Hongera Habarileo-Mnatenda haki kwa vyama vyote arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Habarileo-Mnatenda haki kwa vyama vyote arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by engmtolera, Mar 16, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  1.Habari ya CCM


  MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wassira ameshangazwa na kulaani tabia iliyoanza kuoneshwa na vijana wa Chadema, katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, Arumeru

  Mashariki za kumkashifu Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

  Akimnadi mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM, Sioi Sumari jana katika Kata ya Makiba,
  Wassira alisema kitendo kinachofanywa na vijana wa Chadema kumtukana Mkapa majukwaani ni kibaya na cha kusikitisha na kinaweza kuleta athari kubwa kwa vizazi vya kesho.

  2.HABARI YA CHADEMA

  Naye Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema), amelitaka Jeshi la Polisi nchini kutoa ufafanuzi wa hatua yake ya kupeleka magari maalumu ya kutuliza ghasia “washawasha” na mabomu ya kutoa machozi Arumeru Mashariki zinakoendelea kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Ndesamburo alidai kuwa kutokana na hatua hiyo, Chadema, imekosa imani na Polisi kutokana na kampeni za uchaguzi wa Arumeru Mashariki kugubikwa na hali ya wasiwasi.

  Alisema chama chake hakikubaliani na hatua ya kupeleka magari hayo jimboni humo, kwani
  ni kutisha wapigakura.

  Ndesamburo anadai kuwa tangu Tanzania iingie kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa, vyombo vya Dola ikiwamo Polisi, vimekuwa vikitumika visivyo kwa maslahi ya kisiasa.

  Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Kilimanjaro, alidai kuwa wakati kampeni za uchaguzi zikiendelea kabla ya uchaguzi kufanyika Aprili mosi, kumekuwa na wasiwasi juu ya mafunzo ya kijeshi yanayotolewa katika Chuo cha Polisi (CCP) Moshi.

  Alitaka Polisi itoe maelezo ya haraka kuhusu mafunzo hayo katika chuo hicho kama yana nia na dhamira njema au yanalenga kutumika Arumeru Mashariki kwa lengo la kutisha wananchi wakati wa kampeni na siku ya uchaguzi.

  Ndesamburo alisema ni matarajio ya Chadema kuwa wingu hilo ambalo limetanda Arumeru litapatiwa ufumbuzi wa haraka ili haki na demokrasia ya kweli ipatikane.

  3.HABARI ZA KIPOLISI

  Mkuu wa CCP, Matanga Mbushi, alipotafutwa kuzungumzia madai ya Chadema hakupatikana kwa simu.

  4.HABARI YA TLP


  TLP yalia Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema juzi

  alilalamikia ratiba iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa ni finyu na imelenga kutoa muda mrefu wa kunadi sera kwa CCM na Chadema.

  Alisema ratiba hiyo iliyotolewa na NEC imeonesha CCM itakuwa na mikutano 1,961 , Chadema 642 na TLP 523.

  Alisisitiza kuwa ratiba hiyo imelenga kukikomoa chama chake, kwani muda wa kuanza mkutano ni finyu na sehemu ilikopangwa ni mbali na muda hautoshi.

  Mrema alisema hayo alipozindua kampeni ya kumnadi mgombea wa chama chake, Abraham
  Chipaka, uliofanyika Tengeru karibu na Uwanja wa Patandi.

  Alisema ratiba iliyopangwa ni finyu na wakati mwingine haikuzingatia umbali kutoka sehemu moja hadi nyingine na kwamba ratiba hiyo imelenga kunufaisha CCM na Chadema kutokana na
  usafiri wanaotumia.

  Alisema TLP ni masikini na haitumii helkopta wala mbwembwe bali inamtanguliza Mungu kwa kila jambo, kwani anajua aliwafanyia nini Wameru kutokana na mgogoro uliosababisha watu kufa, makanisa kuchomwa moto na miti kufyekwa.

  "Eti wanasema nimechoka, wawaulize wananchi wa Vunjo watatoa jibu, ndiyo maana hata
  bungeni wamenipa cheo na kampeni zangu situmii helkopta, bali namtanguliza Mungu, hivyo
  wananchi wa Meru mchagueni Chipaka, ili asimamie mapato na matumizi ya Halmashauri ya
  Meru,” alisema Mrema.

  Aliongeza kuwa anatamani awachape viboko wezi, lakini wananchi watamchagua Chipaka ili
  adhibiti wizi unaofanywa na wachache serikalini, huku akijigamba kuwa hakuna ubunge wa dezo bali kuna ubunge wa kazi, hivyo aliwasihi wana Meru kutochagua mgombea ambaye anarithi kazi ya baba yake.

  Chipaka aliomba kura kwa wananchi hao, ili asimamie sera nzuri za chama hicho pamoja na
  kuwatoa wala rushwa aliodai wanakula fedha za halmashauri huku jimbo likikabiliwa na changamoto za ardhi, maji na nyinginezo.

  Alisema ametumwa na wazee 262 waliomwomba agombee na kwa sababu wazee ni watu wenye
  busara, ndiyo maana akajitokeza kuwania nafasi hiyo ili apeperushe bendera ya TLP na kuleta maendeleo.

  5.HABARI YA SAU

  Sau walia na Chadema

  Naye Katibu Mwenezi wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Johnson Mwangosi amempa siku nne Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumwomba radhi kutokana na kudai kuwa vyama vya upinzani vimeungana ili kuishinda CCM.

  Aidha, Chadema imedaiwa kuwa ni chama chenye uroho wa madaraka ndio maana wanakubali
  kutumia nguvu nyingi kusimamisha mgombea na kushindwa kwenye chaguzi mbalimbali.

  Mwangosi alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi
  wa kampeni za SAU pamoja na kutoa ufafanuzi wa kauli ya Mbowe kuhusu vyama vya upinzani kuungana.

  Alisema kauli hiyo, imempa shida kwani inaonekana yeye ni msaliti au mla rushwa kutokana na jambo hilo ndani ya chama hivyo ndio maana ameamua kutoa siku nne kwa Mbowe kumpigia simu na kumwomba radhi.

  Naye Mgombea wa SAU, Shabani Kirita alisema chama hicho kitatumia helikopta kwenye kampeni zao, ili kuyafikia maeneo mbalimbali kwa wakati huku akitamba kuwasaidia wakulima ili wanufaike na kilimo chao.

  6.HABARI YA CCM

  Mwigulu adai kutishiwa kifo

  Naye Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Taifa, Mwigulu Nchemba akizungumza na wakazi wa kijiji cha Valeska Kata ya Makiba, alisema amefika kwao kumshitaki Nassari kutokana na kumtishia kuwa atamuua kwa madai kwamba amekuwa akimsema vibaya katika mikutano mbalimbali jimboni humo.

  “Nilitaka kumshitaki kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) lakini nikaona hapana, dawa yake ni
  kumshitaki kwenu nyie wananchi ili mjue la kufanya. Ukiona kiongozi anafikia hatua ya kutishia kumuua mtu kama mimi ambaye ni Mbunge, itakuwaje kwa watu baki?

  7.HABARI YA NEC

  NEC yatupa pingamizi la Nassari
  Wakati huo huo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetupilia mbali rufaa iliyokatwa dhidi ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi kukataa pingamizi la Nassari lililodai kuwa Sioi si Mtanzania kwa kuwa alizaliwa Kenya.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Malaba alisema
  Tume imepitia sheria ya Tanzania pamoja na Katiba ya Kenya ya zamani ya mwaka 1963 ambayo inaonesha kuwa mtu yeyote aliyezaliwa Kenya baada ya mwaka 1963 atakuwa raia iwapo mzazi wake mmoja ni raia wa Kenya.

  Alisema pia kifungu cha sheria ya uraia namba 6 ya mwaka 1995 cha Sheria ya Tanzania, kimeweka bayana kuwa mtu aliyezaliwa nje ya Tanzania na baba yake au mama yake ni raia wa Tanzania hadhi ya mtu huyo inalindwa na ataendelea kuwa raia wa Tanzania.

  Pia hakuna ukomo wowote uliowekwa katika kifungu hiki dhidi ya uraia wa mtu wa namna
  hiyo.

  Vilevile alisema hakuna mahali popote sheria inapotamka mtu wa namna hiyo kuukana uraia wa nchi moja pale atakapofikia umri wa miaka kumi na nane, hivyo Sioi hakuwa na jukumu, wajibu au sababu ya kisheria ya kuukana uraia wowote baada ya kufikia umri wa miaka kumi na nane.

  Imeandikwa na Arnold Swai,Moshi na Oscar Mbuza na Veronica Mheta, Arumeru.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Hata usafishe kwa JIK habari leo hawana maana tangu enziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 3. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  tatizo langu mimi ni moja tu

  huwa siwezi kukaa kimya.penye YES nita sema penye NO nitasema,Fuatilia post zangu utaona

  sipo JF kumridhisha mtu ama kikundi furani(ukienda kombo iwe CDM OR CCM nitasema sina unafiki)
   
Loading...