Hongera DAR jiji kupata magari ya kuzoa taka; bado magari ya kufagia barabara sasa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,528
Kwa kweli moja ya vitu ambavyo ni kero kwenye jiji la Dar es Salaam na Manispaa zake ni hawa wafagizi wa barabara ambao kwa kweli hawafanyi kazi kwa ukamilifu kwa kuwa barabara nyingi bado ni chafu sana zikiwa zimejaa michanga na vumbi.

Hii inatokana na ukweli kwamba haiwezekani manpower ikafagia michanga kwa kilomita za kutosha eti tatizo la michanga likaisha.

Michanga kwenye barabara nyingi za Dar es Salaam imesababisha ufinyu wa barabara kwa kuwa michanga mingine imeganda pembezoni mwa barabara hivyo watumiaji wanakwepa na hatimae barabara kuwa finyu.

MAPENDEKEZO:
Ni muhimu sasa Jiji la Dar es Salaam au Manispaa hizi mpya kila mmoja wenu fikirieni kununua magari ya kufagia hizi barabara na kazi hiyo ifanyike usiku mkubwa wakati traffic ikiwa ndogo. Uchafu wa barabara Dar unakera na ni sababu ya ajali ndogondogo.

Tafuteni Road Brooms ambazo ni bei chee kuzi-operate kama hiyo pichani au toeni tenda kwa kampuni yenye uwezo wa ku-operate brooms kama hizo badala ya kuwapa kampuni ndogondogo za usafi kufagia barabara kwa mifagio ya kwa Mangi.

broce-250-3-wheel-construction-sweeper-1024x682.jpg
 
Back
Top Bottom