Hongera IGP Sirro kwa kukomesha mauaji Kibiti

Tunaambiwa uko watu wa mabakamabaka wabatoa dozi nzito kwa Raia sio mchezo alafu wewe unatoa pongezi?
 
Kama ndivyo basi kheri na ametimiza wajibu wake kamanda mkuu wa police
 
Ni kawaida yetu sisi watu wa mkoa wa Mara huwa hatutaki "usengerema" ukimwaga mboga tunamwaga ugali.
Sirro mura piga kazi sisi tupo hapa Bumera tunakura kichuri na kimoro!
 
Habari za jioni Kamarada

Kwanza kabisa napenda kumpongeza kamanda Sirro kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya mda mfupi lakini ameweza kuzima jaribio ovu la kutaka kutuchafulia amani yetu hasa siai watu wa pwani.
Siwezi sema kama amemaliza kabisa tatizo ila kwa sisi tunaojua mbinu aliyotumia ni mbinu za kisasa zaidi na bora maana tangu umeutwaa uIGP hali inaelekea kurudi katika kawaida yake.

Ombi langu endelea na jitihada hizo kuturudishia amani yetu ambayo wapo waliokuwa wanatusema eti kwa kuwa mkoa ni wa pwani basi itakuwa ni magaidi ya Kiislam ndio yanayoua watu kumbe ishu zilikuwa na siasa ndani yake.
Na wale walikuwa au ni majambazi tu na wauaji kama walivyo wauaji wengine

Asante Sirro, asante Serikali.
Mbona tumeambiwa jeshi limeenda kibiti kuimarisha ulinzi ? Sasa hapa mkweli nani ? Ww unayesema Sirro au hao waliotuambia jeshi ?
 
Habari za jioni Kamarada

Kwanza kabisa napenda kumpongeza kamanda Sirro kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani ya mda mfupi lakini ameweza kuzima jaribio ovu la kutaka kutuchafulia amani yetu hasa siai watu wa pwani.
Siwezi sema kama amemaliza kabisa tatizo ila kwa sisi tunaojua mbinu aliyotumia ni mbinu za kisasa zaidi na bora maana tangu umeutwaa uIGP hali inaelekea kurudi katika kawaida yake.

Ombi langu endelea na jitihada hizo kuturudishia amani yetu ambayo wapo waliokuwa wanatusema eti kwa kuwa mkoa ni wa pwani basi itakuwa ni magaidi ya Kiislam ndio yanayoua watu kumbe ishu zilikuwa na siasa ndani yake.
Na wale walikuwa au ni majambazi tu na wauaji kama walivyo wauaji wengine

Asante Sirro, asante Serikali.

Kwa kukusaidia tu Mkuu siyo IGP Sirro wala Askari wake ndiyo wameituliza Kibiti, Rufiji na Mkoa wote huo wa Pwani kwa sasa isipokuwa Maadili ya Kizalendo kwa nchi yangu ya Tanzania hayaniruhusu kuweka kila kitu hapa hadharani ila itoshe tu kukutaarifu kuwa kinachoendelea huko kwa sasa hivi hao Wauwaji wanajutia yale yote waliyoyafanya. Kila la kheri Mkuu!
 
Ni kwamba huna taarifa ya kinachoendelea Kule hivi sasa, lands kwa sababa hi I Sasa 'taa' zimeshazimwa kule na jamuwezi tens 'kuona' yanayotokea. Baki hivyo hivyo na mkiweza endeleeni kipongeza press conferences na maandamano.
 
Jeshi la police limeshindwa,kuna mtu amenieleza limekwenda JWTZ!hivyo ikiwa hivyo sirro hausiki hapo!
 
Tofautisha kati ya kukomeshwa na kutoripotiwa...saa hizi kinachofanywa ni SKSB ( silent killing silent burring) media zote ziko busy na report za Makinikia sio mauaji
 
Back
Top Bottom