Hongera CHADEMA kwa Utetezi

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Wasalaam!

Kwanza nianze kuwashukuru wanachadema na kamandawa anga kwa kupigania yafuatayo;
1.Kamanda wa anga na chama imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha haki za wabadhirifu (majipu),wavunja sheria nk na amekemea serikali kanisani hii imekaa poa sana kwani kundi hili lilikosa mtetezi ambapo wananchi wanatamani wanyongwe,lakini kwa ujasiri wa mbowe na wafia chadema hakika wamepata watetezi hivyo "wananchi" tulieni.
2.Kamanda wa anga na chadema mmetete kundi la wanywa pombe,wacheza pool mida ya kazi na hata pale Raisi alipoamuru wakuu wa mikoa kutumia mamlaka yao kuwaweka ndani Kamanda umewakingia kifua hasa ikizingatiwa kwamba hawa ni wapiga kura.
3.Kamanda pia "nimefurahi" kuona baadhi ya vijana wa bavicha na wazee wameanzisha mada na majadiliano kupinga uhakiki na ukamataji wa silaha nimefurahi kamanda kwani Makonda anatatutafuta sisi tuliounga mkono "upinzani".

4.Kamanda wa anga tupiganie na sisi kwa maana ajira zipo matatani,mizigo yetu inakamatwa na wengi wapo ndani bila dhamana,kamanda wa anga hakika ukitutetea kwa kukemea serikali kura zetu ni zako....tunakuenda kamanda wa anga,tunataka kesho jumapili ututetee kwa sauti ili maaskofu wajue jinsi sisi "wafanyabiashara" tunaounga mkono chadema na harakati zake tunavyonyanyaswa.

Hongera kamanda wa anga na wanachadema wote kwa "kujielewa"..!..nina uhakika makamanda wa kurugenzi watachukulia pongezi hizi na malalamiko haya kwa umakini mkubwa!
 
Kwa anayoyafanya...lazima hili kundi la wauza sembe lipate utetezi mzito,hamna kurudi nyuma.
 
Sasa kama mgombea urais wao ni fisadi wewe unategemea nini kutoka kwa kamanda wa anga?
 
Sasa kama mgombea urais wao ni fisadi wewe unategemea nini kutoka kwa kamanda wa anga?
Mkuu hata sisi tunahitaji utetezi,tena siku hizi toka Lowasa aje nimefurahi serikali inashitakiwa ndani ya ibada...naomba atutetee la sivyo "ajira" zipo matatani.
 
Sasa kama mgombea urais wao ni fisadi wewe unategemea nini kutoka kwa kamanda wa anga?
Kama unaaamini Lowasa ni fisadi basi ni kamwanafunzi ambacho kimetoka shule na hakijapata experience. Je ccm si zaidi maana ni mwalimu aliyemfundisha Lowasa. Ukitaka kuamini Lowasa ni mdogo sana katika kamata kamata ya Magu, hajamfikia Lowasa. Maana yake nn yako Marofesori ya rushwa za kutisha.
 
Back
Top Bottom