Hongera "Dr. Slaa"

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
Ndugu wana JF imefika wakati tumeongea hali halisi
kuhusu kutenguliwa kwa GAVANA BALALI nami nimeona
ni vyema nimpongeze huyu bwana anaeitwa DK W. SLAA
tunafurahia mengi na kuchaguliwa kwa gavana mpya lakini
ni vyema tujue kama si huyu kiumbe wa mwenyezi mungu wngi wetu tusingejua kuna wanaotafuna in billions kule BOT,
Kibaya zaidi ni kwamba alikubali kusalimisha maisha yake na kukubali lolote na litokee ,,hakuna alsiejua hata ile email iliyosambaa dunia nzima baada ya kupelekwa kule bungeni mh spika
na ujumbe wake wakaikataa na kuamini yalikuwa ni majungu ya kuchafuana wapi wewe spika mbona uko kimya aeleze kuhusu ile email,,,,,napenda kumpongeza na huyu mkuu ametufundisha kwamba
kule bungeni si sehemu ya kutafuta mabibi ni wito na wanatakiwa kujua nini kilichowapeleka kule bungeni,,,,

2)SITOKUWA NA FADHILA KWA SPIKA KUMPONGEZA KIDOGO KWA KUKUBALI KUUNDWA HIZI KAMATA KWA SHINIKIZO,,TUNAAMINI MOYONI ALIJISIKIA VIBAYA LAKINI SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU,,,,TUNAKUSHAURI UFANE KAZI BILA KWA KULINDANA ,,,ONA SASA ULIKTAA KAMATI ZA MADINI,,RICHMOND SASA UNAPOKEA KWA MINKONO MIWILI REPORT ZA WAJUMBE,,,NAHISI ULIONA AIBU SANA KWA MBUNGE ULIEMFUKUZA NA BAADAE HUYOHUYO KUITWA KWENYE KAMATI YA KUNGALIA UPYA MIKATABA YA MADINI HALI AKIONDOKA BUNGENI KWA KILLIO HICHOHICHO MIMI KAMA MDAU NAKUSHAURI UFANYE KAZI KAMA INAVYOTAKIWA NA SI KAMA WAKINA EL,RA WANAVYOTAKA WATAKURUKA HAO SIKU YA SIKU,,,SUBIRI BOT INAKUJA HIYO SOMA VITUKO HUMO,,,USIJE UKAWA ULIKUWA MJUMBE WA BODI MOJAWAPO HUMO,,,MUWE MAKINI MPO PALE KWA AJILI YA WANANCHI NA SI VINGINEVYO,,

MWISHO TUNAOMBA BWANA SLAA USIFUNGWE MDOMO NA KESI YAKO
HIZO NI MBINU ZA SIASA,,,MWENYEZI MUNGU VILINDE VIUMBE HIVI
NAONA WANA JF TUWEPAMOJA KUWAPONGEZA WATU KAMA HAWA ,,BADALA YA KUPONGEZA KUTENGULIWA KWA GAVANA BALALI,,,HAKUNA ASIEJUA HUYU ALISHAJIUZULU SIKU NYINGI HAKUNA JIPYA HUO NI MCHANGA WA MAMCHOO

MWISHO NIMESOMA MARA GAVANA KAFA,,MAHUTUTI,,AMEZIDIWA..MWANAKIJIJI AKATUAMBIA ANAENDELEA VYEMA,,KAMA WATANZANIA TUOMBE MUNGU AILINDE KIUMBE HIKI,,,AWEZE KURUDI NC=HINI KUTUELEZA UCHAFU WA PALE BOT...AMIN MSIAMINI HUYU MTU NI MUHIMU KWA NCHII HII HIVI SAS AKULIKO HATA HUYO RAISI WETU ALIEMFUKUZA ,,ANAUWEZO WA KUTUFUNGULIA MENGI SANA PALE BOT NASI TUKAJUA KUMBE WAKO WENGI,,MUNGU AMLINDE BALALI,TUNAKUSUBIRI KWA HAMU TANZANIA

"" MUNGU IBARIKI TANZANIA""""
 
Pdiddy,
You have really put my thoughts in words,and very well indeed.
God Bless Dr Slaa and all those who are the voice of the Voiceless
 
Hata mkuki una chuma imara kilichochongoka mbele( Dr Slaa) halafu kipande cha mti( Wananchi JF ndani) kinachomekwa nyuma yake.

Chuma Kiko tayari kuanzisha Patashika wakati wowote na kile kipande cha mti kwa uaminifu hukifuata chuma kila kiendako.

Chuma pekee yake bila mti hufanya kazi kwa shida.
Mti pekee bila chuma pia huweza leta kasheshe lisilo penyeza ndani hadi kwenye kitovu.

lakini Chuma na Kipande cha mti kwa pamoja ni Kachumbari safi kwenye Ngozi nyororo za mafifadi.

Hongera sana Dr Slaa and the Team.
 
mie ninachotaka sasa iwe zamu ya spika na wenzie woote waliokua wanasema BOT hali ni shwari wawaombe msamaha wooote kina SLaa na wengineo...hivi kwanini miandishi yetu ya habari haifuatiliagi mambo ya ccm??lakini wakisikia mwanamuziki flani sijui kaachana na mkewe...kila gazeti litataka kujua ukweli na kureport
 
Hongera Dr Slaa unastahili pongezi! nitakuwa mwananchi nisiye na shukrani kwa huyu bwana,nchi yangu, na wananchi wengine kwa kutompongeza Dr.Slaa kwa kulishikia bango hili suala la BOT mpaka limeeleweka.
ILA USIISHIE HAPO bado buzwagi,Mkapa na Richmonduli

-Wembe
 
Kwa wakati huu, Tanzania inahitaji raisi aliye kama dr Slaa. Nchi ingesonga mbele. Mafisadi wangeshikishwa adabu. Mkapa angelamba pingu kwa kuinajisi ikulu yetu.

Lakini ndio hivyo tena. Wadanganyika ni wadanganyika tu. Usingizi ni mzito mno. Hiyo valium ya amani na utulivu tuliyonyweshwa sio mchezo.
 
Bravo Dr. Slaa, wapinzani kwa ujumla, JF na wanachi kwa kuwaunga mkono.

Kuna Swali najiuliza kila wakati na sipati majibu mtanisaidia.

Serikali iliuza mashirika mengi sana kupitia PSRC na watu walikua wanalipwa mishahara minono sana.

Je zilipatikana kiasi gani kwa mashirika yote na fedha zilizopatikana kutokana na uuuzaji huo zimekwenda wapi?

Kuna mashirika yaliyouzwa kwa mkopo kama TTCL, Yona/mkapa coal mine, Sumaye/Arusha Hotel na mengine, Je arrears ni kiasi gani na nini mpango wa serikali kupata madeni Hayo?
 
Watanzania wengi wanasubiri siku yao ifike nao watese na fedha za wizi.

Kukaa kwao kimya huko si kwa kuto jua maovu ni kwa kuona wataharibu kijiwe na hivyo zamu yao ikifika watapata nunge.

Wasijue kwamba wataishi kuhesabu Boriti usiku kwa kulala nusu njaa kila siku.
 
Mtaalam,
Unauliza ni kwa nini waandishi wetu wa habari hawafuatiliagi mambo? Jibu ni rahisi sana. Bahasha. Mimi nilitegemea maswali mengi baada ya rais kumtengua mtu aliyejiuzulu lakini kilichofuata ilikuwa ni misifa tu na jinsi rais alivyokasirishwa kana kwamba ndiyo mara ya kwanza kupata habari hizi.
 
Hata mkuki una chuma imara kilichochongoka mbele( Dr Slaa) halafu kipande cha mti( Wananchi JF ndani) kinachomekwa nyuma yake.

Chuma Kiko tayari kuanzisha Patashika wakati wowote na kile kipande cha mti kwa uaminifu hukifuata chuma kila kiendako.

Chuma pekee yake bila mti hufanya kazi kwa shida.

Mti pekee bila chuma pia huweza leta kasheshe lisilo penyeza ndani hadi kwenye kitovu.

lakini Chuma na Kipande cha mti kwa pamoja ni Kachumbari safi kwenye Ngozi nyororo za mafifadi.

Hongera sana Dr Slaa and the

HAPO JUU MKUU MADELA INABIDI NIKUPONGEZE KWA VINA
 
Bila kumsahau aliyeitoa habari hii hapa JF (Mgongo Mgongo au Mchambuzi?) Naegemea kuamini kuwa anastahili pongezi kwa kiwango kile kile cha Slaa.
 
Katika mizunguko na maongezi ya hapa na pale na watu tofauti, nimegundua wengi wao hawaoni umuhimu wa wapinzani kuwepo katika taifa letu. Wanawaona watu kama Dk Slaa, Zitto wana njaa na wanatafuta mahali pa kujipatia kula ndio maana wanasema wasemayo. Hawana imani kwamba wanaweza kupambana mpaka mwisho bila kunyamazishwa kwa kupewa bahasha nono.

Uzalendo wa watanzania wengi bado ni duni watu wengi hawana uchungu na nchii, na wengi wao hawawaungi mkono wale ambao wameonyesha uzalendo na mapenzi waliyonayo kwa nchi hii.

Dk. Slaa and your team dont give up, watanzania walio wengi wawe na imani na wapinzani na hapo ndipo malengo yatatimia. Muwe imara stand for what you beleive in na mjue kwamba wengi tuko nyuma yenu, tuna imani na nyinyi na kazi mnayoifanya. msituangushe kama wengi waliokuwepo hapo mwanzo
 
Kwa wakati huu, Tanzania inahitaji raisi aliye kama dr Slaa. Nchi ingesonga mbele. Mafisadi wangeshikishwa adabu. Mkapa angelamba pingu kwa kuinajisi ikulu yetu.

Lakini ndio hivyo tena. Wadanganyika ni wadanganyika tu. Usingizi ni mzito mno. Hiyo valium ya amani na utulivu tuliyonyweshwa sio mchezo.

wewe si unaona sasa hivi wanavyomwagia JK misifa eti kwa "kumfukuza" Balali, utafikiri nchi hii imelogwa na mchawi wake alishafariki!
 
Bila kumsahau aliyeitoa habari hii hapa JF (Mgongo Mgongo au Mchambuzi?) Naegemea kuamini kuwa anastahili pongezi kwa kiwango kile kile cha Slaa.

Aliyetoa habari hii kwanza ni Zanaki. Mugongo alileta ikiwa na 'exciting' heading.
 
Ndugu wana JF imefika wakati tumeongea hali halisi
kuhusu kutenguliwa kwa GAVANA BALALI nami nimeona
ni vyema nimpongeze huyu bwana anaeitwa DK W. SLAA
tunafurahia mengi na kuchaguliwa kwa gavana mpya lakini
ni vyema tujue kama si huyu kiumbe wa mwenyezi mungu wngi wetu tusingejua kuna wanaotafuna in billions kule BOT,
Kibaya zaidi ni kwamba alikubali kusalimisha maisha yake na kukubali lolote na litokee ,,hakuna alsiejua hata ile email iliyosambaa dunia nzima baada ya kupelekwa kule bungeni mh spika
na ujumbe wake wakaikataa na kuamini yalikuwa ni majungu ya kuchafuana wapi wewe spika mbona uko kimya aeleze kuhusu ile email,,,,,napenda kumpongeza na huyu mkuu ametufundisha kwamba
kule bungeni si sehemu ya kutafuta mabibi ni wito na wanatakiwa kujua nini kilichowapeleka kule bungeni,,,,

2)SITOKUWA NA FADHILA KWA SPIKA KUMPONGEZA KIDOGO KWA KUKUBALI KUUNDWA HIZI KAMATA KWA SHINIKIZO,,TUNAAMINI MOYONI ALIJISIKIA VIBAYA LAKINI SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU,,,,TUNAKUSHAURI UFANE KAZI BILA KWA KULINDANA ,,,ONA SASA ULIKTAA KAMATI ZA MADINI,,RICHMOND SASA UNAPOKEA KWA MINKONO MIWILI REPORT ZA WAJUMBE,,,NAHISI ULIONA AIBU SANA KWA MBUNGE ULIEMFUKUZA NA BAADAE HUYOHUYO KUITWA KWENYE KAMATI YA KUNGALIA UPYA MIKATABA YA MADINI HALI AKIONDOKA BUNGENI KWA KILLIO HICHOHICHO MIMI KAMA MDAU NAKUSHAURI UFANYE KAZI KAMA INAVYOTAKIWA NA SI KAMA WAKINA EL,RA WANAVYOTAKA WATAKURUKA HAO SIKU YA SIKU,,,SUBIRI BOT INAKUJA HIYO SOMA VITUKO HUMO,,,USIJE UKAWA ULIKUWA MJUMBE WA BODI MOJAWAPO HUMO,,,MUWE MAKINI MPO PALE KWA AJILI YA WANANCHI NA SI VINGINEVYO,,

MWISHO TUNAOMBA BWANA SLAA USIFUNGWE MDOMO NA KESI YAKO
HIZO NI MBINU ZA SIASA,,,MWENYEZI MUNGU VILINDE VIUMBE HIVI
NAONA WANA JF TUWEPAMOJA KUWAPONGEZA WATU KAMA HAWA ,,BADALA YA KUPONGEZA KUTENGULIWA KWA GAVANA BALALI,,,HAKUNA ASIEJUA HUYU ALISHAJIUZULU SIKU NYINGI HAKUNA JIPYA HUO NI MCHANGA WA MAMCHOO

MWISHO NIMESOMA MARA GAVANA KAFA,,MAHUTUTI,,AMEZIDIWA..MWANAKIJIJI AKATUAMBIA ANAENDELEA VYEMA,,KAMA WATANZANIA TUOMBE MUNGU AILINDE KIUMBE HIKI,,,AWEZE KURUDI NC=HINI KUTUELEZA UCHAFU WA PALE BOT...AMIN MSIAMINI HUYU MTU NI MUHIMU KWA NCHII HII HIVI SAS AKULIKO HATA HUYO RAISI WETU ALIEMFUKUZA ,,ANAUWEZO WA KUTUFUNGULIA MENGI SANA PALE BOT NASI TUKAJUA KUMBE WAKO WENGI,,MUNGU AMLINDE BALALI,TUNAKUSUBIRI KWA HAMU TANZANIA

"" MUNGU IBARIKI TANZANIA""""
Yaani spika wetu wa sasa ni bogus kuliko spika aliyepita yaani hatofautiani na kivuitu kwani wote wana shahada ya sheria ya hapo mlimani lakini mmh huyu jamaa kwa kuboronga,mambo ya OIC yeye ndiye alikuwa waziri wa sheria,na kuna scandal moja inamhusu hadi walitaka kumnyima uwakili sasa standards and speed zipi alizotupa? ni zile za kugombana na zitto kumbe anampa umaarufu?nachofahamu mimi spika anatakiwa awe ni mtu anayelijengea uwezo bunge yaani wabunge wake ili waweze kuibana serikali vizuri lakini spika tena anakuwa kufuli la kuwafunga midomo wabunge wasiikabe koo serikali sijapata kuona.kwani anaogopa nini chama?manaake spika hayupo responsible kwa serikali bali kwa wabunge waliomteua.Spika tanzania amegeuka kuwa executive anakuwa maarufu kuliko Pm wakati hapa Uk penyewe mie simjui spika wala sijawahi kumsikia kwenye vyombo vya habari,watu wanamsema Gordon Brown au Blair live sasa Sitta angekuwa ndio spika hapa si angemuomba Queen alivunje bunge?mmh spika komaza demokrasia ndani ya bunge,acha kuwa jaji ruhusu wakina slaa waseme,whats wrong with putting up an argument? kama sio kweli watapewa nafasi ya kubisha,lakini usimzibe mdomo mtoa hoja.
 
Mtaalam,
Unauliza ni kwa nini waandishi wetu wa habari hawafuatiliagi mambo? Jibu ni rahisi sana. Bahasha. Mimi nilitegemea maswali mengi baada ya rais kumtengua mtu aliyejiuzulu lakini kilichofuata ilikuwa ni misifa tu na jinsi rais alivyokasirishwa kana kwamba ndiyo mara ya kwanza kupata habari hizi.
Hili ndilo tatizo la mfumo wetu huu wa ministerial responsibility Balali kwa kuwa alikuwa bendera inayoonekana basi bendera imeshushwa na kuwekwa kapuni mlingoti ambao ndio shina lake umeachwa unasimama,sasa kwani balali ndio muhasibu wa benki? kwani balali wakati anafanya kazi idara zote yeye ndio alikuwa akiamua? si kulikuwa na vikao vya management? mmh hapa ndio huwa nachoka mi nilitegemea Balali afukuzwe kazi lakini pia menejiment nzima ya benki isimamishwe kazi,ili kuruhusu uchunguzi wa kina ufanyike wakati interim management inafanya kazi kwa niaba.Manaake balali haiyumkini hakuwa peke yake ana watu wake mle BOT baadhi ya nyaraka zitapotea tu.Watuambie pia balali aliko tukamtakie hali na kumuuliza vipi "ulikula na nani" au kaka ulilazimishwa na Benn,wee tueleze tu.
 
Mtaalam,
Unauliza ni kwa nini waandishi wetu wa habari hawafuatiliagi mambo? Jibu ni rahisi sana. Bahasha. Mimi nilitegemea maswali mengi baada ya rais kumtengua mtu aliyejiuzulu lakini kilichofuata ilikuwa ni misifa tu na jinsi rais alivyokasirishwa kana kwamba ndiyo mara ya kwanza kupata habari hizi.

Vyombo vya habari bongo vinasikitisha. Mimi nilitegemea kabisa kwa mfano Mzee Luhanjo aulizwe 'live' afafanue maana ya kutengua.

Halafu kuna vipindi vya luninga vya kitimoto, kama tuambie, tutafika? pambanua, na jenerali on monday. Sioni kama masuala mazito yanaongelewa, hasa yakiwahusisha watawala wakuu kama raisi, pm, vp, na mawaziri.

Kwa mfano nilisoma kutoka Raia Mwema kwamba PM Lowasa aliwahimiza wakulima wa tumbaku Tabora kulima zaidi; halafu kwa upande mwingine waziri wa kilimo Wasira akiwaambia wakulima wa tumbaku waachane na hicho kilino. Hapa ndipo ilitakiwa hasa akina Makwaia wa Kuhenga, na wenzake wawakalishe kiti moto uso kwa uso PM na waziri wake watetee misimamo yao. Lakini aahh! Bongo yetu hii sijui ni ufalme wa kijamhuri au jamhuri ya kifalme...am lost!

Ningependa kuona kwa mfano suala la katiba mpya lizue mjadala mkubwa. Jenerali Ulimwengu(channel 10), au tuambie ya TVT(sio tv ya serikali?) wakiwakutanisha 'live' wenyeviti wote wa vyama vya siasa kitaifa: JK uso kwa uso na Lipumba, Mbowe, Cheyo, Mbatia, Mrema, Mtikila, Makaidi, etc. Wananchi tupate kusikia kwanini katiba mpya ni lazima au sio lazima.

Waandishi mnatuangusha. Your journalism is too passive. Time to market is very important concept even in politics, or non-business issues. When an issue occurs, a reaction or comment should be immediate. This is what I mean by time to market.
 
Back
Top Bottom