Uchaguzi 2020 Hongera John Mnyika uliona mbali kuliachia Jimbo kwa heshima

Kajeba

JF-Expert Member
Oct 15, 2020
820
1,961
Hakika aliyewahi kuwa mbunge wa Kibamba Mheshimiwa John Mnyika aliyaona yatakayotokea katika uchaguzi mkuu 2020.

Aliamua kustaafu ubunge kwa kutokugombea na kupisha nafasi kwa wanachadema wengine kushindania.

Wengi na mimi nikiwemo tulijiuliza kulikoni mtu asigombee kutetea kiti cha ubunge kuwakilisha wananchi wake?

Mnyika aliona mbali na alikuwa na siri ya matokeo ya Uchaguzi huu.

Hakika Mnyika ameitunza heshima yake kwa kustaafu kiheshima kuwatumikia wananchi wa kibamba.
 
Kama ruzuku yote ilikuwa inaishia kwa Mbowe, hela za wafadhili kwa Mbowe, hakuna ofisi ya chama siyo makao makuu wala majimboni, achilia kwenye mashina. Maajabu wanasubiri ushindi kama wana wa Isarel walivyoshushiwa mana jangwani. Ukweli ni kwamba Mnyika hana raha kabisa, ni basi tu hana jinsi. Siyo ajabu hata hiyo nafasi ya KM akiitema, kwa kisingizio cha kustaafu siasa. Mbowe ameua upinzani tz.
 
Back
Top Bottom