Hongera JamiiForums, Sauti yenu Imefika Wizara ya Elimu kuhusu Watoto kutokufunga Shule Likizo

Huyo mvula jamaaa ana screenshots zake zote na by then jamaa alihack namba za mkewe jamaa huwezi jua kama hio ishu anayo kichwani, anaendelea na maisha yake anasema anasubiria muda sahihi na sehemu sahihi
Hata mimi nimem mind kinoma Mvula. Nimgekua na cha kumchangia mwana ningempa hata hela ya bisibisi tu. Ila shemeji yetu naye anazingua mwambie amwache
 
Huyo aliesign barua kwa niaba ya katibu mkuu ndio anatoka na mke wa mshikaji na ashapigiwa simu na mshikaji ila bado anaendelea
Sasa hapo mwenye kosa ni nani kati ya huyo jamaa anayetoka na huyo mwanamke au huyo mwanamke wa jamaa yako. Kama unampenda sana rafiki yako mwambie aachae na huyo mke wake kwa sababu atakuwa hampendi jamaa yako. Ukiona mke au rafiki yako wa kike anatembea na mwanaume mwingine mpaka wewe umejua na yeye amejua na umeshamkanya na bado anaendelea kutembea naye wewe jua kabisa hakupendi kwa hiyo kula kona vinginevyo jela itakua inakuita kama sio kitanzi kabisa. Ila wanaume wengine wana moyo sana mpaka unampigia simu mtu anayemlamba mkeo aka "mume mwenza" daa unaongea nini sasa na yeye.
 
Sasa hapo mwenye kosa ni nani kati ya huyo jamaa anayetoka na huyo mwanamke au huyo mwanamke wa jamaa yako. Kama unampenda sana rafiki yako mwambie aachae na huyo mke wake kwa sababu atakuwa hampendi jamaa yako. Ukiona mke au rafiki yako wa kike anatembea na mwanaume mwingine mpaka wewe umejua na yeye amejua na umeshamkanya na bado anaendelea kutembea naye wewe jua kabisa hakupendi kwa hiyo kula kona vinginevyo jela itakua inakuita kama sio kitanzi kabisa. Ila wanaume wengine wana moyo sana mpaka unampigia simu mtu anayemlamba mkeo aka "mume mwenza" daa unaongea nini sasa na yeye.
Jamaa ni mafia ngoja tumuache tu tuone yajayo ntawajuza next episodes
 
Jamaa ni mafia ngoja tumuache tu tuone yajayo ntawajuza next episodes
Mwambie jamaa yako "black and white" kuwa mke wake hampendi kabisa kwa sababu kwa tabia za wanawake zilivyo akipenda amependa kweli kwa hiyo hapa penzi limeshahamia kwa huyo jamaa wa wizarani ndio maana pamoja na mumewe kujua na kumkanya bado anaendelea na huyo jamaa wa wizarani. Pamoja na umafia wake yeye aachane nao kwani mara nyingine huwa unafeli anaweza jikuta yupo nyuma ja nondo au kaburini kabisa halafu kawaacha watuhumiwa wake wazima huku wanaendelea na starehe zao yeye mnampeleka tu stori siku za "visitor" akiwa lupango.
 
Hili suala la kuwabakiza watoto shuleni sioni kama lina tija. Na sasa limekuwa suala sugu kwa sababu ni mwaka wa tatu sasa linajadiliwa linaishia hewani kwa sababu wizara ya elimu na hususan waziri wa elimu mwenyewe hajawahi kutoa tamko lolote lile kwa mdomo wala maandishi. Na sina hakika sana hata bungeni ambako kuna wawakilishi wa wananchi limewahi kuzungumziwa kwa upana katika hii miaka miwili mitatu linapoibuka na kupotea mitandaoni. Ni wakati sasa kwa serikali itoe tamko ili ijulikane inasimamia wapi kwenye hili suala.

Kwa mtizamo wangu mimi binafsi ni kweli watoto wanatakiwa kusoma sana lakini likizo ina sehemu yake na manufaa yake makubwa tu kiafya na kijamii. Nawashangaa sana wazazi wanaokomaa eti mtoto abaki shuleni wakati wa likizo hivi wamejiuliza iwapo wao wangeambiwa wabaki vyuoni wakati wanasoma mwaka mzima ili wafaulu wangekubali? Je sasa hivi kwa wafanyakazi wapo tayari kufanya kazi mwaka mzima bila kuchukua likizo? Mimi nafikiri waliotunga mitaala ya elimu walikuwa na sababu za msingi sana kuweka vipindi vya likizo tena vinne kwa mwaka mmoja wa masomo. Roboti tu ndio halipumziki lakini mwanadamu wa kawaida lazima apumzike na zaidi kabisa awe mbali na sehemu husika ili abadilishe mazingira ili arudi sawa tena.

Wanafunzi kama ni wa kufaulu ni wakufaulu tu na kama ni wa kufeli ni wakufeli tu. Hivi wale wote walisoma tangu zamani miaka ya 1961 mpaka miaka ya hivi karibuni hizi shule zilipoanzisha huu utaratibu wa kuwabakisha watoto shule walikuwa hawafaulu? Na mbaya zaidi nyingi kati ya hizi shule za siku hizi hazina vipindi vya dini jioni, vina viwanja vya michezo lakini havitumika kwa muhula mzima, wameajiri wafanya kazi wa kufanya usafi wa mabweni, vyoo na kusafisha mazingira, hazina hata busatni za mbaoga wala maua, hakuna "debate" ili kukuza uelewa, hakuna "social clubs" zaidi ni kukaririshwa ili wafaulu mitihani. Hata zile mechi za mpira kati ya shule na shule za karibu hakuna siku hizi eti wanaona wanafunzi wanapoteza muda wa masomo. Mwanafunzi akiamshwa asubuhi ni mwendo mdundo "dose"ya kusoma siku nzima mpaka saa nne usiku kwa mwaka mzima.

Na kuna suala lingine kubwa ambalo linaachwa lakini nafikiri baadae litaleta madhara makubwa sana kwenye nchi. Siku hizi watoto wa shule za msingi wanalazimishwa wanunue "counter books" kuanzia darasa la tatu. Na mbaya zaidi anabeba za masomo yote pamoja na vitabu kuanzia jumatatu mpaka ijumaa. Ukiuliza walimu kwa nini wasitoe ratiba ya masomo wanajiumama tu ohoo mwanafunzi aje nazo tu saa nyingine mwalimu wa somo husika hatakuwepo kwa hiyo eti anaweza kuingia mwalimu mwingine. Najiuliza tu tunambebesha huyo mtoto wa miaka saba nane (siku hizi watoto wanaanza shule mapema sana) mzigo wa "counter books" 3 quire zisizopungua saba ongeza na vitabu kwa wastani vitano hivi kama taifa tumejiaandaaje kuja kuwatibu wagonjwa watarajiwa wa migongo miaka michache ijayo? Na mbaya zaidi siku hizi watoto wana miili midogo sijui hata ni kwanini basi tabu tupu. Hivi siku hizi wanasoma nini cha ajabu huko shule za msingi mpaka wabebe madaftari makubwa hivyo wakati sisi zamani tulikuwa tunatumia tu kidaftari cha "sungura" na kinatosha? Wahusika wa elimu watusaidie katika hili kupitia wakaguzi elimu kata wahakikishe kila shule za serikali na binafsi zinakuwa na ratiba ya masomo na kila mzazi aipate ili awe anampangia mtoto masomo ya kila siku na ukizingatia siku hizi kuna "diary" itakuwa zoezi rahisi. Na kila mwanafunzi anaweza kuwa na daftri moja la "rough" analibeba kila siku ikitokea ratiba imebadilika akalitumia kuandikia somo lolote baadae akahamishie kwenye daftari husika nyumbani kama ilivyokuwa zamani. Njia hii ikitumika basi watoto wetu watakuwa wanabeba madaftari 3 - 4 kwa siku kitu ambacho ndio sahihi kwa umri wao. Vinginevyo hali ikiendelea kama ilvyo tunweza kuwa na taifa la watu waliopinda migongo huko mbele ya safari.
 
Elimu inahitaji marekebisho makubwa sana, hii ya Sasa haimsaidii mtu kutatua changamoto zinazomkabili yeye mwenyewe, na mwisho wa siku anakuwa Hana maajabu kwa jamii yake iliyotumia karibu nusu ya kipato chake Kama siyo chote kumwelimisha kijana huyo.
 
Ni jambo zuri, ila sasa nanyi muwe wazazi sasa, muwape muda wenu. Sio ndio wabaki kulelewa na tv na housegirl kwakuwa mko busy.
 
Ni jambo zuri, ila sasa nanyi muwe wazazi sasa, muwape muda wenu. Sio ndio wabaki kulelewa na tv na housegirl kwakuwa mko busy.
Hahahaha umeandika kwa hasira sana sana
 
Wenye kuona mbali wamegundua mbinu hizo zina madhara makubwa zaidi kwa mtoto hapo baadae kuliko faida ya ufaulu mitihani ya kitaifa. "Fatigue kills faster than pride/ego!"

Hivi darasa la nne kuna nini cha kuwafanya wasiende likizo?Huo mtihani ni mgumu kihivyo?????
 
Ni sahihi ila Walioweka likizo sio Wajinga, watoto wanahitaji mapumziko ujue. Kuna extra curricular activities. Sasa kuwashindilia tu masomo mwanzo mwisho ni kuwakaririsha, which is not health at all
Wanapumzika jumapili
 
Shule ilikua sehemu nzuri sana ya socialization na skill building na sio kukaririshwa.
Tulikua na nyakati za kucheza, kufurahi, kusali na kusoma!

Elimu ya Tanzania inajenga kaburi kubwa sana kwa future ya Watoto wetu

Inaua creativity, kwa mfano, kwanini shule zinunue mboga za majani wakati wangeweza kuwa na bustani za mchicha, tembele etc? Huyu mtoto hajui hata spinach kama inapandwa au inachimbwa.

What a shame?
Wakianza kulima tena mtauliza.

Shule wameenda kulima au kusoma?
 
Wadau huyu Mathias I Mvula anamawasiliano ya kimapenzi na mke wa rafiki yangu tunamtafuta kwa yeyote aliepo Dodoma tafadhari mpaka alishawahi pigiwa simu kuonywa na bado akaendelea yakihitajika na mengine tutayafikisha kwawaziri husika huyu mwanamke yupo morogoro shule za manispaa, aliwahi kumfundisha Ilonga chuo cha walimu kilosa. Popote ulipo Mathias I Mvula ujipange haswaa kwa hilo.
Hahahaha shenzi Sana
 
Hahahaha umeandika kwa hasira sana sana
Wala, nakerwaga tu na wazazi wasiosimamia nafasi zao ipasavyo.
Maana utakuta haya malalamiko si kwasababu wanataka watoto wapumzike ila kwasababu tu wanatoa pesa. Baada ya hapo sasa mtoto atajijua mwenyewe hata muda nae hana.
 
Wadau huyu Mathias I Mvula anamawasiliano ya kimapenzi na mke wa rafiki yangu tunamtafuta kwa yeyote aliepo Dodoma tafadhari mpaka alishawahi pigiwa simu kuonywa na bado akaendelea yakihitajika na mengine tutayafikisha kwawaziri husika huyu mwanamke yupo morogoro shule za manispaa, aliwahi kumfundisha Ilonga chuo cha walimu kilosa. Popote ulipo Mathias I Mvula ujipange haswaa kwa hilo.
Mweeh!!
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom