Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,034
- 7,590
Sina mengi zaidi ya kuupongeza uongozi wa mkoa, halmashauri, wazazi, wanafunzi na wadau wengine mlioshiriki katika kufikia matokeo haya ya kidato cha pili 2016 yaliyoupa mkoa namba 1 kitaifa. Mnastahili kupongezwa kweli kweli ukizingatia hari harisi iliyokuwepo katika kipindi hicho cha mitihani na vilio na mateso mengi yaliyoukuta mkoa kutokana na tetemeko, mmeonesha ushujaa mkubwa sana.
Hizi pongezi ni kubwa mno kwani licha ya kuongoza lakini mmeweza pia kuingiza halmashauri 3 kati ya 10 bora huku ya kwanza ikiwa ni manispaa ya Bukoba, zingine ni Biharamulo 8 na Muleba ikishika nafasi ya 10. Kwa takwimu mmekuwa juu sana kwani karibu kila kundi mmetokea, kuanzia shule 10 bora (Kaizirege) na wanafunzi 10 bora, lakini pia kwenye shule zilizofanya vizuri zaidi (St.Peter Clavery)
Yako mengi ya kusifia na kusisitiza lakini muhimu ni kuwapongeza sana, tunaamini hii ni njia tuliyopotea mda mrefu na sasa taratibu tumerudi kwenye historia yetu kwani sifa moja kuu ya historia ni kwamba huweza kujirudia. Mkoa kuwa maskini haimaanishi vichwani pia kumelala, na njia ya kwanza kabisa kupambana na adui umaskini ni elimu. Hakikisheni moto huu hauzimiki kamwe, iwekeni Kagera iwe kiwanda cha kila mhitaji wa maendeleo ya elimu kwake na kwa ndugu na mwanae.
Hatusahau nafasi nzuri zinazochukuliwa na Kaizirege kila mwaka katika mitihani ngazi tofauti, hakika mnastahili heshima yenu na pongezi kubwa.
NB: Mapambano yaendelee.