Hongera Dr. Slaa kwa kuonesha ukomavu kwenye siasa

Yaani wewe unaweza kupongezwa huyo mtu ambaye aliwasaliti vijana na watanzania kwa ujumla wake? Wewe ni mtu wa ajabu sana ambaye unahitaji neema tu
 
kama kumkataa Lowasa ni usaliti,, inawezekana mnaosema Slaa ni msaliti hamjitambui
 
Tatizo liko hapa, unakumbuka ni nani alikua nyuma ya ule mbpango wake? Mbona alipokuja kuulizwa kwamba alionana na watu wa chama tawala hakukana? Unakumbuka yule binti mfanyakazi hotelini alipoteza kibarua kwa sababu gani? Unaposhabikia kitu jaribu kuwa objective.
Mkuu yule binti alisaidiwa ajira na UKAWA au ndio imekula kwake? Mida hii anauza nanilii ktk vioteli uchwara? Tupe mrejesho.
 
Nani ameonyesha ukomavu wa kisiasa kama Dr. Slaa kwenye siasa za vyama vingi Tanzania ya leo?

Amejitofautisha sana na wanasiasa uchwara wa bongo. Mungu akubariki sana huko uliko na akuzidishie sana tena sana. Wewe peke yako mpaka sasa ndo umedhihiri kuwa ulikuwa mwanasiasa wa kweli uliyekuwa ukisimamia kweli na haki. Hawa uliowaacha wengi wao ni akina pangu pakavu tia mchuzi.

Wengi wao wameendekeza zaidi umimi, tumbo, fitina, majungu na chuki.

Mtaje nani unayemjua wewe aliye zaidi ya Dr. Slaa?

juma
 
Hata kama! Mlikosea kumpokea MTU mliyetuambia fisadi na ushahidi mlisema mnao!! Dunia nzima inawashangaa kwa unafiki wenu!!

Unaweza kuweka ushabiki pembeni tukaongelea ishu inayojadiliwa? Nani kakwambia mimi ni CDM au nilimpokea fisadi?
Falsafa yangu ni moja tu, mtu akikosea bila kujali chama, akosolewe, akifanya jambo jema hali kadhalika apongezwe.
Akienda kinyume cha taratibu na sheria, sheria na kanuni za nchi zichukue mkondo wake kwa mujibu wa katiba. Soma heading ya thread, soma nilichopost kisha changia kwa muktadha huo, vinginevyo endelea na malumbano.
 
Mkuu yule binti alisaidiwa ajira na UKAWA au ndio imekula kwake? Mida hii anauza nanilii ktk vioteli uchwara? Tupe mrejesho.

Point hapa ni kwamba, alisaidia kufichua ukweli na siri iliyokua imejificha nyumba ya ule mpango wa Slaa, kitu ambacho angekipinga au kukataa kama sio kupatikana kwa ile clip. Hoja ya ajira ya yule binti ni none of my business, title inaongelea Slaa.
 
Mkuu yule binti alisaidiwa ajira na UKAWA au ndio imekula kwake? Mida hii anauza nanilii ktk vioteli uchwara? Tupe mrejesho.

Alaf naomba ulitendee hilo jina lako (ID) hadhi linayostahili, nikiwa kama mdau niliyekitumia hicho kitabu cha Engineering Science, jaribu kutulia, kusoma hoja na kuchambua vizuri kabla ya kujibu mkuu. Kumbuka nimesema toka mwanzo hata kama anamapungufu gani, hauwezi kuacha kuutambua mchango wake na harakati zake kwenye medani za siasa za upinzani, lakini hawezi kutolewa kwenye orodha ya wasaliti walioatumika na chama tawala kufanikisha ajenda zao.
 
Hahaaa ume-punic mkuu. Mimi interest yangu kujua km alisaidiwa kwa lolote baada ya kufanya ushujaa na kupoteza kazi?
 
Lakini 'matapishi' yale si ndiye aliyeyaleta, au hufahamu hili?
ungetumia akili kidogo tu japo 10% ungegundua kwamba kama Dr.Slaa ndiye alimleta huyo mtu wenu basi asingeondoka. Lakini kuondoka ni kutokubaliana na kuletwa kwa huyo mtu wenu!!
 
ungetumia akili kidogo tu japo 10% ungegundua kwamba kama Dr.Slaa ndiye alimleta huyo mtu wenu basi asingeondoka. Lakini kuondoka ni kutokubaliana na kuletwa kwa huyo mtu wenu!!
Mimi ninafikiri ungetumia japo 0.5% ya akili zako ungebaini kuwa kabla ya kutokukubaliana kulikuwa na mgongano wa mitazamo. Na kwamba kuondoka kwa Dk Slaa haimaanishi kuwa hakuhusika kumleta Lowassa Chadema!
 
Umethibitisha kuwepo kwa migongano ya mitizamo na pia umethibitisha kuondoka kwa Dr. Slaa baada ya migongano hiyo. Hapa unaonesha kwamba huna akili na mpumbavu wa hoja!
 
Ungemsikiliza vizuri mchungaji Gwajima utajua ni nani aliye engineer suala la Lowassa kuja UKAWA/Chadema; shida moja kubwa ya Lowassa hua sio msemaji sana vinginevyo tungemjua Mr Richmond na hata suala la yeye kuja huku. Hata kama huwezi fikiria vizuri, unashindwa hata ku connect dots!? Kwanini Dr. Slaa alilala kwenye gari pale nyumbani kwake siku ile!?
 
Lakini 'matapishi' yale si ndiye aliyeyaleta, au hufahamu hili?
Kama ni yeye aliyemleta angeondokaje? Mnadandanywa kirahisi na hao wasaliti wenu waliotangaza ufisadi wa mtu kwa miaka 8 na kisha wanageuka kuwaambieni mtu huyo ni malaika. Walisema wana ushahidi kwa miaka 8 lakini sasa wanataka mtu mwenye ushahidi ampeleke mahakamani huyo mtu! Mnazungushwa kama pia na bado ni wafuasi wa hicho Chama! Poleni sana!
 
Ungemsikiliza vizuri mchungaji Gwajima utajua ni nani aliye engineer suala la Lowassa kuja UKAWA/Chadema; shida moja kubwa ya Lowassa hua sio msemaji sana vinginevyo tungemjua Mr Richmond na hata suala la yeye kuja huku. Hata kama huwezi fikiria vizuri, unashindwa hata ku connect dots!? Kwanini Dr. Slaa alilala kwenye gari pale nyumbani kwake siku ile!?
Ulikuwepo nyumbani kwa Dr Slaa au wewe ni Mlinzi wa Dr Slaa? Acha Stori za kwenye kijiwe cha Kahawa ndugu yangu!!
 
Umethibitisha kuwepo kwa migongano ya mitizamo na pia umethibitisha kuondoka kwa Dr. Slaa baada ya migongano hiyo. Hapa unaonesha kwamba huna akili na mpumbavu wa hoja!
Mbona una hasira mzee? Unaikumbuka hoja yako ya msingi au maisha yamekuchanganya unatukasirikia hata tusiohusika?
 
Ndugu yangu hujamtendea haki kiongozi huyu makini-Dr. Slaa, hakuwa na sababu ya kusimama na kutetea kile anachokiamini hakikuwa sahihi. Hakuwa upande wa CCM ila alisema " ukweli daima una upande".

Angalia uchaguzi wa Marekani kwa mfano; viongozi makini wa REPUBLICAN hawakusita kusimama hadharani kumpinga Rais Mteule Donald Trump. Naye amejua walikuwa na haki ya kumpinga. Na kwa sababu za ukomavu wao kisiasa, sasa wanafanya usuluhishi na maridhiano. Tatizo liko wapi? Dr. Slaa hakuamini kama Mheshimiwa Lowassa angekuwa chaguo sahihi na akaeleza maoni yake hadharani. Huo sio usaliti.
Kupinga alikuwa sawa kabisa, lakini je! hao viongozi wa Republican walompinga Trump walikimbia Marekani au kwa sasa wapo pamoja Marekani wakiwaunganisha wamerekani kwa umoja wao?
Dr. hakutakiwa kukimbia,yeye angetoa maoni yake then aendelee na kulijenga taifa akiwa hapa hapa Tanzania na sio kufanya siasa za mtandao halafu tumsifie. Mwanaume aliekomaa haikimbii familia yake eti sababu mke wake anmlengo tofauti, ni sharti ubaki umwonyeshe njia iliyo sahihi.
Dr bado tutazidi kumuuita msaliti.....kukimbia haikuwa suluhisho,alitakiwa aendelee kubaki hapa na aonyeshe ukomavu wake.
 
Back
Top Bottom