Hongera Baruan Muhuza wa Azam. Kipindi chako cha leo kuhusu mkutano mkuu wa CCM, umetisha!

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Katika kipindi cha leo cha Mizani ya Wiki cha Azam Two, Baruan Muhuza alikuwa na kada mmoja wa ccm na Ng'wanza Kamata wa UDSM.
Tofauti na waongoza vipindi wengine wanaohoji mambo rahisi rahisi ili kufurahisha chama au kusifusifu kujikomba kwa watawala.

Muhuza kauliza maswali magumu kwelikweli na ya msingi. Maswali aliyouliza zaidi ni yale ya kauli zenye utata au ukinzani zilizotolewa jana.

Swali mojawapo lilikuwa kuhusu kauli ya Kikwete ya kuhusu umuhimu wa chama kuchangamka na kufanya siasa hasa kwenda kwa wananchi kuimarisha chama. Huku ikionekana kupingana na kauli ya Magufuli ya kuzuia siasa hadi 2020.

Wazungumzaji wote akiwemo huyo kada aliyekuwa mmoja wa wagombea urais ndani ya ccm walionekana kupingana na kuzuia siasa kwani huwezi kufanya siasa bila kwenda kwa wananchi hasa kwenye mikutano ya hadhara.

Swali lingine lilikuwa kauli ya Magufuli kwamba siku ile Kikwete anaimbiwa tuna imani na mtu fulani angekuwa yeye nusu yao angewapoteza. Swali likawa Je, hii hali ya kutokuwa na uvumilivu kiasi hiki si hatari kwa chama. Angekuwa yeye siku ile si ndio chama kingepasuka?

Jibu toka kwa kada wa ccm ni kwamba Magufuli ameoamua kuonesha udhaifu wake ili wengine wamsaidie ili kuwa mvumilivu ikiwa atakutana na hali km hiyo. Ila wote wamekubaliana kiongozi wa chama kikubwa km ccm anapaswa kuwa uvumilivu na utulivu mkubwa katika kuchukua maamuzi magumu. Hivyo anapaswa kujifunza uvumilivu asikisambaratishe chana.

Swali lingine kubwa lilikuwa ni ishu ya kuwataka watumishi wa umma wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa kutii chama na kukitumikia chama.
Wote wa wazungumzaji wamesema kwamba hiyo kauli ilikuwa ya bahati mbaya. Kada wa ccm kasema ni vizuri watumishi wa umma waachwe wasimamiwe na wasimamizi wao km kanuni za utumishi zinavyotaka na sio kusimamiwa au kuingiliwa na makada wa
chama. Kamata kwa upande wake amesema kauli ya Magufuli imedhibitisha madai ya muda mrefu ya vyama vya upinzani kwamba kuna watu wanapaswa kuwa watumishi wa umma lakini wao wamekuwa wakifanya kazi za chama kinyume cha taratibu za utumishi wa umma. Hasa wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi. Km mkurugenzi ni kada atatenda haki kw wapinzani? Hivyo wameshauri utumishi wa umma utenganishwe na ukada wa vyama vya siasa km inavyopaswa!

Kwa ufupi, Baruani Muhuza kweli ni mwandishi mweledi kwelikweli. Kamata anaonesha ana kaukada kidogo lakini Baruani Muhuza kambana kwelikweli ikabidi tu aseme ukweli!
 
hahaha!!! unawashwa wapi jameni ukunwe!? mfanyakazi wa crdb aache kutekeleza plan za benki ahangaike na ilani?
Ilani iliyoshinda uchaguzi ni ya ccm.

Kila mfanyakazi wa nchi hii anatakiwa kusimamia yaliyoahidiwa kwenye ilani ya ccm.

Eg, elimu bure, ujenzi Wa barabara , upatikanaji wa madawa hospitalini etc.
 
Ilani iliyoshinda uchaguzi ni ya ccm.

Kila mfanyakazi wa nchi hii anatakiwa kusimamia yaliyoahidiwa kwenye ilani ya ccm.

Eg, elimu bure, ujenzi Wa barabara , upatikanaji wa madawa hospitalini etc.
Wewe niiiiii .... malizia mwenyewe.... ila ujumla hujitambui.
 
Yaani Unamaanisha kwamba amekivua nguo chama chawala? Hahahaaha Safi kabisa, Waaambie wachutame
 
Ni huku kwetu tu swali moja lina majibu mengi ie kuna wakati 1+1=2 na kuna wakati 1+1=3.Sasa jaza mwenyewe.
 
Ilani iliyoshinda uchaguzi ni ya ccm.

Kila mfanyakazi wa nchi hii anatakiwa kusimamia yaliyoahidiwa kwenye ilani ya ccm.

Eg, elimu bure, ujenzi Wa barabara , upatikanaji wa madawa hospitalini etc.
HUJAELEWA rudia kusoma uzi hapo juu
 
HUJAELEWA rudia kusoma uzi hapo juu
Kama alivyokabidhiwa mzee magufuli ilani, na iwe hivyo kwa sekta zote nchini; NGOs, Hospitali, makanisani, misikitini na kwingineko, ili utekelezaji wa ilani yao isimimamiwe na kuhubiriwa ipasavyo huko kwenye nyumba za ibada....
 
Hahaha! Wanataka kulazimisha concept ya chama kushika hatamu ndani ya mfumo wa vyama vingi! Kama sio vurugu wanatafuta ni nini?
 
Ilani iliyoshinda uchaguzi ni ya ccm.

Kila mfanyakazi wa nchi hii anatakiwa kusimamia yaliyoahidiwa kwenye ilani ya ccm.

Eg, elimu bure, ujenzi Wa barabara , upatikanaji wa madawa hospitalini etc.
Unaandika CCM tu bila hata kujua maana ya point yako,,,ccm ndo mavi gani kama sio mkojo unaonuka ndani ya nchi
 
Maskini.... Muhuza leo anasifiwa kwa maswali rahisi kabisa haya... UKAWA waneishiwa
 
Back
Top Bottom