"Hongera JK kwa kukuza uchumi"-watanzania wa Australia

It is encouraging !!! Kumbe kuna wanaoyaona mazuri ya JK ?? Nilizoea kusoma madongo tu !!
Umoja wa Watanzania waishio Australia umempöngeza rais Kikwete kwa kukuza uchumi wa nchi,na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 dunian,ambazo uchumi wake unakua kwa kasi sana.
Pia wamempongeza kwa kuruhusu uhuru wa habari,kwani japo wao wapo ughaibuni lakin wanapata habari
sosi:habari kwa ufupi ya saa kumi alasiri@ radio one
 
yes yes yes and now the USD is 1900 kweli uchumi unakua

Umoja wa Watanzania waishio Australia umempöngeza rais Kikwete kwa kukuza uchumi wa nchi,na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 dunian,ambazo uchumi wake unakua kwa kasi sana.
Pia wamempongeza kwa kuruhusu uhuru wa habari,kwani japo wao wapo ughaibuni lakin wanapata habari
sosi:habari kwa ufupi ya saa kumi alasiri@ radio one
 
Alieandika kitabu cha Mfalme Juha aliona Mbali
Tuna mengi ya kushangaa Tanzania mwaka huu! Yaani ile ya juzi wa wasomi wetu wa mlimani kumtunuku jamaa udaktari wa heshima wa sheria kwa kushindwa kusimamia sheria zilizopo zifanye kazi haijapoa vichwani, leo hii wanajitokeza wengine wanampongeza kwa kukuza uchumi aliouua kabisa!! Ama kweli duniani kuna mambo!!!
 
Unajua ukiwa nje muda mrefu na akili zako zinakuwa nje, kumpongeza raisi kwa uchumi kukua kwa kasi!!! Sidhani hawa nduguzetu walimpongeza kweli? Kwani karibu watanzania milo mitatu inakuwa ndoto na hiyo sio vijijini tu hata dar es salaam watu wanapata mlo wa jioni tu, hata nbauli watu hawana, mafuta bei juu, gase bei juu, shilingi inashuka thamani kila kukicha,deni la dowance lipo palepale, mwarabu wa loliondo kauziwa watu kama wanyama, iptl ipo pale pale inakula fedha kiulaini, vyombo ya usalama na mihimili la dola vimekithiri rushwa, vituo vya police vinafanya kazi kwa command ya baadhi ya matajiri wasiojua hata mguu upande mguu sawa, tenda zxa silaha jeshini kapewa rostam azizi, hospitali hazina dawa, na dawa zilizopo hazitibu, shule hazina walimu, wanaharakati wanapuuzwa na kutishiwa kuuwawa,

Wenzetu huko nje msimuone raisi kama Mungu ni mtu wa kawaida na hizi sio zama za kumtukuza wakati taifa letu linaangania mikononi mwake.
 
Ni kweli uchumi unakua kwa kasi sana si mnaona inflation ni 17% pamoja shilingi imeongezeke thaman dhid ya $<1$= 1800> hongera jk na watanzania wa aus
 
Ni kweli uchumi unakua kwa kasi sana si mnaona inflation ni 17% pamoja shilingi imeongezeke thaman dhid ya $<1$= 1800> hongera jk na watanzania wa aus

labda wenzetu wana vyanzo vyao,but kwanin jeykei asiwashushue?
 
Siamini kama haya ni mawazo ya watu walio sincere zaidi ya kuwa mawazo ya wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Australia. Kama ni mawazo ya watanzania waishio Australia basi hawana maana na warejee Bongo wafaidi huo uchumi wanaousifia. Huwezi kukuza uchumi chini ya serikali ya kifisadi na kisanii yenye kuendeshwa na kujuana na kulipana fadhila. Uchumi ungekuwa unakua shilingi yetu isingeanguka anguka kama alivyokuwa akianguka anguka Kikwete wakati wa kampeni. Shilingi yetu, waambiwe, iko ICU. Tunazidiwa hata na sarafu ya Burundi na DRC pamoja na vita yao ya miaka mingi! Kilichokua Tanzania ni ufisadi na usanii. Huwezi kukuza uchumi chini ya mgao wa umeme na ulanguzi wa mafuta. Kama haya ni mawazo ya watanzania waishio Australia basi ni wa kuhurumiwa na waliyemwambia hawamheshimu kwani wamempa uongo na sifa za hovyo.
 
Acha kutuchefua mkuu. watu tumekimbia nchi, wewe unasema kuna maendeleo? yepi hayo? subiri uone bomu la ajira kwa vijana, miaka 2 au 3 ijayo
 
Back
Top Bottom