Hongera CUF - Chama Cha Wananchi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera CUF - Chama Cha Wananchi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 27, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Napenda kutoa hongera za dhati kwa Chama Cha CUF - Chama Cha Wananchi mimi ikiwa ni mmoja wapo wa hao wananchi ,kwa kufanya uchaguzi na kuumaliza kwa busara kabisa ,tunajua anaeshindwa haachi kulalamika hata Maximo nae hulalamikia wachezaji wake.

  Napenda nichambue hoja za msingi za baadhi ya watu ambao wana msimamo tofauti na kwamba matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa CUF hayaridhishi japo wanashindwa kuweka wazi ni wapi hayaridhishi.

  Hoja ya kubadili viongozi:

  Kila pahali panapotakiwa kuongozwa hua kuna utaratibu wa kuchagua viongozi na utaratibu wa cuf ni kama wote tulivyoona tangu mwanzo mpaka hapa tulipo,kama kulikua na haja ya kubadili uongozi ni kwa kura kupitia wajumbe sio vyenginevyo hivyo kama matokeo hayaridhishi ni hawa wachache hawakuridhika sio wananchi wote!

  Hoja ya kutokua na imani:

  Wengi kati ya wanaotoa maoni yao huja na hoja ya kutaka vijana waongoze, jamani hii dunia ya leo kama kila kitu twataka chende kwa mabavu ya vijana bila busara za wazee na hikima hatutafika pahali, hili lazima tulijue!!
  kweli twahitaji nguvu mpya lakini mtumzima dawa na hawa ni wazoefu wa mikiki na dhoruba na mpaka sasa ni wachache wanaolalamika kuhusu ungozi wao mi nadhani tungewapa sapoti ya kweli ili tujivue katika janga tulonalo. viongozi wa juu wa CUF ni wenye uwezo mkubwa tu na wenye hamu ya kuleta maendeleo ya kweli katika nchi yetu na wanaokubalika kote Tanzania na kimataifa, ukiona jinsi wananchi wanavyo wapokea vizuri wanapokua katika ziara zao kote nchini ndio utaamini kweli wananchi wanaimani kubwa na hawa viongozi, tizama mikutano, sikiliza hutuba zao jinsi zinavyowagusa mojakwamoja wananchi halafu useme hawana imani nao si ukweli hata kidogo ni kutaka kupandikiza chuki na kukivuruga Chama halafu wakae pembeni wachekelee.

  Hoja ya kutofika popote;

  Kwa asietaka kuona haoni japo sote twatambua kama CUF ndio tegemeo la mabadiliko Zanzibar na Tanganyika kwa ujumla na ndio chama pekee kilichoweza kutoa upinzani wa kweli na hata kuifanya ccm iweze kubadili baadhi ya sera zeke na uonevu wa waziwazi unaoendelea, kwa miaka 16 CUF imepiga hatua kubwa na sasa MTanzania anaweza kutoa maoni na hata kuikosoa serekali kupitia chama!kuweza kua na wabunge na wawakilishi wanaotoa upinzani katika serekali zote mbili hii pia ni hatua na sasa tunaona baadhi ya mambo yanayoendelea ndani ya baraza la wawakilishi na Bunge ni juhudi za CUF kuitetea Zanzibar na Tanganyika mpaka kuwafanya wawakilishi na Wabunge wa CCM kujua kwamba hichi ni chetu na tukisemee hii pia ni hatua!

  Hoja ya kupigiwa kura:

  Hoja hii ni ya msingi sana kwani tangu mwaka 2000 CUF wamekua wakipata kura kutoka kwa wanachama wa vyama vyengine mpaka kutoka katika chama tawala! mimi kama mwananchi niliepiga kura 2000 na 2005 najua ya kwamba CUF inakubalika na wananchi walio wengi na wanapata kura hata kwa wana CCM tatizo ni jinsi ya kuzilinda!
  Mimi napenda tujitahidi kuisapoti CUF kama chama Kikuu cha Upinzani na kilicho na hamu kubwa ya kubadili hali ya nchi yetu kiuchumi na kimaendeleo, nimuda wa kukaa pamoja kujadili nini cha kufanya kuisaidia CUF kushika uongozi nasio kukilalamikia kwa kurudisha viongozi wake katika kukiongoza chama.
  Mapambano yanaendelea.
   
  Last edited: Feb 27, 2009
 2. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CUF imepoteza mvuto kwa watanzania , na haswa kutokana na viongozi wake kukaa kwenye muafaka miaka 2 na hawakuwajulisha watanzania wanajadili nini na baada ya hapo hawana majibu ya kuridhisha kuwa nini kinaendelea, inaonekana hata wakiugwa mkono kama walivyougwa Pemba hawawezi kulinda ushindi wao, wanaweza kunyanganywa kirahisi na wakakaa kimya.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Usitegemee kama Lipumba au Seifu watalinda ushindi hilo halipo wala hawatakuwa mstari wa mbele katika jambo hilo ,kura na ushindi vinalindwa na wananchi wenyewe ambao ndio wanaoamua nani awaongoze ,kuhusu muafaka ni njia moja ya kuleta maelewano na kinachofanya kuwa au kiwe siri ni kuepuka kutokueleweka ,na nafikiri maafikiano yalikuwa yakirudishwa kwenye vikao vya chama husika na huko wajumbe wakiyazungumza na kuyachambua na kuyarudisha kwenye mazungumzo.Sio mambo au kila kitu huwa kinatangwazwa ndugu hakuna mechi ya mpira katika siasa.
   
 4. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka una kazi.....

  CUF ni chama cha wananchi wa nchi ipi? Zanzibar? Unguja? Pemba? Tanganyika? ama Tanzania...nifafanulie tafadhalin kaka?

  Just constructive critique....

  Omarilyas
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwani kipo nchi gani ?
  Kwa nijuavyo mimi kuwa CUF inapatikana kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  United Republic of Tanzania. United Tanganyika - the part on the African continent and islands of Zanzibar.
  Tanzania means Tan(ganyika) + Zan(zibar) + ia
  [​IMG]
   
 6. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Mwiba;

  Mwiba; hakika hiyo ramani yako imenivutia sana, na pia kwa kweli inaonesha ni jinsi gani ulivyo makini katika kufuatilia mipaka ya nchi yetu,

  Mwiba; Siku zote nimekuwa nikikueleza kuwa kwa kuwa CUF kwa sasa imeainishwa kama chama cha kidini na kufanya watanzania Bara kutoafikiana na chama hiki sasa si wakati Muafaka kuangalia mtizamo mwingine?

  Mwiba;utakubali kuwa CUF baada tu ya kuwa namshiko kule visiwani CCM kwa nguvu zao walijitahidi kukididimiza na hata kukivika uhusika wa dini na mpaka sasa ndivyo walio wengi wanavyokitambua chama hiki chenye nguvu huko visiwani.

  Mwiba; sasa ni ni ni hatima ya chama hiki ambacho kila kukicha Lipumba ndiye Mwenyekiti?

  Unakumbuka ule uchaguzi wa Tarime Jinsi Lipumba alivyokuwa akifyatuka na maneno utazani ni CCM?

  Huyu Lipumba ameshapoteza dira hata hivyo chama hiki nacho mkinaanza kupoteza mwelekeo,

  Mwiba; Mtu anaweza kuwa mtumwa wa fikra lakini si mtumwa wa ........, naomba utie akili Mkubwa wangu, hii Tanzania ni yetu sote kama tutamuenzi mtu kwa kumtunuku uenyekiti wa Maisha si mbaya sana.

  Mwiba; kwa ushauri wangu nenda na wewe kagombee chochote humu ndani ya chama hicho, lakini sasa usikose kuwa ...... na hiii ni hatari sana kama tukiishi kwa misingi ya Di.... hiii itatutoa roho.

  Mwiba; Kweli hii ndiyo unayoiita demokrasia? ama kiini macho?

  Mwiba;Muda umefika tumuambie Prof kuwa arudi vioni akielimishe ndugu zetu aaache kupoteza muda kule kwenye siasa.
   
 7. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  KIRANJA!!!

  Kazi ya kulinda kura/ushindi ni ya kila mmoja wetu, viongozi kazi yao ni kuratibu,kupangilia na kutuelekeza nini cha kufanya kuelekea ktk maendeleo ya kweli kisiasa,uchumi,sayansi, michezo n.k.

  Hayo yote yatapatikana km tutaitumia vzr haki yetu ya kupiga kura, kuilinda kura yako na mwisho kusimamia ushindi wa kura yako. Ukikubali kurudi nyumbani kucheza pool ujue hujajua bado thamani ya kura yako; so usitegemee aje Lipumba akulindie kura yako isiibiwe.

  HONGERA CUF
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,217
  Trophy Points: 280
  Baada ya CUF kujengewa taswira mbaya ya udini huku bara ilikuwa ni busara kubadili safu ya uongozi ili kujenga taswira mpya ya chama cha kitaifa cha upinzani.

  Uchaguzi umekwisha, wale wote wenye mapenzi mema na CUF, hawanabudi kuwaunga mkono viongozi waliochaguliwa kwa hiyo demokrasia ya CUF.

  Ushauri, bara msimsimamishe tena Lipumba, nyimbo yake haiwezi kukesha ngoma. Na Zanzibar msimsimamishe tena Maalim, japo atashinda, kamwe hatakabidhiwa nchi, mtapokwa tena na kuishia kulia.

  Hivi kweli hamuuoni uwezo wa Juma Duni ama Hamad Rashid?. Yeyote kati yao akishinda, mnakabidhiwa nchi, sio Maalim.
   
 9. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Pasco;

  Pasco;hapo mkuu sijakusoma ina maana umeongea na state? ama kutabili tu?
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,217
  Trophy Points: 280
  Haya sio mambo ya utabiri, ni personal opinion.
  Kwa siasa za Zanzibar, mara zote CUF wanashinda lakini walipokwa ushindi, sababu za kupokwa zipo na kama atasimama tena Maalim, atashinda tena na watapokwa tena kwa sababu zile zile.

  Wanaocheza mchezo huo mchafu wa kupoka ushindi wa CUF sio CCM, its above the party lines. CUF wanajua, CCM wanajua na wafuatiliaji siasa za ZnZ wanajua.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM mtapiga makelele lakini mkae mkijua huu ndio mwaka wenu wa kuitawala Tanzania ,hatamu zinavuliwa na mnawekwa pembeni ,kusubiri kujibu nani na nani aliuza nchi ? Kila mmoja wenu aandae utetezi na ajue nani alimtuma kufanya ubadhirifu ,ole wako kama huna ushahidi ,Wananchi hawatakubali ubaki kwenye magolofa lazima utelemke shamba mkakamate jembe pamoja ila nyie mtaenda kutafuta zaabu pale Maweni Muheza ,lazima mpasue mwamba ili mludishe zaabu yetu atukubali.

  Kama mlikuwa hamna habari sasa nawapasulia wazi kabisa ,mgombea Uraisi kwa ticketi ya vyama vya upinzani ni Lipumba Mtanzania mwenye uchungu na Nchi yake ,sidhani kama wengi wenu mmeanza kuliona hilo ,ila ndio ameshaelekea katika kujiandaa tena kwa safari ya tatu ,kama mtaangalia mmesikia tetesi za viongozi wengine wakuu wa vyama vya upinzani kurudi au kujipanga kwenye viti vya ubunge ,viongozi wakuu wote isipokuwa Lipumba , hilo ni azimio la pamoja lililofikiwa katika vikao maalum vya kijitu kizima na washauri mbalimbali wa mambo ya siasa ,hapa bakini kupiga domo ,hivi mnaamini kama CUF haikupata kiti hata kimoja cha Ubunge hapa Tanganyika ? Mtu mwenye akili timamu hawezi kulikubali jambo hilo hata kidogo lazima ataguna tu na kukuona mambo yaliopita huyafahamu. Viongozi wenu wakuu wanajua fika kuwa Lipuma alishinda uchaguzi Mkuu uliopita ,jambo ambalo ni siri kubwa iliyokuwa imefichwa hapa Tanzania na wabunge wengi wa CUF walikuwa ni washindi kwa maana hiyo CUF ni Chama pekee ambacho kama matokeo yangetangazwa kwa haki basi CUF ingekuwa na viti vingi ndani ya bunge ,sipendi ubishi au kubishana kwani haitasaidia kitu ,zaidi ninalolitaka ni ukweli wa kukubalika yaliojiri ili kuifanya CUF isipate hata kiti kimoja ,mtu hata awe kichwa mchungu anaweza kujiuliza inakuwaje unatokea mshindi wa pili wa Uraisi na kukosa kiti hata kimoja hapa Tanganyika ?
  Sidhani kama hapa JF ni mambumbumbu wa kushindwa kuuelewa ukweli ,tunachotakiwa kufanya si kuchukiana wakati sote tupo katika kambi moja ni lazima ukweli tuukubali ili tuzidi kusogea mbele ,na wakubwa watu wazima wameliona hilo na kulitolea saluti au kulikubali kuwa CUF ni Chama nambari one Cha upinzani ,CUF ikiunganisha kura zake za Zanzibar na kuunganisha kura za Upinzani hapa Tanganyika basi CCM itawachwa mbali sana ,wakubwa wa vyama vya upinzani wamelitafakari na kuliona hilo ,hivyo panapoharibika hapana budi kutengenezwa kwa nia safi ikiwa lengo ni moja tu la kumkomboa Mtanzania na utawala wa CCM uliodumu kwa muda wa miaka 47 ambao umeshindwa kumfikishia maji taa pakulala bora Mtanzania wa hali ya chini.

  Mimi nawashangaa wale ambao wanakuwa mstari wa mbele kuona CUF ni Chama cha kidini sijui terorist ,yaani mambo kibao ambayo yote imeshabebeshwa na bado haijatetereka.Lakini pia sioni ajabu kwani wanalinda ,wanalinda maslahi ya CCM ,wanaipa nguvu CCM na baadhi ambao wamo ndani ya upinzani wamevaa ngozi ya kondoo wakipita wakihubiri mambo mema kumbe ni wasaliti.

  CUF itabeba bendera ya wananchi kutoka vyama mbali mbali vya upinzani na kuipeperusha Tanzania nzima wakiwataka wananchi wawaunge mkono kwani umoja wa na wakuu wa vyama hivyo tayari wameshaipa CUF go ahead ,kinachosubiriwa ni kutangazwa rasmi ili kuwataka wananchi na wapenzi pamoja na wanachama na watanzania kwa ujumla kuiangusha CCM kwa kishindo.

  Hivyo kwa wale ambao wanataka kuona utawala wa CCM ukifikia mwisho na wao wapo hai basi ni lazima waungane na WaTanzania wenzao kumuunga mkono Lipumba mtu ambae WaTanzania wanayo kila sababu ya kujivunia.
   
 12. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kwani bado Seif anaota siku moja atakuwa raisi Visiwani?
   
 13. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  SIo Seifu wala sio wewe jambo la kuwa au kuutwaa Uraisi WaZanzibari wanamuachia Mwenyezi Mungu na wewe kama ni muumini wa dini unajua vizuri sana juu ya msemo huo ila kama ni mfuasi wa Chama Cha Maswaibu ,utajikatia shauri kivyako vyako.
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,217
  Trophy Points: 280
  No, haoti, yaani sio ndoto, bali yeye na wanacuf wanaamini alizaliwa ili awe rais sultan wa Zenj.

  Pia wanaamini Lipumba ndio wa bara.

  Wanaamini chama cha upinzani ni kimoja tuu, CUF.
   
Loading...