Hongera chadema kwa kuwaletea watanzania katiba mpya

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Juzi Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji(rtd)Joseph Sinde Warioba alitangaza uzinduzi wa Rasimu ya Katiba mpya kwa mbwembwe nyingi na hakika imepokelewa kwa mikono 2 na Watanzania wote. Kuna mambo mengi yameainishwa kwenye Rasmu hiyo yanayotakiwa kwenda kujadiliwa kwenye Mabaraza ya Wilaya,Kata na Taasisi mbalimbali zenye shughuli zinazofanana.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba mchakato huu wa kupata Katiba Mpya ya Tanzania ambayo tuna hakika inaenda kutuletea serikali 3 kama ilivyoainishwa kwenye Rasimu ni USHINGI MKUBWA SANA KWA CHADEMA. Huu ni ukweli mabao hauwezi kupingwa kwani CHADEMA ndiyo WAANZILISHI wa mchakato huu wa kutaka Tanzania iwe na Katiba mpya baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Katika Uchaguzi wa 2010 CHADEMA walionekana kuwa washindani wakubwa wa CCM na inasemekana kuwa isingelikuwa NEC(Tume ya Uchaguzi),Usalama wa Taifa-UWT na Polisi kuingilia na kuchakachua MATOKEO ya Uchaguzi huo CCM wasingelioona Ikulu. Matokeo yalianza kuashiria mapema kabisa kuwa CHADEMA walikuwa wakipata kura za kishindo kwenye maeneo muhimu ambayo zilikuwa ngome za CCM. Hapo ilibidi kucheza rafu ili kuinusuru CCM. Kitendo ambacho kiliifanya CHADEMA kutokubaliana na MATOKEO na hivo kupelekea madai ya kutaka matokeo yasitangazwe kwa vile Uchaguzi haukuwa wa Huru na Haki.Hapo ndipo yalipoanzia madai ya CHADEMA ya kutaka kuwa na TUMAE HURU YA UCHAGUZI na kutaka MATOKEO YA URAIS KUHOJIWA MAHAKAMANI mambao ambayo tayari yamezingatiwa kwenye RASIMU HII!

Yes, M4C imezaa matunda ya kuwapatia Watanzania Katiba Mpya lakini pia kurudisha Serikali ya TANGANYIKA ambayo ilikuwa imemezwa na Muungano tangu mwaka 1964. Huu ni ushindi kwa CHADEMA. Hongereni sana na Mungu awabariki huku tukiomba ya kwamba Mungu atuweke hai ili mwaka 2015 itakapofika Serikali ya TANGANYIKA chini ya Katiba mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Hii ndiyo itakuwa ZAWADI ya WATANGANYIka KWA CHADEMA kwa kurudisha hadhi ya Taifa lao lilllokuwa limepotea na kumezwa na Muungano wa Tanzania.

Big up CHADEMA.
 
Mweee CDM ndio mkombozi pekee. CUF ni maliberali full kulana migongo.
Wengine ndio washa jifia kama Chama cha Zamani kilivyofia Lumumba alipo fariki Patrice Lumumba
 
Anaye kubali akubali anaye kataa eendelee kukata, CDM kinapendwa ndio tumaini pekee la watanzania walio wengi kwa sasa, ccm mmepoteza mvuto kwa wananchi, bila CDM kuweka kwenye ilani yao ya 2010, ccm mgeendelea na ile ile katiba ya kulinda maslahi yenu badala ya maslahi ya Taifa
 
CDM ni mkombozi wa Watanzania wote....Ahsante CDM kwa kutupatia Tanganyika yetu hadhi yake..
 
Mkuu , kwanza nikupongeze kwa kutambua kwamba CDM ndiyo iliyoleta HUU MCHAKATO WA KATIBA , na ningependa pia kukuhakikishia kwamba haya mapungufu ya hapa na pale na hasa kuhusu MUUNDO WA TUME HURU YA UCHAGUZI ,tutayashughulikia kwa umakini mno ,bila shaka unafahamu kwamba bila ile tume mbovu ya akina KIRAVU , Peter Serukamba au Makongoro Mahanga wasingekuwa bungeni leo hii na wala lile TUSI zito la Serukamba lisingeingia kwenye HANSARD .
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom