Hongera Askofu Mteule John c Ndimbo kuteuliwa kuongoza Jimbo la Mbinga

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Tarehe 12.3.2011 ni siku ya kumbukumbu kwa Padre John Chrisostom Ndimbo kutangazwa na Baba Mtakatifu kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Mbinga.Anakuwa Askofu wa pili tangu kuanzishwa kwa Jimbo hilo mwaka 1986.Askofu wa kwanza amestaafu kwa mujibu wa sheria za kanisa katoliki.Alikuwa Dr Emmanuel Mapunda.

Hakika ni pongezi nyingi kwake kwani anastahili kushika nafas hii.Padre huyu ni mwana elimu mzuri aliyeapata kufundisha katika seminari ndogo ya Likonde tangu alipopata daraja la upadre mwaka 1989.Alikuwa mkuu wa seminari tangu mwaka 1995 hadi Octoba 2010 akiwa pia ni mwalimu wa Fizikia na Hesabu.Lakini pia katika miaka hii ya karibuni alikuwa akifundisha somo la Kiingereza kidato cha tatu na nne.Matunda ya somo hili yameonekana katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010.

Sisi tuiliopata kufundishwa naye tunaamini ana uwezo wa kuwa kiongozi katika ngazi aliyopo.Binafsi nina mwona kama ndiye alinifungulia mafanikio yangu kielimu hata kimaadili.Nimeifahamu Fizikia na hesabu kupita kwake.Hakika na mwalimu wa kupongezwa sana.Japo nafas anayoshika ni nyeti na ngumu lakini naamin ataimudu kwa uwezo wa Mungu aliyemchagua.Mungu akupe mafanikio mema.
 
LIKONDE SEMINARY my bro alisoma na kumaliza form 4 hapo miaka ya mwanzo ya themanini. hiyo shule inatoa watu vichwa balaa. jamaa ni holder wa CPA ana masters ya business adminstration na ana degree ya IT. wakati anasoma likonde dream yake ilikuwa awe engineer anapiga hesabu physics chemistry biology vibaya mnoo na fine arts anakuchora huku akikuangalia. so kila nikisikia LIKONDE nakumbuka a school of excellence. km askofu ndimbo kapitia hapo basi he is a man for that post.
 
Hakika Chimunguru huyu askofu alikuwa ni chachu ya maendeleo ya kielimu pale.Alifanya vizuri sana.Japo najua changamoto inayomkabili mbele yake ikiwa ni pamoja na kurudisha nidhamu ya mapadre wake kwani kwa siku za karibuni maadili yamepungua kwa baadhi ya mapadre.
 
Back
Top Bottom