Hongera CHADEMA kushinda kata ya Ipole (Sikonge)


F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
15,185
Points
2,000
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
15,185 2,000
Wakuu,

inatakiwa niseme ukweli maana nikiwa mzaliwa wa kijiji hiki nimefurahishwa sana na ushindi wa CDM kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Kata ya Ipole ikuwa ngome kuu ya CCM katika jimbo la Sikonge ikifuatiwa na CUF tangu mwaka 1995 na ccm imelishika jimbo hili tangu uhuru.
2. Hakukuwa na Tawi lolote la CDM katika kata hii hadi April 2012 ambalo lilikuwa rasmi
3. Katika uchaguzi mkuu uliopita CDM haikusimamisha mgombea wa udiwani na hata mgombe wa Urais upitia CDM (Dr Slaa)
alifahamika na watu wachache sana kwenye kata hii.
4. CDM imefahamika sasa na vijana wengi bado wanazijadili sera za CDM kulinganisha na CCM ambazo hazitekelezeki - CDM imeacha gumzo na hata baadhi ya wazee wameshabadilisha misimamao yao


Kwa nini CCM wameshindwa:

CCM wameshindwa kwa sababu kuu moja tu wamewasahau vijana wa kata hii ambao wengi wanaishi maisha magumu sana, Mbunge wa Jimbo hili hajawahi kufanya mikutano na vijana na hana mikakati yoyote iliyo wazi ya kuwakomboa kutokana na wimbi la umaskini. na hii ndiyo weak point ya kufanya M4C ipenyeze.

Sasa hiyo ndiyo ilikuwa adhabu kwa CCM - na adhabu hii ndiyo itakayofanyika na kwingine kote katika jimbo hili: - Ni vigumu mno mno mnyamwezi kukubali mabadiliko sasa ikifikia hatua hiyo basi think twice:

Ombi kwa CDM:

CDM imedhihirisha kwamba Tabora si tena Ngome kuu ya CCM na kwa kutumia Diwani ambaye ni kijana (Motivated) basi mnaweza kuanza kujijenga mkitumia IPOLE kama ngome kuu. Hongera sana wapiganaji wetu na hongera kwa CDM taifa kufika hadi kwetu maana sasa tunajiona ni sehemu ya M4C.

Nawapongeza sana makamanda, ingawa mlishuhudia maisha duni ya wananchi waliokata tamaa hasa vijana na kina mama, miundombinu duni; huduma za afya, barabara; maji ni balaa tupu; ni hapo hapo kijijini IPOLE ambapo alizaliwa mpiganaji mwingine KasangaTumbo Christopher (RIP)kwa wale mnaokumbuka historia.
 
paul nsangu

paul nsangu

Senior Member
Joined
Nov 23, 2012
Messages
178
Points
0
Age
43
paul nsangu

paul nsangu

Senior Member
Joined Nov 23, 2012
178 0
vizuri wana sikonge muda wa kuwabwaga magamba umefika. bado kata ya makonde ludewa.
 
C

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
3,605
Points
0
C

Concrete

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
3,605 0
Kuindoa CCM madarakani ni kazi rahisi sana kama kila mtu anayeipenda CHADEMA atahakikisha mambo yafuatayo yanafanyika.

1/MKUTANO Kila kitongoji(Kijiji/Mtaa)

2/SHINA Kila kitongoji

3/BENDERA Kila kitongoji

4/TAWI Kila kata

5/MGOMBEA BORA Kila uchaguzi

6/KAMPENI Kila uchaguzi

7/WAKALA Kila kituo.

8/MWANACHAMA kila nyumba

9/HOJA BORA kila mjadala.

10/ELIMU YA URAIA kwa kila mtu.

11/TAWI IMARA kila chuo

12/OFISI BORA kila mkoa
 
Mwita Maranya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2008
Messages
10,569
Points
1,250
Mwita Maranya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2008
10,569 1,250
I wish kila kijiji na kila kitongoji kielewe mchawi mkuu wa nchi hii anayetuwangia mchana na usiku ni ccm! Period!
Hiyo inawezekana ikiwa wale wote tuliona ufahamu huo tukitumia nafasi zetu kuwafahamisha na kuwaelimisha ndugu zetu ambao tunadhani kwamba bado wako katika lindi la usingizi wa ccm.

Wakishautambua ukweli na kuchukua hatua ni dhahiri kwamba mchawi wetu atakuwa amedakwa mchana kweupe na kuuawa kwa maslahi ya wananchi wote.
 
cacico

cacico

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
8,389
Points
1,250
cacico

cacico

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
8,389 1,250
hiyo inawezekana ikiwa wale wote tuliona ufahamu huo tukitumia nafasi zetu kuwafahamisha na kuwaelimisha ndugu zetu ambao tunadhani kwamba bado wako katika lindi la usingizi wa ccm.

Wakishautambua ukweli na kuchukua hatua ni dhahiri kwamba mchawi wetu atakuwa amedakwa mchana kweupe na kuuawa kwa maslahi ya wananchi wote.
amen my dear! Amen! Lol!
 
M

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2010
Messages
2,511
Points
0
M

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2010
2,511 0
wakuu,

inatakiwa niseme ukweli maana nikiwa mzaliwa wa kijiji hiki nimefurahishwa sana na ushindi wa cdm kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Kata ya ipole ikuwa ngome kuu ya ccm katika jimbo la sikonge ikifuatiwa na cuf tangu mwaka 1995 na ccm imelishika jimbo hili tangu uhuru.
2. Hakukuwa na tawi lolote la cdm katika kata hii hadi april 2012 ambalo lilikuwa rasmi
3. Katika uchaguzi mkuu uliopita cdm haikusimamisha mgombea wa udiwani na hata mgombe wa urais upitia cdm (dr slaa)
alifahamika na watu wachache sana kwenye kata hii.
4. Cdm imefahamika sasa na vijana wengi bado wanazijadili sera za cdm kulinganisha na ccm ambazo hazitekelezeki - cdm imeacha gumzo na hata baadhi ya wazee wameshabadilisha misimamao yao


kwa nini ccm wameshindwa:

Ccm wameshindwa kwa sababu kuu moja tu wamewasahau vijana wa kata hii ambao wengi wanaishi maisha magumu sana, mbunge wa jimbo hili hajawahi kufanya mikutano na vijana na hana mikakati yoyote iliyo wazi ya kuwakomboa kutokana na wimbi la umaskini. Na hii ndiyo weak point ya kufanya m4c ipenyeze.

Sasa hiyo ndiyo ilikuwa adhabu kwa ccm - na adhabu hii ndiyo itakayofanyika na kwingine kote katika jimbo hili: - ni vigumu mno mno mnyamwezi kukubali mabadiliko sasa ikifikia hatua hiyo basi think twice:

ombi kwa cdm:

Cdm imedhihirisha kwamba tabora si tena ngome kuu ya ccm na kwa kutumia diwani ambaye ni kijana (motivated) basi mnaweza kuanza kujijenga mkitumia ipole kama ngome kuu. Hongera sana wapiganaji wetu na hongera kwa cdm taifa kufika hadi kwetu maana sasa tunajiona ni sehemu ya m4c.

Nawapongeza sana makamanda, ingawa mlishuhudia maisha duni ya wananchi waliokata tamaa hasa vijana na kina mama, miundombinu duni; huduma za afya, barabara; maji ni balaa tupu; ni hapo hapo kijijini ipole ambapo alizaliwa mpiganaji mwingine kasangatumbo christopher (rip)kwa wale mnaokumbuka historia.
zomea zomea za wananchi ni kwamba wameichoka sisim-magamba!!! Tatizo tu ni kwamba bado wananchi wengi wa vijijini hawajapata elimu ya uraia haswaaaa ndo maana bado wamevaa magamba ...wanasahau kwamba magamba hufanya sura ya kitu ionekane hovyo!
 
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2008
Messages
11,549
Points
2,000
Sikonge

Sikonge

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2008
11,549 2,000
Taratibu taratibu hadi somo litaeleweka. Sisi Wanyamwezi tumeshatukanwa sana hapa JF na kwenye FB na mtukani mkubwa ni Majjid Mjengwa ambaye hutumia UHEHE wake kutupa za usoni haswa haswa.

Huwezi kumkatalia moyoni ingawa kwenye mitandao tutakuwa tunamshambulia ila ukweli tunauona. Sisi tumekuwa chambio la CCM kwa miaka kibao na kibaya zaidi, wakishida, wanaondoka na kutusahau. Ila sisi na ujinga wetu tukiwaona tena wakija na kutupa Khanga, Tshirt, kofia, vyakula nk basi tunafungua tena miguu na wanatutenda.

Ipole wameonyesha kuwa kutendwa sasa basi. Walau tujaribu na wengine na siyo kila siku huyu huyo mmoja na mambo hayaendi. Hongera sana Bandugu wa Ipole kwa kuanzisha moto na milele mtakumbukwa kuwa mlionyesha njia kwa mkoa wa Tabora. Tunaomba tu M4C irudi Tabora na kutembelea kata zote kama walivyofanya Morogoro.

Wanyamwezi ukiwaamsha, hadi utafurahia jinsi watakavyoichukia CCM. Muda wa mabadiliko na kuipa CCM likizo umefika.
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
15,185
Points
2,000
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
15,185 2,000
zomea zomea za wananchi ni kwamba wameichoka sisim-magamba!!! Tatizo tu ni kwamba bado wananchi wengi wa vijijini hawajapata elimu ya uraia haswaaaa ndo maana bado wamevaa magamba ...wanasahau kwamba magamba hufanya sura ya kitu ionekane hovyo!
ni kweli elimu ya uraia bado ngumu hasa kwa kina mama na wasichana, ila kwa wavulana hilo nakubishia.

Vijiji vingi sasa vina TV's na wanafuatilia sana vikao vya bunge, nilifika ipole Pasaka nikawa pale kwa wiki mbili hivi, niliona vijana wanajadili sera za CDM wakilinganisha na za CCM ambazo hapo hapo walisema za UONGO Mtupu, pia walianza kuhoji hata wajibu wa mbunge wao anafanya nini miaka yote akiwa mbunge wa jimbo hili. Walitaka pia kujua msimamo wangu wa kiitikadi --(as reference) nilipowaambia CCM alikuwepo ila kwa sasa haipo na waifute katika mawazo yao.... vijana wote wapo walilipuka kwa furaha, nafikiri kama ningewaambia mimi ni kada mzoefu wa MAGAMBA, baada ya likizo yangu ingeharibika.

Sikufuatilia mikakati ya CDM lakini nilishangaa na sikuamini kata kuhamia CDM, Najua ukimuuliza NAPE atakwambia IPOLE ndiyo nini? sawa lakini bandubandu hadi 2015 tunamaliza gogo. Bravo wapiganaji hasa Mwenyekiti na Katibu wa CDM wilaya ya Sikonge -- Kazi nzuri.
 

Forum statistics

Threads 1,285,942
Members 494,834
Posts 30,879,987
Top