Hongera DC Kheri James, tusaidie kutatua changamoto hizi Kibamba

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,120
7,701
Kipekee nampa Pongezi Heri James kwa kuteuliwa kuwa DC wa Wilaya ya Ubungo.

Wananchi wa Ubungo wana imani kubwa na wewe haswa kwa uzoefu ulio nao na maono uliyo nao, ulifanya kazi kubwa ulipokuwa Mwenyekiti wa UVCCM.

Wilaya ya Ubungo ni Miongoni mwa wilaya mpya katika Jiji la DSM na Makao yake Makuu yapo maeneo ya Luguruni kata ya Kibamba.

Maeneo ya Jimbo la Kibamba kwa kiasi kikubwa ndio yanashikilia wilaya hiyo mpya lakini maeneo hayo yanachangamoto kubwa ya miundombinu ya barabara.

Mtangulizi wako hakuwa na amshaamsha sana ya maendeleo na hivyo kupelekea wilaya kudorora zaidi.

Maeneo yaliyosahaulika kabisa ni Kibamba, Kiluvya Gogoni, Kiluvya Hondogo n.k, hayo maeneo yana changamoto kubwa ya barabara mbovu.

Hakuna mradi wa DMDP hata mmoja kwenye maeneo hayo shirikiana na mbunge wa Jimbo hilo la kibamba ili kwa pamoja mlete maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo.

Hongera sana Heri Jemsi.
 
Kwa kweli kwa wilaya ya Ubungo mmepata "Jembe Ulaya".

Sasa wilaya itachangamka, angalu sasa itasomeka, miradi ya maendeleo ita ongezeka haswa kwa maeneo ya pembezoni.

Kimsingi ukitaka Wilaya ya Ubungo iendelee basi hakikisha maeneo ya pembezoni kama vile kibamba, kiluvya nk yana boreshwa zaidi.
kuna maeneo tayari yana maendeleo ya kutosha kama vile sinza, Ubungo yenyewe, mbezi beach n.k.
 
"....hadi tuwatie mimba wake zenu ndio mjue tunafanya kazi"

Alisikika DC akiongea peke yake.
 
atapimwa kwa utendaji wake wa kazi ktk kipande chake.
akiweza kutatua changamoto na kuleta maendeleo ktk kipande chake basi atakuwa amejiwekea heshima kubwa sana.
rekodi nzuri ya utendaji itabaki na itamlinda ktk maisha yake yote.
 
akila kiapo aanze kazi mara moja bila kuremba, kero zina julikana, ufuatiliaji na usimamizi ndio ilikuwa tatizo,
 
Back
Top Bottom