hongera KINANA..HII NDO CCM TULIYOKUWA TUNAITAKA

KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
184
Si wanaopiga kelele au kukejeli mikutanoni wanafanya kejeli hapana wanatoa ujembe kuwa wanamatatizo yanahitajika kuelezwa na kutatulia: Habari itv ..

Safi kinana wazi chama kinarudi upya na naungana tena na makala ya kibanda katika gazeti la tanzania daima.
 
Si wanaopiga kelele au kukejeli mikutanoni wanafanya kejeli hapana wanatoa ujembe kuwa wanamatatizo yanahitajika kuelezwa na kutatulia: Habari itv ..

Safi kinana wazi chama kinarudi upya na naungana tena na makala ya kibanda katika gazeti la tanzania daima.



Machoni kama watu!!!!!!!!!!!!
 
Hiyo ni michezo ya kuigiza, wewe unamsifia kwa kuvaa vizuri uhusika, basi akamkaripie pia Waziri wa utalii
 
Si kote anapigiwa makofi.

Angalia hapa:
MAWAZIRI watatu wa Rais Jakaya Kikwete juzi walizomewa baada ya kupanda jukwaani kujibu kero mbalimbali za wananchi katika mkutano wa kwanza wa viongozi wapya wa CCM taifa, ulioongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana.

Tukio hilo lilitokea juzi mkoani Mtwara ambako Kinana na mawaziri hao walikuwa katika ziara ya chama kujibu kero mbalimbali za wananchi.Mawaziri waliokumbwa na dhahama hiyo ni Christopher Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Tamisemi) Naibu wake, Aggrey Mwanri.

Chiza ndio alikuwa wa kwanza kukumbana na zomeazomea hiyo, lakini mambo yalikuwa magumu zaidi kwa Ghasia ambaye alizomewa tangu alipoanza kuzungumza mpaka alipomaliza.Ghasia ambaye pia ni mbunge wa Mtwara Vijijini, alirushiwa makombora na Rukia Ismail Athumani ambaye alimshutumu yeye pamoja na Mbunge wa Mtwara mjini, Asnein Murji kwamba waliruhusu gesi kupelekwa Dar es Salaam wakati wananchi wa mkoa huo hawajafaidika nayo.

“Ghasia na Murji kwanini mnaudanganya umma kwa kupeleka gesi Dar es Salaam, sisi hatuna ubaya na chama ila hatutaki gesi iende huko” alisema Athumani huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.Kabla ya dada huyo kuteka hisia za wananchi kwa kuwasilisha kero hiyo, Kinana alimruhusu mwananchi mwingine, Issa Kambona ambaye pia alieleza kuwa hakubaliani na suala la gesi hiyo kupelekwa Dar es Salaam.

Kinana alisema amesikia hoja hizo za wananchi na kwamba atamueleza Waziri wa Nishati na Madini azungumze na wananchi wa Mtwara kuhusu gesi hiyo.Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu, Ghasia alilazimika kupanda jukwaani kujibu makombora aliyokuwa akirushiwa na wananchi waliofika katika mkutano huo.

“Sio kweli kwamba hatutetei maslahi yenu, gesi iliyopo ni nyingi hamuwezi kuitumia na kuimaliza, kuna futi za ujazo trilioni 20,000 na tunaweza kuitumia kwa zaidi ya miaka 90, hata hivyo, Wizara ya Nishati na Madini imetoa ofa ya kuwalipia chuo vijana 150 kila mwaka,” alisema Ghasia, lakini wananchi hao waliendelea kumzomea.“Uongo, uongo, hatutaki, hatutaki, huyoo, huyooo” walisikika wakisema wananchi hao, hali iliyomfanya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kuingilia kati, kujaribu kuwatuliza.

“Kelele unazozisikia dada (Ghasia) zinaashiria kuna jambo, nafasi hizo 150 hawazipati, kama zinatolewa basi kwa upendeleo,” alisema Nape huku akishangiliwa na wananchi hao.Baada ya hali kutulia kiasi, Ghasia alijaribu kuendelea kutoa ufafanuzi, lakini kitendo cha kuanza kuzungumza, wananchi hao walianza tena kuzomea.

“Kila mtu amelelewa katika mazingira tofauti, hilo halinihusu…watu wangu wa Mtwara vijijini wamenielewa,” alisema Ghasia na kuteremka jukwaani hali iliyozidisha kelele za kumzomea.Nape alisawazisha mambo kwa kusema, hoja ya wananchi hao imechukuliwa na itawasilishwa kwa Serikali ili kuona namna ambavyo inaweza kukaa na wananchi hao na kuweka maslahi yao mbele.

Ilivyoanza

Pazia la zomea zomea lilifunguliwa na Chiza alipopanda jukwaani kujibu hoja ya kuyumba kwa soko la zao la korosho, ambapo wananchi walimpinga baadhi ya kauli alizozitoa.“Tatizo la korosho ni baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na wengine ni watendaji wa Serikali …nipo hapa na wala siondoki, nitalishughulikia hili ili korosho zinunuliwe” alisema Chiza huku sauti za wananchi zikimpinga kwa kusema “uongooo”.

Hata hivyo, Chiza aliweza kukabiliana na hali ya zomeazomea jukwaani baada ya watuliza wananchi kwa kusisitiza kuwa ataendelea kuwapo Mtwara, kushughulikia tatizo hilo ili ununuzi uendelee.Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwanri alipata wakati mgumu mara alipopanda jukwaani na kuanza kuzungumzia namna ya kumaliza kero ndogondogo zinazoletwa na mamlaka zake, wananchi walikuwa wanazoea “huyoo…hatutaki” lakini baada ya kuanza kuongea alionekana kuiteka hadhira na mambo yakawa shwari. “

“Tumesema wauza vitumbua, wasibughudhiwe … mkurugenzi njoo jukwani, nakuagiza kuanzia leo marufuku wanafunzi kurudishwa shuleni kwa sababu ya michango” alisema Mwanri huku akishangiliwa.Awali Kinana alisema mkutano huo unalenga kuzipatia ufumbuzi kero za wananchi ambazo zinawezakuwa kikwazo kwa chama hicho kuingia madarakani mwaka 2015.

Katibu mkuu huyo wa chama tawala alisema umefika wakati wa chama kusimamia utendaji wa Serikali kutatua kero za wananchi wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni pamoja na kuyumba kwa soko la korosho na gesi.“Najua hapa kuna kero kubwa mbili, korosho na gesi, nimekuja na Mawaziri hapa watatoa majibu leo” alisema Kinana huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu ulioudhuria mkutano huo.


Chanzo: Gazeti la Mwananchi

MY TAKE: sUMBAWANGA JE????? aRUSHA WAKIFIKA ITAKUWAJE? mWANZA? sHINYANGA????

Kwanini hatukuambiwa hii mapema? Imetokea Mtwanra na kuandikwa na Mwananchi la leo.


Na hapa:


quote_icon.png
By Kurunzi

NAHUKO SUMBAWANGA MAMBO YALIKUWA HIVI.

Mjini Sumbawanga mambo yalikuwa magumu kwa viongozi wapya wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wao, Kinana, baada ya kukumbana na zomeazomea ya wananchi kwenye mkutano wake.

Kinana aliingia mjini humo jana kwa ndege akiongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Katibu wa Organizesheni Seif Khatib na Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwandri, na kisha kwenda eneo la Isesa kufanya mkutano. Kwa kuwa eneo hilo ni ngome kuu ya CHADEMA, viongozi hao walianza kuzomewa na hivyo wakati wakiondoka wafuasi wao waling’oa bendera na mlingoti kwenye shina la wapinzani wao na hivyo kuzidisha chuki.

Wakiwa katika mkutano wao wa ndani, uliibuka mzozo mkubwa baina ya viongozi na waendesha bodaboda waliokuwa wamekodishwa kubeba bendera kwa ujira wa kujaziwa mafuta na sh 10,000.
“Walitaka kuwageuka vijana wale ambao kimsngi wengi wao si wafuasi wao kwa kuwalipa sh 2,000 badala ya 10,000 lakini baadaye walilazimika kuwalipa kulingana na makubaliano,” kilisema chanzo chetu.

Mchana wakiwa kwenye mkutano wa hadhara eneo la Liboli, Nape aliwaudhi baada ya kuanza kutoa matusi ya nguoni na hivyo akazomewa kwa nguvu kiasi cha kudai wanaozomea wana mimba. Hata Mwanri naye alipata wakati mgumu wakati akitoa ufafanuzi wake na hata Mkuu wa Mkoa, Stella Manyanya, alipoitwa na Kinana afafanue naye alizomewa hatua iliyomfanya Katibu huyo kutumia busara ya hali ya juu kuwatuliza wananchi na mkutano ukamalizika.
 
arudishe mashine ya kufua nguo ya hospitali ya mount meru.

aturudishie makontena ya meno ya tembo yaliyokutwa china.

mikutano anayofanyia ndani si ni ya wanachama wa ccm,kwani hao wana shida nao mziki ni kwa wananchi ngoja amalize tumshushie mziki mtwara na rukwa.
 
Si wanaopiga kelele au kukejeli mikutanoni wanafanya kejeli hapana wanatoa ujembe kuwa wanamatatizo yanahitajika kuelezwa na kutatulia: Habari itv ..

Safi kinana wazi chama kinarudi upya na naungana tena na makala ya kibanda katika gazeti la tanzania daima.

Chama kinarudi upya kivipi? Si bado mafisadi akina Kinana, Chenge, Lowassa, Rostam, Riziwani, Mkapa, nk ni wana-CCM? Au unafikiri mkipiga sound sana mtatusahaulisha ufisadi wa EPA, MEREMETA, RADA, DEEP GREEN FINANCE, MWANANCHI GOLD, MGODI WA KIWIRA, MABILIONI MLIYOFICHA USWISI, USAFIRISHAJI HARAMU TWIGA/MENO YA TEMBO, nk?
 
Hizi threads mnazoanzisha zinatoa mwanya zaidi ya kuumbua hao viongozi wenu wapya.

Kinana haraka sana atakuwa sababu kubwa ya kudidimia kwa CCM kwa rekodi yake ya ulafi kwa maliasili zetu.
 
Ngudu Kinana badala ya kutumia hela kuzunguka nchi nzima angefanya jambo moja tu muhimu - ahakikishe hela za Swiss zinarudi nchini haraka. Matatizo anayoyaona huko vijijini yanaweza kutatuliwa kwa kiasi kikubwa kama kuna fedha. Na sasa tunajua kuna mabilioni yamefichwa Uswiss. Kinana aachane na vibarua vidogo vidogo vinavyostahili kufanywa na wakina Nape na badala yake asimamie mambo makubwa kama hayo ya kufilisi nchi.

Pamoja na hilo Ndugu Kinana aamuru serikali itoe maelezo (kama anavyofanya kwenye ziara zake huko Kusini) kuhusu meno ya tembo, na itaje ni nani anahusika, na ni hatua gani zimechukuliwa.
 
Naona siku mbili hizi zimefululiza threads za kulisha watu sumu!
Alafu waanzilishi ni dizain zile zile tuu!
 
Si wanaopiga kelele au kukejeli mikutanoni wanafanya kejeli hapana wanatoa ujembe kuwa wanamatatizo yanahitajika kuelezwa na kutatulia: Habari itv ..

Safi kinana wazi chama kinarudi upya na naungana tena na makala ya kibanda katika gazeti la tanzania daima.

Kipambe Chama chako cha Mapinduzi kwa kadiri uwezavyo,lakini kumbuka kila alichoanzisha mwanadamu hakitodumu milele sisi sote ni Watanzania hebu tujaribu kujifunza uzalendo walau kidoho.
 
Kinana chapa kazi hao wanao zomea ni upepo utapita tu ccm sio size ya cdm hata siku moja wewe ni jembe kubwa utawamaliza hawana pakutokea na mwaka huu watakoma na m4c yao cha mtoto kinana oyeeeeeeeeeee ccm safiiiíìiííííiíií kidumu chama cha mapinduzi.
 
Yani kaongea ukweli na ndio wananchi wanataka kusikilizwa...na kawasikiliza wamemwambia kero kubwa ni maji.... Sasa chama kinarudi kwa wananchi... Hongera kinana...... Sijui m4c itaenda pwani...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom