Hongera Kamanda Tibaigana - Viguza Village Hotel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Kamanda Tibaigana - Viguza Village Hotel

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Superman, Jan 5, 2009.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Kwa wale waliopata nafasi ya kufika Viguza Village Hotel huko Mkuranga watakubaliana na mimi kuwa mwekezaji amejitahidi kufanya kweli na kuonyesha mfano kuwa hata Watanzania tunaweza Ku-Invest katika Hotel Sector kama tukiamua.

  Hotel imejengwa vizuri na huduma zake pia wanajitahidi sana . . .

  Nilipodadisi ni nani mmiliki wa Hotel hivyo . . . Nilielezwa kuwa inamilikiwa na Kamanda Mstaafu wa Kanda Maalumu ya Kipolisi DSM - Commissioner Tibaigana . . .

  Hongera sana Kamanda kwa mafanikio hayo . . . .

  Habari ndo hiyo . . .
   
 2. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nami pia nampa hongera! Inaonekana mafao aliyoyapata kama kiinua mgongo ni baab kubwa na Polisi wanalipwa vizuri sana.

  Lakini pia ungefafanua kidogo kutuondolea mashaka. Tungetaka kujua kama alipata mkopo benki au ni kiinua mgongo tu na mishahara aliyojiwekea kipindi cha kuajiriwa au ameingia ubia na mwekezaji mwingine vinginevyo maswali ni mengi kuliko majibu.
   
 3. I

  Ipole JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani tunataka hawa wastaafu wetu wawe ombaomba wanapojitahidi kujiandalia miradi inakuwa tatizo basi hebu tueleze kama unafahamu uwekezaji wake siyo halali
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hongera Tiba, lakini kumbuka kesi ya mauaji ya vijana wawili, Mine Chomba na Hija Shaha Salehe inakusubiri. Hata muifiche vipi tutaiulizia, na ikumbukwe ulifikia hata kumiliki gari moja lililohusishwa na mauaji hayo, gari la marehemu Mine Chomba.
   
 5. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #5
  Jan 5, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nakushangaa umemnukuu Dr mwakiembe kuwa watanzania sio mabwege tena na bado unahoji????? wewe kaa na mawazo yako wenzio wanapeta
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama kuna mtu anapenda wawe ombaomba lakini pia hakuna mtu anayependa uwekezaji au mafanikio yapatikane kwa njia zisizo halali. Lakini pia hakuna mtu yoyotwe aliyesema kuwa uwekezaji huo si halali au ni wa kifisadi.
   
 7. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kamanda kaza buti hakikisha unaendelea kujijengea uwezo wa kujitegemea hatutafurahi kukuona unakuwa ombaomba nguvu bado unazo.
   
 8. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Sio vibaya kama Tiba angewashauri wastaafu wenzake jinsi ya kuanzisha miradi ka hii. Manake wastaafu wengi wanakuwa choka mbaya baada ya muda si mrefu. Manake wanakosa rasilimali za kuwekeza.
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Afande mstaafu Tiba kabla ya kustaafu aliwahi kuhojiwa na gazeti moja juu ya matarajio yake baada ya kustaafu; alijibu kuwa yeye na rafiki zake walikuwa na mpango wa kuanzisha hoteli huko mkuranga nadhani ndio hiyo. Mmoja wa marafiki zake wakubwa ni Adadi Rajab [ former DCI] kwahiyo sintashangaa kama Adadi ni shareholder wa mradi huo. Hongera Tiba...........Ubunge vipi unamuachia Masilingi?
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Tiba mpango mzuri baada kustaafu....maana wengine wanakurupuka na miradi wasieweza kwa maana hawakufanya research mapema huwa wakishika kibunda ndio wanaanza kupaparika 2 yrs kwisha na wanakufa mapema.
   
 11. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nani amekwambia huyu kafanya research?!
   
 12. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #12
  Jan 5, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Safi sana; mkuu unaweza kutuwekea picha ya hiyo hoteli?
   
 13. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Baada ya hongera
  Maswali ya msingi
  Ana leseni?
  Analipa kodi?
  Ameajiiri wazawa wangapi?
  Waajiriwa wanalipwa mishahara iliyokubaliwa?
  Waajiriwa wanalipiwa mafao ya uzeeni?
  Anafuata sheria za kutunza mazingira?
  Wateja wake wanapatiwa usala,a wa kutosha
  Ubora wa bidhaa je?
  n.k n.k n.k

  Haya si maswali ya chuki ila ni kumkumbusha kuwa afuate sheria katika utendaji wake maana anazijua na alizisimamia
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Jan 6, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280


  ..........ACHENI USHAMBA .....YAANI MNATAKA NINI WATANZANIA ...MTU AMEJITAHIDI KUJIBANA ILI AKISTAAFU MSIANZE KUMCHEKA ...KUWA PESA ZAKE AMEJENGEA CHUPI...MNAANZA KUHOJI HOJI........WEWE !..MTU KATUMIKIA TAIFA MIAKA 40..MNATAKA ASHINDWE HATA KUJENGA KAHOTELI KALUZEEKEA....

  NIMEGUNDUA WATANZANIA NI WATU AMBAO MNAPENDA WATU WAAADHIRIKE KAMA GEORGE LIUNDI..ILI MUWACHEKE....TUACHE TABIA HII...

  WATU WOTE TUNAO WAJIBU WA KUTUNZA KIDOGO TUNACHOPATA ILI TUSIJEKUCHEKWA BAADAYE....TUJENGE NYUMBA NA MASHAMBA TUYANEEMESHE......MRADI TUSIKWAPUE....FAINALI UZEENI!!

  HONGERA TIBA....HIVI NANI NAJIANDAA...NA IPO SIKU NITAKAMATA KADIGI DIGI KANGU NIJE NIKATAFUNIE HAPO KWENYE KIOTA KAKO...teh teh kiiddin!!...
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Jan 6, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  pia tukumbuke ..hata mkaona mtu leo anadhalilika baada ya kustaafu na nafasi alikuwa nayo ya kuwa na uwezo halali...mjuwe kama asingeendekeza ulevi na ngono..basi angekuwa mbali.....ngono na ulevi vingekuwa bati na tofali angekuwa na majumba mengi tu.....!!!...siku hizi tujifunze kuchukuwa wanawake kwa mali kauli!!!...wengine ...tumezowea mali kauli na waala hatukosi....
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Jan 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Ushauri murua kabisa kwa kuanzia mwaka....!
   
 17. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Wakulu,

  Jambo msilolijua ni sawa na usikuwa giza.Kama watanzania mngejua aliyejenga Hiyo hoteli kwa ajili ya Tibaigana mngeshikwa na upumbuani.

  Nchi hiii bwana..Mie na mimi nataka kuwa Waziri tu sasa hivi
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Isije kuwa una kijiba cha roho tu...! Angalia usife nacho
   
 19. l

  lageneral Member

  #19
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakubwa,na hiyo Mwanzo lodge ya huko Mkuranga ni ya nanai?Nilidhani ndiyo ya mzee Tibaigana
   
 20. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Gembe,
  Unamuogopa nani?
   
Loading...