HONGERA CUHAS-BUGANDO: SASA VIJANA wamekubali kuwa wanafundishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HONGERA CUHAS-BUGANDO: SASA VIJANA wamekubali kuwa wanafundishwa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by CHIETH, Oct 29, 2011.

 1. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu WanaJF,

  Napenda kutumia jukwaa hii tena kuipongeza Chuo kikuu cha Udaktari Buagando Kwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye ufundishaji. Kama Miezi miwili hivi iliyopita nilitumia jukwaa hili kuiarifu jamii na wamiliki wa chuo hiki kuwa hali ya ufundaishaji hapo si nzuri licha ya karo kubwa wanayolipa wazazi.

  Baada ya post yangu hiyo nilisikia kuwa viongozi wa chuo hicho walihaha kutaka kujua ni nani aliyepost thread iliyokuwa inawaumbuwa kwa jamii. Walibaki kuwalaumu maskini wanafunzi kuwa ndiyo waliandika maneno hayo hapa JF. Wangejua kuwa mimi si mwanafunzi wa hapo ila nina interests na chuo hicho wasilaumu wanafunzi hao. Ningependa pia kuwa shauri kuwa JF ni sehemu ambapo kila mtu anaweza kutoa kero zake. Ukweli ni kwamba nilikuwa nafuatilia Mgogoro kati ya MD3 (2010/2011) na dean of faculty of medicine ndiyo maana niliamua kutoa kero hizo hapa ili wahusika na wenye interest na chuo hiki wawajibike kuwaokoa wanafunzi wale wasiharibiwe maisha na mtu mmoja.

  Ninashukuru kwamba walikuwa wasikivu na kuweza kufanya marekebisho makubwa katika ufundishaji wa "MANAGEMENT OF DISEASES". Habari nilizopata kutoka Bugando ni kwamba wanafunzi wa MD3 (2011/2012) sasa wanafundishwa mpaka wanakubali kwamba medicine sio lele mama. Na hili ndiyo wananchi tulikuwa tunataka. Haiwezekani ukalaumu wanafunzi eti hawaingii darasani wakati walimu hawaingii pia darasani kufundisha. Hivi sasa hata mtihani ukitungwa mwanafunzi akafeli atajilaumu mwenyewe na hatapata kisingizio eti si kufundishwa.

  Nilisikia sauti iliyorekodiwa ya mkutano iliyoitishwa na makamu mkuu wa chuo, katika rekodi hiyo nilisikia makamu mkuu msaidizi Taaluma ambaye pia ni profesa akiponda wanafunzi eti wasisubiri kufundishwa. Napenda kumshauri Profesa kwamba hii si sociology au open university ambapo wanafunzi wanaweza kujisomea tu na kufaulu mitihani. Medicine inahitaji mwalimu ili mtu awe daktari mzuri.

  Hata hivyo napenda kuwapongeza kwa mabadiliko makubwa mlioanza nao. Vile ville wanafunzi wanaomba pia mabadiliko haya yaende idara ya surgery na gynaecology/obstetrics.

  Tafadhali napenda kuomba uongozi wa chuo na walimu wasiwabughudhi wanafunzi kwa taarifa hizi kwa kuwa mimi si mwanafuzi ila ni mtu niko kwenye kazi zangu za kitaifa. Tunapenda kuona vijana wetu wanahitimu na kupunguza shida za watanzania waliowengi kukosa madaktari wazuri.

  Mwisho nawapongeza maaskofu kwa huduma wanaotoa kwa watanzania bila ubaguzi wa kidini,rangi na ukabila. Kwa pamoja tutaweza

  Nawasilisha.
   
 2. l

  laun Senior Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ni mwanafunzi tena shujaa
  The site iz secure dont worry.
  Kwa jinsi ulivyoandika hatumuhitaji federal agent wa fbi kugundua kuwa wewe ni mwanafunzi hapo . Nakupongeza kwa kufichua ubovu kiasi cha kuleta mabadiliko,tunawahitaji wengi kama nyie ili kuokoa elimu yetu, piga kitabu mdogo wangu
   
 3. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Hayo matatizo haliyoeleza hapo ndugu mtoa thread hayapo tu bugando bali hivi vyuo vyetu vya serikali ndio yamezoeleka na kwa bahati mbaya hakuna sehemu ya kutoa malalamiko na kusikilizwa,tena wakikuona unajidai unajuajua utapigwa supplementary zinazo approach ku-disco kwahiyo wanafunzi wanayanyamazia tu mapungufu ya vyuo vyao.Mf chuo kikuu kimoja hapa dsm anakuja lecturer kwenye theatre ila hana mike na hata kama anayo basi speaker zinakua hazitoi mawimbi ya sauti ipasavyo,kinachofanyika ni wanafunzi kulala mwanzo mpaka mwisho.
   
 4. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Hongera bugando.
   
 5. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Bugando kwa uwajibikaji.
   
 6. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuthibitisha kama mimi ni mwanafunzi. Bugando inamchanganyiko mkubwa wa watu na wanafahamu kila kitu kinachoendelea hapo. Sasa kusema mimi ni mwanafunzi unawatafutia hao wanafunzi bif na walimu wao. Hata hivo nimependa your comments na inanitia moyo kuwa watu wanapata taarifa kupitia JF.
   
Loading...