inategemea na akili ya mtoto, kama ana akili za utafutaji anaweza pewa mtaji lakini lazima aonyeshe juhudi binafsi kwanza,
Aisee Mimi ningekuwa mtoto wa nje pangechimbika.Kunipa basic needs na kunisomesha Ni haki yangu sababu sikuomba unizae.Pia kupewa sehemu ya utajiri wa mzazi Ni haki yangu Sio ombi Wala hisani Wala kitu kinachotegemea huruma ya baba mzazi .Aisee pangechimbika Wala Sio Siri.
 
Huyu jamaa ana akili tofaut na ambavyo Watu wanavyomchukulia kwa yy STD niliwahi kumsikiliza hata kwenye mkutano wa madini na rais speech yake ilinikosha sana kuliko hata wabobezi WA madini WA tz
Mfumo wa kidunia uko hivyo umesetiwa kwa makusudi ili uendelee kama nchi lazima uwe foreign currencies siyo local currencies sasa kuzipata foreign or forrex lazima utafute kitu cha kuwavutia wageni waje na dollar!
Mbunge wangu Kishimba aliongea bungeni watu wote waliona point sana kuhusu elimu wewe ukibadirisha mfumo wa elimu mpaka upate endorsement ya wakubwa kupitia UNESCO la sivyo dunia inakutenga unatoka inje ya universal ndo universities doctor aliesomea Mhimbili ,Bugando,Udom ,anatamburika kama doctor of medicine duniani alipo zote professionals zinatamburika duniani sasa wewe waka mfumo wako wakila mwaka umehitimu madarasa mawili unatengwa na dunia kama North Korea na nk unaruhusiwa kubadili lugha tu
 
hilo wazo zuri sana,japo kishimba la saba lakini ana mawazo kama mtu mwenye degree kumi
 
Ni moja ya speech yenye madini kuliko zote.Ni mmoja ya wasukuma ambao ajaenda shule lakini ana output fact kuliko wenye PhD za kukariri output utadhani awajasoma hata kujitambulisha tu tabu
Kabisa huyu jamaa ni kichwa
 
jamaa ameona mbali... mfumo mzuri elimu ya awali ya msingi iwe mwisho darasa la 5(hapa mwanafunzi atasoma writting and reading skills pamoja na historia na technical theory) elimu ya juu ya msingi iwe miaka miwili( hapa mwanafunzi atajifunza all technical skills) baada ya hapo mwanafunzi atafanya mtihani wa kwenda shule za sekondari .
Hili ndiyo hitaji kwa kila mpenda maendeleo ya wanainchi lakini watawala wetu wanaweza kulifanyia kazi?
 
Mfumo wa kidunia uko hivyo umesetiwa kwa makusudi ili uendelee kama nchi lazima uwe foreign currencies siyo local currencies sasa kuzipata foreign or forrex lazima utafute kitu cha kuwavutia wageni waje na dollar!
Mbunge wangu Kishimba aliongea bungeni watu wote waliona point sana kuhusu elimu wewe ukibadirisha mfumo wa elimu mpaka upate endorsement ya wakubwa kupitia UNESCO la sivyo dunia inakutenga unatoka inje ya universal ndo universities doctor aliesomea Mhimbili ,Bugando,Udom ,anatakumburika kama doctor of medicine duniani alipo zote professionals zinatamburika duniani sasa wewe waka mfumo wako wakila mwaka umehitimu madarasa mawili unatengwa na dunia kama North Korea na nk unaruhusiwa kubadili lugha tu
Hapa hatusemi kubadili mfumo tunachotaka ni wale wenye ufaulu wa juu waendelee na elimu lakini hawa wengi wenye ufaulu mdogo wafanye kazi kuzalisha ktk viwanda ,mashamba watakayokuwa wameyaanzisha kuliko kulazimisha mifumo ya vitu visivyo na tija
 
Back
Top Bottom