Hongera kikwete kwa kuleta ukombozi wa kisiasa nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera kikwete kwa kuleta ukombozi wa kisiasa nchini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gosbertgoodluck, Nov 5, 2010.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wengi wetu tunamtazama kikwete kwa jicho hasi kutokana na namna anavyoongoza nchi. Wananchi wengi mitaani na kupitia vyombo mbalimbali vya habari wamekuwa wakimlalamikia kikwete kuhusu hali ngumu ya maisha inayozidi kuwa mbaya siku hadi siku.

  Mimi binafsi nina mtazamo tofauti kabisa. Actually, kwangu mimi kikwete ni shujaa wa mabadiliko hapa nchini. Ninamweka kwenye daraja la Dr. Slaa. Kwa nini nasema hivi, nitaeleza. Kwa muda mrefu sasa tangu wakati wa uongozi wa mzee ruksa, nchi yetu imekuwa ikipita katika kipindi kigumu sana. Maisha ya wananchi yameendelea kuwa duni tofauti na nchi nyingine. Kinachosikitisha ni kwamba hata pale tunapopiga hatua angalau moja mbele, tumekuwa tukiteleza na kurudi nyuma hatua mbili zaidi. Yote hayo yamakuwa yakitokea chini ya ccm na wananchi wakiendelea kuimba nyimbo za 'kidumu chama cha mapinduzi'. Inapofika wakati wa uchaguzi wanasahau kila shida na adha inayowapata, wanaipigia ccm kura nyingi. Yote hayo yametokea mpaka kipindi cha mwisho cha rais mkapa. CCM imeendelea kujivika nguo ya chama cha kizalendo na kimevuta watu wengi wa kila aina. Lakini vilevile ccm imeendelea kuvuta watu wengi kwa mtazamo kwamba ni chama kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Nyerere aliyeipenda nchi hii kupita upeo. Hatimaye mwaka 2005 akaingia huyu ambaye mimi binafsi ninamwita shujaa wa siasa za ukombozi nchini, wenyewe wanamwita dokta (kipropaganda tu) kikwete.

  Chini ya uongozi wa kikwete sura halisi ya ccm imeweza kudhihirika mbele ya wananchi. Wananchi wameweza kung'amua kuwa ccm si chama cha wakulima na wafanyakazi kama bendera yake inavyoonekana, bali ni chama cha matajiri, walanguzi, wabwia unga na manyang'au wote wa nchi hii. Ni chama kokolo kilichozoa na kuhifadhi aina zote za uchafu (taja uchao wowote unaoweza kuukumbuka). Ni chama kilichofikia jeuri hata ya kuwatetea wahujumu uchumi waziwazi tena mbele ya hadhara ya wananchi (rejea kikwete kunyanyua mikono ya akina Mramba na Chenge). Ni chama chenye serikai inayokubali kubadilishana madini na rasilimali nyingi za thamani kwa vyandarua vya mbu huku wananchi wake wakiogelea kwenye dimbwi la umaskini. Ni chama kinachojisiku kwa mafanikio ya 'idadi' au 'uwingi' na siyo 'ubora'. Ni chama kinachofanya hila za kila aina kuua uhuru wa vyombo vya habari ili kuzima na kunyamazisha kabsia sauti ya wananchi na ili kiendelee kuwatawala na kuwanyonya.

  Lakini kma wasemavyo waswahili, Mungu si Athuman na kila karne ina shujaa wake, hatimaye nchi imempata shujaa nae ni kikwete. Shujaa huyu amefanya mengi lakini kubwa zaidi ni kufanikiwa kivua chama chake koti la bandia na sasa kinaonekana mbele ya wananchi kikiwa kimevaa koti lake halisi na ndiyo maana wananchi wengi sasa wamekitambua barabara. Hii ilikuwa ni hatua muhimu katika kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi hapa nchini. Vyama vya siasa vikiongozwa na chama cha chadema vimeanza kufanya kazi yake ya kuwafumbua macho watanzania ili walione koti halisi la chama kilichowarubuni miaka na miaka. Wananchi wengi na hasa vijana wenye macho makali tayari wameng'amua hilo na sasa hawadanganyiki tena. Hatua ya kwanza waliyochukua mwaka huu ni kujiandikisha wengi kupiga kura. Walifanya hivyo na kwa nguvu zao zote walichukua hatua nyingine muhimu ya kulinda kura zao. Kwa jitihada hizo, majimbo yote muhimu na maarufu hapa nchini tayari yapo chini ya wananchi kupitia chama chao cha chadema. Majimbo ambayo wananchi wake bado wapo kwenye lipi la usingizi bado yameendelea kuiunga mkono ccm.

  Kwa hiyo, kwangu mimi haya ni mafanikio makubwa yaliyoletwa na kikwete na bila kificho sina budi kumpongeza sana. Ninayo matumaini makubwa sana kwamba kasi yake hiyo ataiendeleza katika ngwe yake ya mwisho ya uongozi wa nchi hii. Kinachonifurahisha ni kuwa ahadi lukuki alizotoa (zingine za kufikirika tu) zimejenga msingi mzuri wa kazi yake aliyoianza ya kuivua ccm koti lake la bandia. Ni ahadi za danganya toto lakini amezisemea kwa jeuri na wananchi wamemsikia na wameziorodhesha ili iwe rahisi kukumbuka ifikapo 2015. Wito wangu kwa viongozi wa vyama vya upinzani hususan chadema ni kuwa waendelee kutumia ipasavyo mazingira hayo yanayotengenezwa na shujaa wetu kikwete ili hatimaye ukombozi kamili wa wananchi uweze kupatikana ndani ya miaka michache ijayo. Moto wa wanachi kutaka mabadiliko umewashwa na shujaa wetu. Kazi ya Dr. Slaa na wanaharakati wote wazalendo ni kuendelea kuuchochea ili ifikapo 2015 ukombozi kamili upatikane.

  Mwisho, ninarudia tena kumshukuru sana kikwete kwa kutujengea mazingira mazuri ya kuleta ukombozi wa kisiasa na kiuchumi hapa nchini.

  Mungu ibariki Tanzania,
  Mungu ibariki Afrika.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,744
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni Mikhail Gorbachev wa Tanzania, na kizuri zaidi ni kuwa afya ndiyo inazidi kuwa mgogoro, ukombozi uko jirani.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Hii kitu yako ndefu sana.......acha niiweke pendingi kwanza.

  Nitaisoma baadaye, japo inaonekana kama crap hivi
   
 4. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 5. b

  bob giza JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mbona raha, kaiba kura afu anakufa soon ehehehehe Mungu mkubwa ahimidiwe..usicheze na Mungu eti..ana njia njingi..mimi huwa nasema ni afadhali ucheat, umdanganye na kumwibia mkeo au mumeo kuliko kuibia umma...Mungu hatakuacha isee..tangulia kikwete unaturushia stimu..
   
Loading...