Hongera Dr. Slaa kwa kuonesha ukomavu kwenye siasa

Alimkaribisha lowassa,watu wakamuonyesha ramani ya canada kwenye atlas,akamkana lowassa..na hadithi yangu imeishia hapo
acha umburura, walimsihi masaa nane wapi mzee kasimama wima kama cha kwanza, wakamuwekea sumu, mzee kachomoa, chezea kasisi wewe!
 
Namheshimu na kutambua mchango wake kwenye siasa za upinzani Tanzania, kitendo cha kutumika na chama kilichopo madarakani dakika za mwisho na kusaliti upinzani ilinifanya nimshushe thamani sana.
Endelea kuaminishwa nawe ukaamini. Siku ukija kuelewa, too late.
 
Nani ameonyesha ukomavu wa kisiasa kama Dr. Slaa kwenye siasa za vyama vingi Tanzania ya leo?

Amejitofautisha sana na wanasiasa uchwara wa bongo. Mungu akubariki sana huko uliko na akuzidishie sana tena sana. Wewe peke yako mpaka sasa ndo umedhihiri kuwa ulikuwa mwanasiasa wa kweli uliyekuwa ukisimamia kweli na haki. Hawa uliowaacha wengi wao ni akina pangu pakavu tia mchuzi.

Wengi wao wameendekeza zaidi umimi, tumbo, fitina, majungu na chuki.

Mtaje nani unayemjua wewe aliye zaidi ya Dr. Slaa?
Mara kawa Mkweli.Lumumba mnamakengeza
 

Jiulize amaepata wapi pesa ya kununua nyumba canada?

Huko canada anaendesha maisha kwa kipato kipi?


watanzania mko wepesi sana kufikiria

Kilichotokea mwaka jana ni Kuwa;

Mbowe ametusaliti kwa sababu alikiuka misimamo yake ya siku zote

Slaa alitusaliti kwa sababu alikubali kufika bei kwa CCM na amepewa pesa ndefuuu na sasa anaishi canada

MBOWE NA SLAA WOTE NI WASALITI WA NDOTO ZA WATANZANIA

Walioumia mwaka jana ni watu kama mnyika,mdee na nasari ambao walikuwa very honest...kumbe viongozi wao kina slaa na mbowe ni wasaliti kila mtu kwa wakati wake
SLAA alichofanya nikuondoa unafiki,jaribu kufikiri kiduchu tu km luwasa aliumia baada yakufanyiwa ukatili ndan ya ccm,akakimbilia cdm kujifariji what about dr slaa aliyejenga chama kwa mda mrefu leo anafanyiwa ukatili na mbowe kwa tamaa za fedha?fikiri jomba inaumaje?
 
Endelea kuaminishwa nawe ukaamini. Siku ukija kuelewa, too late.

Kuaminishwa kitu gani? Mie nasikiliza vitu vingi, naona kisha nachambua na kupata msimamo wangu. Unakumbuka baada ya clip kuvuja alikubali kuwa na ukaribu na watu flani mahasimu wa CDM tena mbele ya TV? Hapakua tena na namna ya kujificha.

Wewe una haki ya kuamini unachotaka na mimi kadhalika nna haki ya kufikia hitimisho lolote kwa kadri nnavyouelewa upepo.
 
Back
Top Bottom