Hongera CCM/TFF kwa kuileta Brazili na siasa za wasiodanganyika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera CCM/TFF kwa kuileta Brazili na siasa za wasiodanganyika!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 3, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Tanzania Daima (Jumatano)

  UNAWEZA kushangaa kwanini nawapa hongera CCM badala ya Shirikisho la Soka nchini kwa hatimaye kuleta timu bora zaidi ya soka duniani, yaani ya Brazil.

  Nikiwa mdau wa mambo mengi ikiwamo soka nimejikuta siku chache zilizopita nikirukaruka na magwanda yangu ya rangi ya taifa na bendera mkononi kufurahia kwa shangwe kuwa hatimaye serikali ya CCM kupitia wadau wake mbalimbali imefanya mojawapo ya vitu ambavyo ni vizuri zaidi kutupa wananchi burudani.

  Tangu Rais Kikwete aingie madarakani amejitahidi sana ‘kuinua' soka – msiniulize kama inainuka au mifumo ya watu ndiyo inainuka zaidi na kwa kila kipimo ameendeleza jadi ya kuweka mambo ya mpira mbele na kutuhakikishia wananchi kuwa tunakuwa na burudani ya kudumu. Kwa hili anastahili pongezi kama vile Mkapa anavyostahili pongezi kutujengea uwanja wa kimataifa wa soka pembeni kidogo ya mojawapo ya hospitali mbovu zaidi kwa kina mama wetu kujifungulia ya Temeke! CCM idumu.

  Nilitaka niandike makala ya kukosoa lakini nilijikuta nashindwa hasa baada ya kujua kuwa Watanzania ni watu wanaopenda burudani na kujirusha, yawezekana kuliko taifa jingine lolote duniani.

  Sasa ningeandika makala ya kukosoa nina uhakika kuna baadhi ya watu wangekasirika na kudai kuwa "Mwanakijiji anapenda kulalamika sana". Hivyo nimeamua kuandika makala hii kuunga mkono ‘juhudi za serikali' kuwaburudisha wananchi na kuwafanya wasahau mambo ya msingi na muhimu yenye kugusa maisha yao.

  Baada ya kuwatimua mbayuwayu waliotaka kuwa tetere kwa maelezo kuwa nchi yetu ni ‘maskini' sana, genius wetu wa kibongo wakaamua kutufafanulia umaskini wetu kwa mambo mengine na ahadi nyingine motomoto ambazo zinanifanya nijiulize kama huu umaskini wanaouzungumzia ni ule wa kwenye vitabu au ni kweli upo.

  Sasa kwa vile tunaelekea kwenye uchaguzi, wakuu wetu wa nchi na wapambe wao wametambua njia nyepesi zaidi ya kuwafanya wananchi wawashangilie kwa ‘uongozi' ni kuwaletea burudani za kila namna.

  Kuna msemo wa kale kuwa "maskini mpe pombe" – msiniulize huu msemo umetoka wapi na ulitungwa na nani. Ukweli ni kuwa maskini ukimpa pombe mara kwa mara utamhakikishia furaha ya kudumu na maisha ya njozi yasiyokoma lakini vile vile utakuwa umemwezesha kwa kiasi kikubwa kusahau adha na matatizo yake ya kila siku.

  Wakati wowote akianza kutoka katika ulevi na kuangalia nyumba yake ilivyo chafu, mavazi yalivyoraruka na kunuka, mikono yake ilivyo na malelenge kwa kazi ngumu wewe mkaribishe kitochi kingine au kibuyu kingine cha wanzuki, mbege, ulanzi na kama kuna uwezekano ile ‘vodka' ya kienyeji yenye kutengenezwa na mtambo maalumu uliofichwa uani kule kwa mama nanino.

  Na hata kama ukiona labda hana hamu ya ulevi hakikisha unapitisha ngoma ya mdundiko, msere, au mkaribishe kwenye tafrija ambayo kwa hakika atajisikia na yeye ni wathamani.

  Akikuuliza kuhusu masuala ya elimu ya watoto wake wewe mpatie sigara avute kuondoa wasiwasi wake, na akiuliza kuhusu mitaro ya maji machafu mwambie mnaenda Leaders Club au Uwanja wa Kirumba ambapo kuna bendi maarufu kutoka Kongo DRC!

  Sasa, ujio wa Brazil ni muhimu sana kwa CCM na kwa viongozi wetu; ni ishara ya kukua kwa uchumi na mafanikio ya taifa letu. Maskini wa Tanzania ambao bado wanahangaika na mshahara wa mbayuwayu, na wananchi wanaohangaika na makazi bora, uzazi salama, magonjwa ya kuambukiza na ukosefu wa madawati kwa maelefu ya watoto wao wanaweza kusahaulishwa matatizo hayo kwa dakika 90 za kabumbu safi kabisa.

  Ni kutokana na ukweli huu kuwa burudani kwa maskini huwa kama kileo basi ni wazi kuwa mpango huu bila ya kujali gharama yake ni miongoni mwa mipango maridadi kabisa iliyowahi kufanywa na watawala wa nchi yetu katika kutuliza maumivu ya wananchi.

  Ninafahamu kuna watu wanataka kujua ni kiasi gani kimetumika kuwaleta Brazil na wengine wanaogopa hata kufikiria kiasi hicho. Wa kundi hilo la pili wao wako tayari kuona burudani ya aina yoyote ile inapatikana kwa Watanzania na kutoihusisha burudani hiyo na matatizo ya wananchi wetu.

  Ukifikiria sana utaona ni kweli kwa watu wengi hawako tayari kuona uhusiano uliopo kati ya burudani ya soka na tatizo la nyumba za walimu; uhusiano wa soka na wanafunzi walioandamana kudai vyoo shuleni kwao, au uhusiano wa soka na ukosefu wa maji safi kilomita kumi tu toka Ikulu! Kwa hawa hakuna uhusiano wowote kati ya matumizi ya serikali na matatizo ya wananchi.

  Lakini wapo wale ambao wanaamini kabisa (na labda kwa haki) kuwa ni muhimu kuwapa burudani na kileo cha starehe Watanzania ili wasahau matatizo yao na yale ya watoto wao. Ukiangalia utaona kuna ukweli kwani ni katika burudani hizi za kila siku tunasahaulishwa matatizo yetu.

  Kama huamini angalia vipindi vinavyofuatia matangazo ya habari usiku. Baada ya kutupasha habari za watoto waliouawa huko Mbeya, ubakaji huko Morogoro, matatizo ya ardhi huko na huko na hali ngumu ya uchumi hatupewi tena muda wa kuzama katika fikra.

  Kwa haraka vipindi vya telenovella vinaanza na kutuzamisha katika matatizo ya mapenzi, usaliti na mahusiano huku tukipata burudani ya kufurahia mapenzi ya kuigiza na wengine tukikaa pembeni na machozi yakitudondoka kusikitikia wacheza filamu.

  Na wiki hii yote kuelekea mechi na Brazil watawala wetu hawatasita kutuimbia wimbo wa kututaka tufurahie nafasi hii adhimu ambayo haijawahi kutokea sehemu hii yetu ya Afrika na ni lazima "tutumie fursa hii muhimu" kuweza "kutangaza Tanzania ili kuvutia watalii". Na sisi katika upotofu wa mawazo yetu tumesahau kabisa kuwa ni hawa hawa waliotuambia mkutano wa Sullivan ungetangaza sana Tanzania, na ni hawa hawa waliotuambia majuzi tu kuwa World Economic Forum Africa nayo ingetangaza sana nchi yetu. Na kama vile walioingiwa na pepo la usahaulifu, ni hawa hawa ambao walitumia miaka ya mwanzo ya utawala wao kuzunguka dunia nzima kujulikana na kuijulisha Tanzania.

  Tutakuwa ni watu wa ajabu sana kama tutafikiria ati ujio wa Brazil utaifanya Tanzania ijulikane zaidi duniani kwa watalii kuliko Kenya!

  Tutakuwa ni watu wa kushangaza tukifikiria kuwa baada ya kipenga cha mwisho kulia jina la Tanzania litakuwa linafahamika zaidi sehemu mbalimbali duniani na kufanya kufahamika huko kugeuzwa mtaji wa kiuchumi.

  Watawala wetu wameshindwa kuchukua hatua za kuitangaza Tanzania kwa bei rahisi zaidi kuliko kuleta Brazil.

  Kwa mfano, tuna mamia ya vijana wa Kitanzania ambao wanasoma katika vyuo mbalimbali huko Uingereza na Marekani (nitumie mifano ya nchi hizo mbili). Kwa miaka yote hii sijasikia utaratibu wa serikali yetu kujaribu kuwafahamu vijana hawa na hasa vipaji vyao katika michezo na kuwasupport ili waweze kushiriki mashindano mbalimbali ya riadha kwenye nchi hizo wakiwakilisha Tanzania. Ukifikiria ni gharama ndogo zaidi kufanya hivyo kuliko kuanza moja hapa nyumbani.

  Kwa mfano, kwenye vyuo huko Texas au London wanafunzi wa Kitanzania ambao serikali imesema inawasupport (kwa makubaliano fulani) wanashiriki mashindano ya riadha wakipeperusha bendera ya Tanzania. Mashindano mengi ya riadha ya vyuo hurushwa Marekani karibu yote na ingekuwa ni nafasi ya bei rahisi zaidi ya kujitangaza kama bendera yetu ingepeperushwa na vijana wetu huko. Nchi za Jamaica, Kenya na nimeona hivi karibuni Rwanda wanatumia njia hii zaidi.

  Matokeo yake yanapokuja mashindano ya kimataifa utashangaa kuona vijana wengi wa nchi hizo wakishiriki wakiwa wanatokea Marekani au Uingereza lakini wakitangaza majina ya nchi zao. Unafikiri inakaribia gharama ya kuwaleta Brazil?

  Kama kuna watu wanaamini kabisa kuwa ati kwa ujio wa Brazil Tanzania itajulikana zaidi, mtu huyo hajakaa chini kufikiria. Hivi ukilinganisha ujio wa Brazil na Ujio wa Rais wa Marekani ni upi unatangaza zaidi nchi? Yaani mechi ya dakika tisini na ujio wa karibu siku nne ni upi ungetakiwa kutupa nafasi katika vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa na kutangaza nchi yetu? Kwa watawala wetu na mashabiki wao wanaamini kabisa kuwa Brazil itaitangaza Tanzania zaidi!

  Naomba kwa heshima nitofautiane nao. Kwanza, kwa sababu hakuna kipimo cha kisayansi ambacho wanaweza kutuonyesha kupima mafanikio hayo kabla na baada ya mechi ya Brazil, pili, kwa watu wengi wataangalia mechi hii zaidi kama burudani tu na si zaidi ya hilo.

  Njia pekee kwa mfano tungeweza kusema ya kutangaza Tanzania ni kama mechi hiyo itakaporushwa kwenye nchi mbalimbali duniani, basi matangazo ya biashara yanayohusu Tanzania na vivutio vyake yatakuwepo kwenye nchi hiyo.

  Je, ndugu yangu Mkuchika anaweza kutuambia kuwa hilo limepangwa kufanyika au ndiyo tutakuwa tunatangaziana sisi kwa sisi juu ya umuhimu wa Safari Lager na matanki ya SIMS tukifikiria kuwa kwa kufanya hivyo tunatangaza dunia nzima.

  Lakini pia zaidi ni kuwa tungeweza kutangaza vile vile kama tungeweka matangazo ya mechi hiyo moja kwa moja kwenye mtandao wa intaneti ili hata watu wasioweza kuona kwa kupitia runinga wangeweza kuona kwenye tovuti rasmi ya Tanzania ikiwa na matangazo ya biashara. Hili hata hivyo nina uhakika wa asilimia 100 hakuna aliyelifikiria.

  Ninachosema ni kuwa, tusisome zaidi kwenye ujio wa Brazil. Tusifikirie makubwa yatatokea kwa sababu Brazil wamekuja na kucheza na Tanzania.

  Na kwa hakika tusijidanganye kuwa ati baada ya mechi basi wachezaji wetu watakuwa wameambukizwa mbinu bora na uchezaji wa hali ya juu wa kabumbu. Maendeleo hayaambukizwi hata uyakalie karibu bila nguo! Maendeleo hayaji ati kwa sababu umeyasoma vitabuni au umeyashuhudia uwanjani.

  Kama hilo lingekuwa kweli si tumempata kocha wa Brazil ambaye tumemlipa mamilioni ya shilingi ambayo yangeweza kusomesha makocha wetu wa timu zote za ngazi za juu na hata kwa vyuo vyetu vikuu lakini soka yetu imepanda kiasi gani? Kama maendeleo yangekuwa yanapitishwa kama joto la jua, ujio wa Ivory Coast, Togo, na nchi nyingine si zingetubadilisha vya kutosha?

  Watanzania tusidanganyike. Hii mechi ni nzuri kwa burudani tu, nje ya hapo tutakuwa tunazugana.

  Tufurahie kabumbu hilo la samba na kufurahia kuwa tumepata heshima hiyo. Hata hivyo tusidhani kuwa ujio wa Brazil ndio tiba ya matatizo yetu katika soka. Nina uhakika hata ije timu ya soka kutoka Ufalme wa Mbinguni ikiongozwa na Mikaeli Malaika Mkuu, bado Watanzania tutakuwa ni wasindikizaji. Sababu ni kuwa hatuko tayari kulipa gharama ya maendeleo.

  Ni kutokana na hilo basi tutambue kuwa ujio wa Brazil ni kileo cha kutufanya tusahau matatizo yetu na ya watoto wetu. Ni burudani ya ngomani kwa maskini na ni sawa na mdundiko kwa wasio na mahali pa kula. Itatusahaulisha kwa muda matatizo yetu, shida zetu na huzuni zetu za kila siku.

  Mechi hii itatusahaulisha kuwa:

  Kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa hai nchini zaidi ya 100 hufa kabla hawajatimiza miaka mitano wakati Brazil ni 29 kwa kila 1,000 ambao hufa.

  Kati ya kina mama 100,000 wanaojifungua ni 160 hufa huko Brazil wakati katika Tanzania yetu hii ya CCM ni karibu 950!

  Uwezo wa kusoma na kuandika ni asilimia 70 ya mbayuwayu (Kikwete alisema asilimia kama hii inafuata upepo) wakati Brazil ni asilimia 90 ya watu wake wanajua kusoma na kuandika – enzi za yule wasiyemtaja kwa jina tena tulifikia asilimia 98! Ni rahisi kutawala taifa la wajinga kuliko la wasomi!

  Wakati maambukizi ya HIV kwa watu wazima Tanzania ni karibu asilimia nane huko Brazil ni 0.3!

  Hadi ilipofika mwaka 2007 Tanzania ilikuwa imepoteza watu wapatao 96,000 kwa ugonjwa wa ukimwi wakati Brazil ilikuwa imepoteza watu 15,000. Zingatia kuwa idadi ya watu Brazil ni 192 milioni wakati Tanzania ni 40 milioni.

  Katika takwimu za maendeleo ya watu za Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2009 Brazil iko katika kiwango cha kati, ikiwa ni nchi ya 75 wakati Tanzania ikiwa ni nchi ya 151.

  Sasa haya yote (na ningeweza kulinganisha mengine) ni katika kujaribu kuonyesha tu kuwa tufurahie soka ya Brazil inapokuja lakini tusijidanganye wala kudanganyana wala kuwadanganya wengine kuwa ati mechi ya dakika 90 itaibadilisha Tanzania, uchumi wake na mwelekeo wake wa baadaye.

  Ni sawa na kumpa kileo maskini akalewa chakari halafu ukatarajia kuwa kesho ataamka kuwahi kazini!
  Tanzania itabadilishwa na viongozi wazuri na walio bora, wenye maono sahihi ya taifa na ambao wako tayari kulipa gharama ya maendeleo.

  Tanzania haitaendelezwa kwa mazingaombwe ya michezo bali kwa vitendo madhubuti vya usimamizi wa sheria na utekelezaji makini wa sera. Siri ya mabadiliko ya taifa letu haiko Brazil wala Marekani, na haiko Japan au Uingereza; siri hiyo iko mikononi mwetu.

  Sasa tuchukulie mechi hii kama burudani ya muda na kufurahia kwa fedha zitakazopatikana (sijui kama watarudisha walizowekeza).

  Na wakati huo huo hatutaona ubaya kama watajitahidi kuwaleta Real Madrid, Chelsea, Manchester United na Arsenal. Na wakijisikia wanaweza hata kuleta timu za Ufaransa na Ujerumani na hata Cameron na Morocco. Yote ni burudani tu.

  Tukitambua hilo basi natoa wito twende tushangilie – kama una uwezo na kama hauna uwe kama mimi, angalia kwenye runinga bila kujisikia vibaya, lakini vyovyote itakavyotokea ukifika mwisho wa mechi tuondoke kwa furaha tukiimba:

  Brazil tumewaona,
  Lakini hatudanganyiki!

  Na kama tutafanikiwa kuwafunga – sitashangaa hilo likitokea, basi tuimbe tena kwa furaha zaidi kuwa:

  Brazil tumewafunga,
  Na bado hatudanganyiki.

  Na badala ya kuishukuru CCM, tuanze kujipanga na CCJ! Kwani yote hatimaye yana mwisho!
   
 2. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Hapa tu ndo katengeneza point hai!
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  "Brazil tumewafunga,
  Na bado hatudanganyiki"


  UMENENA MM
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Natumaini kitakuwa kibwagizo kizuri tu cha kuwaamsha watawala kuwa hata walezi kuna wakati huamka!
   
 5. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2010
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Hivi kweli wameletwa kwa shillingi billion kumi na ngapi vile? nimesahau figure naomba sana tukumbushane. Brazil kuja kucheza na Tanzania, Tanzanai anailipa brazili as ateam, billion kumi na ushee...., lakini mi nadhani pesa tunayo sana ila basi tu hatujui matumizi!
   
 6. g

  gutierez JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  sasa huyo rais wa marekani ni huku kwetu tz na nchi zinginezo zinazofagilia marekani ndio anathaminiwa kiasi hata barabara zinasafishwa kwa omo na foma,ni tunda la msimu kama embe,lakini brazil ipo toka enzi za kina pele,romario,ronaldo,ronaldinho,robinho hadi kina zicodinho,nchi zingine huyo rais wa marekani anapigwa mawe tu hana thamani,sina mengi sana ila nimekukumbushia tu usione kila nchi inamuona rais wa marekani babu kubwa,mugabe mwenyewe na matatizo yake ya kisiasa na uchumi na nchi za magharibi kaenda kuwaangalia brazil japo soka sio hobi yake
   
 7. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Bwana Mwanakijiji,makala hii imenigusa saaaana almanusra nitoe machozi.Sina la kuongeza ila naamini kwa dhati kabisa kuna siku maandishi yako yatabandikwa mahala flani kwa minajili ya kuhamasisha uzalendo kwa vizazi vya wakati huo.Laiti uchungu ulionao kwa nchi yetu ungekuwa unapatikana kwa mfumo wa virusi basi kungekuwa na ulazima wa "kuambukiza virusi" hivyo miongoni mwa Watanzania wengi tu ambao kwa namna flani ni kama wamenyunyiziwa dawa ya usingizi kama si kurogwa.

  Ubarikiwe sana.
   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Hyperbole,

  Personally I do not appreciate unnecessary psychedelic talmudic zigzagging, hidden codes, vague and frivolous Nostradamic stanzas used more for stylistic effect and empty poetry than meaning, Rosetta Stone-like encryption overkills, political double-talk, misplaced linguistic Sudoku, fantastic Kakuru, Kikwete's coquettes, over-elongated Da Vinci code's goose chases and the likes of these.

  Sie simpletons pamoja na wapenzi wa concise delivery tunaweza kushangaa huyu Mwanakijiji kageuka ndumilakuwili au vipi?

  Au analipwa kwa kila neno ndiyo maana analeta habari ndeefu zilizojaa alfu lela ulela, na hadithi ndani ya hadithi yenye ndoto ya mtu anayehadithia hadithi ya wezi walioingia katika pango wakakuta mzee anawahadithia hadithi ya Harun Rashid na kasri lake na hadithi zilizosimuliwa ndani ya hadithi...?


  Scarface anakwambia, you want to shoot, shoot. All this hyperbole will only distract and end getting you killed in the war.

  Kuna watu hawajui hyperbole, watakushangaa tu.

  Naelewa eminent criticism ni nini, which is supposedly the height of class when it comes to criticism.Lakini unapoweka hyperboles kama hii mwanzo wa habari yako inakuwa imevuka hata eminent criticism, inakuwa inaenda kwenye unafiki na kuwa wooden and scripted. Ukiforce hyperbole na eminent criticism sehemu visipostahili una risk kuonekana hujui unasimama wapi kwa watu wanaopenda kudeal na facts na kutupa hyperbole na over-exaggeration.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,075
  Trophy Points: 280
  Mkjj una kipaji kikubwa sana cha uandishi. Umetulia na kutafuta info muhimu zaidi za kuipa uzito mkubwa habari hii. Hongera sana kwa kazi nzuri. Habari hii ingebidi iandikwe katika magazeti yote ya nchini ili isomwe na wengi waweze kuelewa nini kinachoendelea ndani ya Tanzania yetu. Please keep it up!
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  I like that what you accuse me of you practice urself right now. Bahati nzuri wengine tunaandika kwa ajili ya mtu wa kawaida ambaye hatalazimika kuchukua dictionary ya kiswahili kujua tumesema nini au kulazimika kurudia rudia mistari kujaribu kudecipher maana. Na katika ulimwengu wenye conflicting interests ni muhimu kujua how to balance those interests..

  kwenye hili hakuna haja ya kuradicalise anything.. just a message given to the intended audience.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Mimi naona wewe ni yule ndege Kong'ota!...mkuu unawezaje kupasua haya mawe?
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Inabidi niwe kama mbayuwayu kwa kweli.. LOL
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Tofauti yangu mimi na wewe ni kwamba mimi siandiki for the masses, na wewe unaandika for the masses.

  Big difference.

  Halafu tofautisha genuine poetic effect / sarcasm niliyokupa hapo juu na dilapidated hyperboles zako ambazo ziko so open to interpretation to the extent of being practically meaningless. Kama unataka kuandika ushairi na hadithi style hii ni sawa, lakini kama unataka kuandika serious political commentary, serious thinkers watakuona frivolous joker.
   
 14. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, bado unaiwaza CCJ? Makala ilianza vizuri, thanks for that.
   
 15. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Orwell's rule for written English:

  1,never use a metaphor,simile,or other figure of speech which u r used to seeing in print.
  2,never use a long word where a short one will do.
  3,if it's possible 2 cut a word out,always cut out.
  4,never use the passive where u can use the active.
  5,never use a foreign phrase, a scientific word,or a jargon word if u can think of an everyday English equivalent.

  Break any of these rules sooner than say anything outright barbarous.

  Bora Mwanakijiji aliyeandika makala ndefu,ya kuvutia na yenye uzito mkubwa na inayoeleweka (kwa sie tunaofahamu makala ni kitu gani) kuliko wewe uliyeandika kitu kifupi na kisichoeleweka (except for your misguided attempt ya kutuonyesha una misamiati mingapi ya Kiingereza).Tell you what,sio kila anayejua alfabeti anaweza kuandika makala,na uandishi wa makala unaotegemea kamusi mkononi ni mithili ya kupanda Milima ya Himalaya kwa kutambaa (will take ages if not eternity).

  Mwanakijiji,tunaojua kuelewa tumelelewa vizuri,wenye kutafuta zaidi ya kuelewa ulichoandika wapuuze tu.

  Serious thinker?What a joke!
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Obviously sarcasm is not your strong suit.

  As for Orwell's rule, as cliche ridden and generalizing as it is, I am glad you brought it up.Mwanakijiji needs it more than I do, and he needs to apply it in whatever language he uses.

  Just look at his piece. Watu makini wanaonunua magazeti wanataka ideas, data, context, history, projection, punditry. Siyo ushairi wa kujaza gazeti kwa kurudia rudia mambo kama riwaya za kiarabu au agano la kale. Kama wanataka poetic over-exaggeration na mizaha mingine watakuja hapa JF. I am particularly critical kwa sababu hii piece imeandikwa katika gazeti, na si kipande cha hapa JF tu ambacho ningeweza kuki tolerate zaidi.

  Orwell's rule my foot, if you use a simile not usually seen in print, it might as well be foreign.Contradiction. The point of using a simile is to provide a shorthand for an idea, a shortcut if you like, of saying a complex idea in a simple way. When not being sarcastic as above, If I have a choice of using a popular simile that is readily understood or an obscure simile, of course it would make sense to use the popular one. This attempt at uppity may suit "The Economist" and it's clientele, but I am not writing for 'The Economist" and do not have to abide by their style book. By the way even "The Economist" and "The New York Times" use liberally similes usually seen in print, what does that say about your dead "Orwell's Rule" ?

  About never using a long word where a short one will do, tell that to Mwanakijiji, tell him never to use a long article where a short one will do.

  So goes for cutting words

  Never use a passive voice? I say never say never unless you are saying never say never.

  The use of a passive voice maybe be perfectly fine, depending on the stylistic context.

  Ndiyo nyie mnaofikiri kitu complex kama lugha kinaweza kuwa dumbed down to a couple of static laws.

  How serious of a thinker can you be with a scripted imagination like that?
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jun 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  the problem you are applying that standard to me but not to you. Unalazimisha "sheria yako ya uandishi" ifuatwe na kila mtu na kwenda nje ya sheria hiyo ni kujitakia matatizo... on the other hand.. kitu complex kama lugha kinaweza kweli kuwa dumbed down to a couple of static laws?
   
 18. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tatizo lako ni ubishi pasipo hoja za msingi.Unaamini kuwa unajua kupita kiasi kwamba hakuna nafasi ya kukosolewa.

  Kwa kukusaidia,japo natambua kuwa natwanga maji kwenye kinu kwa vile utabisha tena,uandishi wa makala ni tofauti na uandishi wa posts kwenye forums,especially zile zinazoandikwa kwa minajili ya kuhamisha frustrations kutoka kwa mwandishi kwenda kwa yeyote yule.

  Hiyo makala unayojaribu kuikosoa imejitosheleza,lakini mwandishi halazimiki kulazimisha msomaji mbishi aafikiane nae. Kichekesho ni kuwa wengi wa wakosoaji wakubwa wa makala au machapisho ya wenzao hawana uwezo hata wa kuandika japo wasifu wao,na kimbilio lao kuu ni kuhamisha maneno kutoka kamusini.

  By the way, kama makala ni ndefu au huipendi kwanini uisome?Hukulazimishwa kusoma, hukuamrishwa kuwa ni kosa la jinai kuachana nacho, lakini la muhimu zaidi, kipi unachoweza kuandika ambacho makala unayoipigia kelele haina?
   
 19. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Hapa naona hujakosea maana Sideeq "mla ngamia" akianza kuteremsha madudu yake ni kizunguzungu tu kwa kwenda mbele. Damn!
   
 20. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  Hapa mwenye macho na uelewa na ufahamu haambiwi tazama msg delivered without error
   
Loading...