Hongera jk kwa kuzuia vibanda vyetu kubomolewa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera jk kwa kuzuia vibanda vyetu kubomolewa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by muzachai, Mar 22, 2011.

 1. m

  muzachai Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu wa nchi.

  Nakumbuka usemi wa mzee mmoja ambae alisema" atakachosema mkuu wa nchi hadharani kugeuka kama sheria" . hivyo basi tunaomba TANROAD , watendaji wa ardhi MTULIE. Acheni kutunyanyasa tumejima we kukajenga sasa mnatuonea donge na tujibanda twetu kwa sababu nyie bado mnapanga huko sinza na masaki. Asante mkuu maana sasa hivi tutalala usingizi mololo. jamani usiombe nyumba yako kupigiwa x .
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,332
  Trophy Points: 280
  hongera kwa lipi? angewachukulia hatua wale wote waliotoa viwanja na kuruhusu ujenzi kwenye hifadhi za barabara bila kufuata sheria za nchi.
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Raisi anashiriki kuvunja sheria kwa maslahi ya chama...anatafuta public support kutoka kila angle..imagine waziri husika amekuwa demoralized kiasi gani sasa atafanya kazi nje ya job decription yake
   
 4. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ninapinga JK kupewa hongera kwa alililolifanya. ankatisha taamaa wafanyaji kazi wake hodari ..kwa manufaa na vijisifa dhaifu kabisa!!
   
 5. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  'Kweli tuu wazembe wa kufikiri. Mimi nakushauri kama kuna uwezekano utafute pengine hiyo iwe sehemu ya kuzugia. Nani anajua kesho watasema nini!a'
   
 6. S

  SuperNgekewa Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hongera ni kwa JK na pia Mzee Mizengo Pinda kwa kumzuia huyu mbomoaji na mzulumaji wa mali ya raia kinyume cha sheria, kinyume cha katiba na kinyume cha haki. Huyu jamaa tangu mwaka 1995 alipowazulumu wakazi wa Ubungo haki zao baada ya Anna Abdala kumkatalia Mkapa jukumu hilo kwa kuogopa dhambi ya kutenda dhuluma naye akamwomba Mkapa ampe yeye jukumu hilo la kuendesha dhukluma hiyo, tangu siku hiyo amekuwa akichakachua sheria za kutunga mwenyewe au za kizushi au zilizo-retroactive yaani zinazotungwa baadaye ili kudanganya umma kuwa yeye ndiye anayetekeleza sheria na siyo mvunjivu mkubwa wa sheria za nchi na haki za binadamu.


  Kuna mtu alisema kuwa huyu jamaa ana mdudu kichwani ndiyo maana anaona raha kuwavunjia watu nyumba bila kujali wala haki zao wala madhara yanayowapata. Watu wengi wamekufa kwa presha ya kuvunjiwa nyumba zao na kudhulumiwa mali zao na huyu jamaa anatumia jina la serikali kuendeleza maovu kinyume kabisa na majukumu ya msingi ya serikali ambayo ni kulinda uhai, mali na uhuru wa raia zake, raia mmoja mmoja na raia wote kwa jumla.


  Kwa bahati mbaya hii nchi yetu wasomi wengi waliopita chuo kikuu cha UDSM nao wana mdudu kichwani pia kwani wanafuhia dhuluma anazotendea wananchi huyu bwana wa Bomoa Bomoa baada ya akili zao kuchakachuliwa na Maprofesa wa Mlimani ambao mtezamo wao umekuwa hasi, unaopinga maendeleo ya watu binafsi na kufurahia kila wakati mtu anapofanya bidii ya kupiga hatua chache mbele anaporudishwa nyuma kwa bidii zake kuharibiwa na watendaji hasi wachache walioko serikalini.


  Ukweli ni kwamba katika nchii hii yetu raia wanajitahidi sana kupiga hatua za maendeleo mbele lakini kila baada ya muda si mrefu linajitokeza litendaji la serikali lenye choyo na roho mbaya hivyo linabomoa maendeleo ya raia ili kuwarudisha nyuma. Hii ndiyo sababu kubwa ya umaskini wetu kudumu kwa muda mrefu hivyo kwani watendaji serikalini waliochakachuliwa akili zao wako na wale Maprofessa wa UDSM wanaochakachua fikra za watu kwa kuwafundisha mtezamo wa kubomoa huku wakijitia kuwa wanajenga bado wako, wengine tangu miaka ya sabini.


  Hawa wabomoaji wanapenda mambo ya nyuma nyuma tu hawataki watu wanaosonga mbele na ndiyo maana wanafurahia kila wanapoona mwananchi anayepiga hatua moja mbele anarudishwa hatua mbili nyuma.


  Huyu Magufuli anatoka huko kwao Chato. Mimi naamini kabisa kuwa picha ya barabara aliyokuja nayo mjini ni ya njia ya ng'ombe ya huko kwao Chato kwani hajui kabisa kuwa kando kando ya barabara kunakaa kitu kingine chochote isipokuwa vichaka tu na ameshindwa kabisa kuelewa kuwa barabara zinajengwa kwa ajili ya matumizi ya watu na siyo ili zikae hapo tu mbali na makazi ya watu kama vianzio vya maji.


  Mungu awajalie Mhe Pinda na Mhe JK kwa kutofumbia macho maovu ya mmoja wa watendaji wakuu wa serikali na ni matumaini yetu kuwa watajenga utamaduni mpya wa kukosoana kuanzia ndani ya Cabinet na siyo kuendeleza ule utamaduni wa kuoneana haya huku ikijulikana wazi kuwa mmoja wao anaharibu na kuendeleza dhuluma na hata uvunjaji sheria na wa katiba ya nchi.
   
Loading...