Hongera BAVICHA kwa kupinga mazingaombwe ya Mambosasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,628
218,059
Ile Taasisi pekee ya vijana ( BAVICHA ) ambayo ni Imara Kupita zote kwenye eneo la maziwa makuu na Africa , imepinga vikali sarakasi za RPC wa Dar es salaam ndugu Mambosasa ya kuwaachia huru wauaji halisi wa Akwilina , ikiwa ni katika kutengeneza njama za kishamba za kuwahusisha viongozi wa chadema na mauaji hayo.

Ikumbukwe kwamba Lazaro Mambosasa mara tu baada ya mauaji hayo ya kishenzi kutokea alikiri hadharani kuhusika kwa jeshi la polisi kwenye mauaji hayo ( ukiwa muongo usiwe msahaulifu ) , lakini ghafla amegeuka kwa mtindo wa U- TURN na kudai polisi hao hawahusiki tena na akadai kwenye maandamano yale kila kiongozi wa chadema alikuwa na silaha , na kwamba miongoni mwao anatafutwa aliyemfyatulia risasi Akwilina.

Mwenyekiti bora wa Taasisi za Vijana barani Afrika Mh Ole Sosopi amepinga vikali maelezo ya Mambosasa , na kudai kwamba polisi wameua , wamejikamata , wamejichunguza na hatimaye wamejiachia wenyewe , Sosopi amemuomba Rais wa Tanzania kuunda Tume ya Majaji kuchunguza uchafu huo , Tayari mpango wa Bavicha kusambaza waraka kwenye balozi zote zilizomo nchini umekamilika .

Mungu ibariki Bavicha .
 
Kwa sasa Bavicha ndio ufunguo wa akili mpya ya vijana barani Africa
Well done Bavicha

Haiwezekani damu ya yule kijana Akwilina muwe mmeimwaga, halafu mjitwalie kujichunguza halafu wenyewe mnajiachia huru kwa madai kuwa imekuwa vigumu kumbaini Muuaji!!!

Ukifuatilia hata maelezo yake Kamanda Mambosasa yanajicontradict, huwezi wewe mtu mmoja, baada ya mauaji yale ya "kizembe" sana, tarehe 17/2/2018 ukiri kuwa mauaji yale yamefanywa na mmoja wa askari wake.......

Halafu baadaye, DPP Mganga, aje na story nyingine kuwa tumewaachia huru maaskari wote kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyehusika na kifo hicho, na badala "tumegeuza kibao" na tunawashikilia viongozi wote wakuu wa Chadema, kuona kuwa mmojawapo ndiye aliyefyatua risasi zilizomwua mwanafunzi yule!

Ninyi askari wa TZ fanyeni kazi yenu kwa weledi, mnajiharibia sana kwa kufanya kazi kwa "maagizo" toka kwa Jiwe, kwa kuwa hivi sasa nyote mnaonekana "punguani" kabisa!

Tukumbuke kuwa Jiwe aliwahi kutamka hadharani kuwa I WISH I COULD BE IGP!

Je hiyo ndiyo kazi ya IGP "ikishinikizwa" na maagizo toka juu??
 
Last edited:
Huyu kamanda huenda ana ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu wataalamu wa afya ya binadamu watatutajia jina lake! Kwani kigezo alichokitumia kuutangazia umma juu ya uhusika wa polisi katika mauaji yale ni kipi? Kama yeye aliamuru uchunguzi na kisha kuwabaini aliwapeleka sero na alijiridhisha kuwa kweli hawa ndiwo na huyo dpp kawaachia kwa sababu azijuazo ni kwanini basi mambosasa asingewakamata tena na kulifungua jalada upya ili kumwonyesha dpp kuwa ana sababu tosha za kufanya hivyo? Haoni kama dpp kamshushua kuwa hajui kazi yake ipasavyo?
Basi niseme sawa na nimwambie kuwa huko mahabusu za polisi wamejaa watuhumiwa dizaini ya hao polisi na dpp awafanyie wepesi waachiwe!
 
Ukweli mtupu !
 
Mambosasa tafadhali usikate mauno na hizi ngoma wanazopiga wanasiasa..utakuja kujuta Kamanda ooonho...!
OMARI MAHITA IGP AMBAYE REKODI YAKE YA UKATILI NA KEJELI DHIDI YA WAPINZANI BADO HAIJAVUNJWA , BAADA YA KUSTAAFU ALIBURUZWA MAHAKAMANI KWA KESI YA AIBU SANA YA KUMPACHIKA MIMBA HOUSE GIRL WAKE MWENYEWE NA KURUKA MATUNZO YA MTOTO , BADO HAIJAFAHAMIKA KAMA ALIMBAKA BAADA YA KUMTISHA NA MIVYEO YA UPOLISI AU WALIKUBALIANA , TUNAENDELEA KUMCHUNGUZA , TUKIKAMILISHA MAJIBU YATAWEKWA HAPA HAPA JF
 
Huyu kamanda huenda ana ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu wataalamu wa afya ya binadamu watatutajia jina lake! Kwani kigezo alichokitumia kuutangazia umma juu ya uhusika wa polisi katika mauaji yale ni kipi? Kama yeye aliamuru uchunguzi na kisha kuwabaini aliwapeleka sero na alijiridhisha kuwa kweli hawa ndiwo na huyo dpp kawaachia kwa sababu azijuazo ni kwanini basi mambosasa asingewakamata tena na kulifungua jalada upya ili kumwonyesha dpp kuwa ana sababu tosha za kufanya hivyo? Haoni kama dpp kamshushua kuwa hajui kazi yake ipasavyo?
Basi niseme sawa na nimwambie kuwa huko mahabusu za polisi wamejaa watuhumiwa dizaini ya hao polisi na dpp awafanyie wepesi waachiwe!
kuna kila dalili ya Mambosasa kuja kufungwa huko mbele , tuendelee kuvuta subra .
 
Haya yanayojiri yanatuthibitishia kuwa waafrika hatuwezi bado kujitawala, (Credit to Donald Trump) na kama ni uhuru basi tuliidai ki makosa sana sana.

Imefanya watu ambao ki msingi walistahili kuwa "Desk Clerks" kuikwaa ofisi ya juu kabisa ktk nchi.... Very Pathetic and Shameful.
 
Back
Top Bottom