Hongera Diamond

Ukitoa maisha yake binafsi kama ya mahusiano yake na labda mpangilio wa familia yake

Diamond ni kijana anae paswa kupewa hongera na wapambanaji wote bila kujali upo katika kada au shughuli gani ya kiuchumi na kubwa ni kutokukata tamaa, juhudi,timing, kuwa na team imara NK

Hongera sana Mondi
 
Huyu mdada anamchambua dai basi tu sijui wivu sijui anashida kikojoleo cha dai
Screenshot_20181003-103234.jpg
 
Dada wa marekani kutwa kumsakama huyu dogo, kwasababu kutushawishi tuuane alishindwa na anazeeka masikini wa kutupwa anatamani hata kurudi bongo ale dona lakini ndio hivo alinyea kambi, mondi bado nakuona kwa jicho la mbali mnoo kaza baba
 
Huyu jamaa tumpongeze kwa makubwa anayofanya. Tusikosoe na kutoa kasoro kila siku. Tukiona kuna vijana wenzetu wanajituma na kufanya kazi kwa bidii tuwape moyo na kuwapongeza waendelee kufanya makubwa.

Mimi sio mbeya nayajua maisha ya Diamond nayoyaona tu mitandaoni. Kwa ninayoyaona huyu jamaa anastahili pongezi saana.

-Ni Diamond huyu kaweza kuanzisha brand kubwa ya muziki iliyotushinda kwa muda mrefu east afrika.

-Ni Diamond huyu ameweza kututhibitishia kijana anaweza kutoka Tandale akaangaliwa na Africa nzima Trace au channel O.

-Ni Diamond huyu ameweza kuajiri vijana ambao wanatoa shuhuda isingekuwa yeye wangekuwa wanauza dawa mbagala.

Amefanya makubwa saana, yanaweza yasionekane lakini siku akifariki mtayasema yote. Pongezi kwake.
 
Ni sahihi kabisa. Diamond ni maana halisi ya celebrity..kuanzia muziki wake, maisha yake na watu wanaomzunguka...Diamond ni mithili ya kiwanda....ukimwangusha yeye umeangusha mamia ya watu nyuma yake kiuchumi.... anastahili pongezi kubwa sana, na nyakati fulani vyuo vyetu vya biashara vinastahili kumpa Utambulisho fulani wa heshima.
 
Back
Top Bottom