Wakuu,
Leo watoto wetu wa darasa la saba wamehitimu elimu yao ya msingi kwa kufanya mitihani ya taifa kama ilivyo kawaida chini ya NECTA inayoongozwa na katibu wake Dkt Charles Msonde.
Picha lilianza siku ya jumatatu ambapo iliripotiwa kwamba kuna watu wawili walikamatwa kwa tuhuma za kusambaza mtihani ambao ulitakiwa kufanyika siku ya jumatano na biti kali sana likatolewa dhidi ya wale wote ambao watajihusisha na vitendo vya udanganyifu
Zaidi hii ndio nimeiona ni zaidi ya mbinu za kiTISS, inasemekana kwamba mithani wa somo la kiswahili ulikuwa wa aina mbili
Yaani mkondo A ulifanya mtihani tofauti na mkondo B! Hakika hapa umekusudia kufanya na kubaini jambo fulani la udanganyifu endapo litajitokeza. Hii taarifa nimeipata baada ya kuuliza watoto kutoka shule tofauti na mikondo A na B
Lakini pia naiona NECTA ya Msonde ikijidhatiti zaidi kukomesha udanganyifu katika maswala ya mitihani kwani Msonde alienda mabali zaidi na kuanzisha kamati ya mitihani kwa ngazi ya kila wilaya na mkoa huku zikiongozwa na maafisa elimu, maafisa wa jeshi la polisi na maafisa usalama wa taifa kwa lengo la kuhakikisha usalama wa uandaaji, usambazaji na ufanyikaji wa mitahani hapa nchini katika level mbalimbali
Pia ile hali ya kuchanganya wasimamizi wa Primary na Secondary umetia fora nashauri uendelezwe ili kupunguza mazoea miongoni mwa wasimamizi kitu ambacho hupelekea kuvuja kwa mitihani.
Natumia jukwaa hili kukupongeza Dkt Charles Msonde kwa kazi yako nzuri ndani ya baraza la mitihani la taifa NECTA!