Hongera Jakaya Kikwete vision yako ya kujenga barabara zinazopita juu leo imetimia, wewe ni ‘true leader’

Kama huelewi basi utakuwa mbumbumbu sana ! ni hivi , hakuna anayepinga yanayoendelea bali kinachopingwa ni upotoshaji , SEMENI UKWELI KUHUSU WALIOANZISHA HII MIRADI BADALA YA KUWASIFU WATU WASIO NA MAONO , awamu ya 4 ilifanya yake na awamu ya 5 imeamua kuwa na kipaumbele cha kuua upinzani na kutokomeza demokrasia , mnaficha nini ?
Kwahiyo awam hii haina lolote ktk swala la flyover?
 
Kikwete kafanya mengi sana nchi hii, kweli alikua na mapungufu yake kama kila binaadamu, ila apewe haki yake.

97% ya nchi nzima alitandika barabara kama sio ya lami basi kiwango cha lami, katika uongizi wake. Hii pekeee ni jambo la kumsifia yule mzee.

Nakumbuka kipindi anakua Rais, njia ya kati lami ilikua inaishia Kabla ya kufika Dodoma, kuanzia hapo kama unaelekea mwanza/kigoma/bukoba unaweza ukatenguka kiuno.
 
Kikwete pamoja na kuwa alikua Mwizi ila alijua kula na vipofu

Daraja la kigamboni, Magari ya mwendokasi, na ili daraja la Tazara

Jamaa alikua na vision ya kuona mbali na bright sana kwenye issues za kiuchumi

Huyu jamaa mpaka sasa ajazindua mradi wake hata mmoja tunasubiri labda SGR na Umeme wa maji kama atafanikiwa kabla ya Muda wake kuisha,
airport,stiglers gorge,sgr,tazara flyover,ubungo interchange,rbt nk yote nimeyasikia kipindi cha jk...labda kama nimekumbwa na ugonjwa wa akili leo ndo mniambie sgr ni ya awamu hii..nachompendea magufuli ni kuhakikisha udokozi hakuna..nadhani hili ndo ccm walilompitishia
 
RAIS Jakaya Kikwete, ameagiza hatua za haraka zichukuliwe, kujenga barabara zinazopita juu katika Jiji la Dar es Salaam, ili kupunguza misongamano mikubwa ya magari.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM alitoa agizo hilo juzi, baada ya kupewa taarifa ya utendaji ya CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu ya kukagua shughuli za CCM mkoani humo.

"Hili la flyovers lipewa kipaumbele ili tupunguze msongamano wa magari katika Dar es salaam. Tusipofanya hili jiji hili litakuwa halipitiki katika muda wa miaka mitano, ama hata katika miaka miwili ama mitatu ijayo," Rais Kikwete.

Rais Kikwetepia aliwaagiza wataalam wa mipango miji katika Jiji la Dar es Salaam, kuanza kupunguza maeneo yasiyopimwa kwa kuzingatia kuwa kwa sasa ni asilimia 30 ya jiji ndiyo iliyopimwa.

Alisema Jiji la Dar es Salaam, haliwezi kuendelea kupanuka bila mpangilio na kwamba wakati sasa umefika wa kuhakikisha kuwa linajengwa kwa kuzingatia mipango miji.

"Hatuwezi kuendelea namna hii na mji unaopanuka namna hii. Hili ni jambo zito, kubwa linalohitaji umakini wa haraka kutatuliwa. Ndio maana kipindupindu hakiishi katika mji huu." alisema Rais Kikwete baada ya kupata taarifa kutoka kwa watalaam wa huduma za maji, ardhi na barabara.

Katika mkutano huo, Rais Kikwete pia alipewa taarifa kuhusu hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ukosefu wa maji ya katika jiji hilo.

Rais Kikwete pia aliusifu utendaji wa CCM katika Mkoa wa Dar es Salaam akiwataka viongozi wa chama hicho kutafuta njia za haraka za kutatua matatizo ya wananchi.

"Angalieni na chunguzeni sana matatizo ya wananchi. Haya ndiyo muhimu kwetu kuyashughulikia, tena kwa haraka. Hii ndiyo nguvu ya chama chetu," amesema Mwenyekiti huyo wa CCM

Source: MWANANCHI

Post nzuri mkuu
 
Ukisha amua kupinga kila kitu unaamua kujitoa akili.
Ukweli ni hivi Nchi nchini ya CCM inakuwa ina mipango endelevu inayotekelezwa kwa vipindi.
Mfano Stiglers gorge ni mpango ulioanza tangu Kipindi cha Nyerere, Hizo flyover ni mipango ya Serekali zilizopiata hata Kuhamia Dodoma hivyo hivyo.
Hata Sera ya Viwanda ni Sera ya taifa iliyopitishwa tangu 1999.
Ni suala la Usimamizi...
Wapinzani wa Nchii wangekuja na Hoja Endelevu, sio kila kitu unalalamika na kulamba matapishi..
Moja ya Ahadi ya CHADEMA 2015 ilikuwa ni kupunguza kama sio kuondoa Foleni Dar Es Salaam, Cha ajabu hii initiative inachukuliwa wanalalamika
 
Yeah, vision yake imeanza kuleta matunda. We need visionary leaders, sio kubwatuka majukwaani tu

Kikwete alikuwa hana vision yeyote alikuwa pale kutuibia akiwatumia wakina HOME SHOPPING CENTRE na kuficha hizo pesa ughaibuni huko anakokwenda kubembea kila leo!! Kaingiza nchi hasara kwa kuingia mikataba mibovu na WACHINA kwa faida zake binafsi; na mpaka leo ile mikataba aliosaini karibu anaondoka imefichwa ili asiumbuke!!
 
KIA Terminals jamaa ndio kafanyia mambo...
Thanks KIKWETE

Unamshukuru kwa kwenda kukopa China kujenga uwanja lakini mkishindwa kulipa deni WACHINA wachukue uwanja? Hizo ndio terms za mikopo aliochukua Kikwete toka China!!! Wanatuficha ama sivyo watu wangechachamaa kwa kuweka nchi rehani.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom