Hongera Bi. Elsie Kanza, mshauri wa Uchumi wa Rais Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera Bi. Elsie Kanza, mshauri wa Uchumi wa Rais Kikwete!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Mar 9, 2011.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Bibi Elsie Kanza, Mshauri wa Uchumi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa na Taasisi ya World Economic Forum (WEF) kuingia katika kundi dogo la heshima la vijana waliothibitisha vipaji vya uongozi la Viongozi Vijana Duniani (Young Global Leader- YGL)) kwa mwaka huu wa 2011.

  Bibi Kanza ni mmoja wa kinamama wawili Watanzania vijana waliotangazwa na WEF mjini Geneva, Uswisi, leo, Jumatano, Machi 9, 2011, kujiunga na kundi la YGL ambalo linashirikisha Waafrika 14 miongoni mwa vijana 190 waliochaguliwa kutoka nchi 65 duniani kujiunga na kundi la vijana la Young Global Leaders kwa mwaka huu wa 2011.

  Mtanzania mwingine aliyechaguliwa ni Susan Mashibe, Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni mawili – TanJet na Kilimanjaro Aviation Loegistic Centre - ambayo yanashughulika na usafiri wa anga.

  Mabibi Kanza na Mashibe wamechaguliwa kutoka miongoni mwa viongozi vijana 5,000 waliopendekezwa kutoka duniani pote na hatimaye kuchaguliwa kwenye mchujo mkali na Kamati Maalum chini ya uenyekiti wa Malikia Rania Al Abdullah wa Ufalme wa Hashemite wa Jordan.

  YGL wa mwaka huu wanajiunga katika kundi la viongozi vijana wengine 668 walioteuliwa miaka ya nyuma, na miongoni mwao yumo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bwana Lawrence Masha.

  Kila mwaka WEF hutoa heshima hiyo ya YGL ili kutambua vipaji vya uongozi vya vijana kutoka pote duniani kwa mchango wao katika uongozi, mafanikio ya kitaaluma ana ari yao ya kuleta mabadiliko katika jamii na huchaguliwa kutoka nyanja zote za maisha ikiwemo biashara, serikali, vyuo vikuu, habari na mawasiliano, taasisi zisizokuwa za kiserikali, utamaduni na sanaa.

  Bibi Kanza aliteuliwa kuwa Mshauri wa Uchumi wa Rais Kikwete tokea Machi mwaka 2006. Kabla ya hapo alifanya kazi katika Wizara ya Fedha (2002-2006) na Benki Kuu ya Tanzania (1997-2002).

  Anayo Shahada ya BSc katika Uongozi wa Biashara za Kimataifa kutoka United States International University-Africa (USIA-A), Shahada ya Uzamili ya MSc katika Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Uingereza na Shahada nyingine ya Uzamili katika Uchumi wa Maendeleo kutoka Williams College, Marekani.

  Bibi Kanza ndiye alikuwa Mratibu wa Taifa wa Mkutano wa WEF-Afrika uliofanyika kwa mafanikio makubwa mjini Dar es Salaam Mei, mwaka jana, 2010 na pia ametunukiwa Tuzo la Uongozi la Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Afrika Kusini.

  Wengine waliojiunga na YGL mwaka huu ni pamoja na Makamu wa Rais (Uhandisi) wa Kampuni ya Google kutoka Ukraine, mwanahewa mmoja kutoka Japan, mtangazaji mmoja wa habari wa televisheni ya CNN, mwandishi mmoja wa habari kutoka Nigeria, msanii wa filamu kutoka China, Meya wa Jiji la Calgary, Canada.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu
  DAR ES SALAAM.
   
 2. LD

  LD JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hongera sana Bi. Elsie Kanza.
  Wanawake Tunaweza!!!!!
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kumbe washauri wa uchumi wa Rais hawajasomea uchumi?

  Duh, ndio maana vitu vinaharibika. Halafu what is US International University iliyopo Nairobi, Kenya??? Something is wrong here?
   
 4. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  siasa za vipofu hizo. sifa zinatangulizwa kabla ya mafanikio. maelezo ya background pekee yanatosha kuonesha kuwa ni mtoto wa nyumbani. hajawahi kusoma tz wala hajawahi kuanya kazi za kima cha chini. ni uthibitisho mwingine wa atahri za matabaka tunaoendelea kuyajenga katika elimu. ones future depends on ones quality of eduaction. anakumbusha jinsi wadogo zangu walivyofeli mitihani ya form four na kupotezewa muda wao kwenye shule za kata

  yote heri, Mungu atatunusuru
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  United States International University???!!! Kipo wapi hiki chuo?
   
 6. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
 8. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Hawa ndo watu tunatakiwa kuwa discuss hapa JF nje ndani sio wasanifu hotuba kina January Makamba.

  • Huyu E Kanza ni muumini wa philosphophy gani ya uchumi?
  • Amenadika papers gani za kichumi?
  • Kwenye uchumi kabobobea kwenye mambo gani?
  • Anamshauri nini hasa rais wetu
  Sasa hapa hongera hongera za nini. Uchumi wa Tanzania ndio hivyo.

  Sio haki kabisa kama katika watu mia moja (100) 90 wanamkosoa msanifu hotuba wa rais (January Salva) na katika watu hao hao mia 90 wamsifu mchumi. Teh teh teh teh. Hawa ndo watu wanatakiwa tuwajue

  Huyu mchumi ndio anafanya hata hizo hotuba tuwalaumu kina January na Salava rweyemamu.


  Vipaji vya uongozi au
  perfomance ya uongozi. Maana hata JK ana kipaji cha uongozi ndio maana akawa rais lakini perfomnce yake ni tofauti na kipaji.

  Mambo ya ku reward traits badala ya performance just Bcs yanafanywa na mataifa na taasisi za kimataifa yatatupofusha na ni danganya toto changa la macho

  Sina cha kumpongeza huyu dada
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hongera zake sana. Tunashukuru kwa taarifa hii.

  Naomba kujua umri wa huyu dada maana ameingia kwenye rekodi za viongozi vijana. Nikiangalia CV yake amenza kazi tangu 1997 alikuwa na umri gani? Au vijana kwa hii tuzo inamaanisha umri gani? Just want to know.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Mar 9, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
  Sasa huyu mshauri wa uchumi yeye anajua sababu za Tanzania kuwa maskini? Manake bosi wake alisema hajui...
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kipo katika ranking za africa cha 78 link hii hapa chini:-

  Ranking Web of World universities: Top Africa
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Mar 9, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,407
  Trophy Points: 280
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ndio maana serikali haina sera zozote za kupambana na mfumuko wa gharama, kudhibiti matumizi na kuinua hali ya uchumi nchini. Rais mwenyewe ni agricultural economist, ingawa hajafanya lolote katika kilimo. Mshauri wake ni mtaalamu wa biashara za kimataifa. Wapi na wapi?
   
 14. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Dada Regia umesahau kuwa hata JK katika miaka yake ya hamsini na alijiita kijana??nampa Hongera zake...tunaomba tu atuwakilishe vyema!!
   
 15. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu katika kutengeneza economic policy ya nchi inafaa uwe umeshiba vizuri uchumi na kufahamu kwani inategemea zaidi na mazingira ya nchi husika.

  Ukitazama CV ya huyu amesoma Bsc ya Business Administration ambapo sidhani kama kuna uchumi humo au zaidi litakuwa ni somo moja la uchumi. Inawezekana ikawa Microeconomics, kwenye macro hawagusi hawa. Vilevile mshauri anatakiwa awe amebobea katika fani husika ili awe na scenarios mbali mbali katika kumshauri rais.

  Sasa maswali ni je Tanzania hakuna wachumi waliobobea? Pili ameandika wapi au kufanya kazi gani za uchumi kuonyesha na yeye amebobea?
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu ndio maana nikasema something is wrong here kwasababu Marekani chuo hakipo kipo Nairobi Kenya
   
 17. o

  othorong'ong'o Senior Member

  #17
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Anazawadiwa kwa lipi ambalo amelifanya?,au sifa ni young leader,basi hata mie ni young leader kazini kwangu!
   
 18. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hongera ya nini uchumi wenye uko kwenye jalala. Is that achievement wakati watanzania wanalalamika kila kitu bei juu. I'm not jealous but sijui hizi hongera za nini!!
   
 19. k

  kamalaika Senior Member

  #19
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Chuo kiko San Diego na kina campus nchi tofauti duniani ikiwemo Kenya. Campus ya Kenya inaitwa USIU-A
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu angalia usije kubandikwa kuwa wewe hupendi wanawake wakifanikiwa najua hongera zote kwakuwa mwanamke ila swali linabakia pale pale je yeye ni mchumi? tunaomba CV yake basi.
   
Loading...