Honey nimekumiss sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Honey nimekumiss sana

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Yona F. Maro, Aug 22, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Honey

  Sema

  Huwa napata furaha sana kila ninapopata muda angalau kidogo wa kukuandikia yaani kukujulia hali yako , kuulizia maendeleo yako , kukusalimia na kujua mambo mengi zaidi kuhusu wewe , Honey najua wewe ni mzima tena sana na utakapopata barua hii kama ulikuwa umefifia najua utaamka utaanza kungaa na kuangaza kuliko nyota kama ulikuwa umelala najua utaamka kama mlinzi , kwa hakika wewe ndio Mlinzi wa maisha yangu mimi ni wa maisha yako pia .

  Honey

  Nina muda mrefu kidogo sijakuandikia email yoyote zaidi ya kupigiana simu , kuandikiana sms na njia zingine za mawasiliano lakini kwa maandishi ni muda kidogo sijakuandikia , samahani sana kwa hilo , najua unajua kwamba ninakuwa na majukumu mengine mengi tu ya kuandika na kufanya vingine , siwezi kuchanganya hivi na mapenzi yetu kile ninachoandika ni maalumu kwa ajili yako peke yako sio kwa dunia nzima ndio elewa maana yake .

  Honey

  Kwa kweli nashukuru sana kwa kuweza kufikishana mpaka hapa tulipo sasa hivi , mpaka hapa ninapopata nafasi ya kukuandikia email hii ni ngumu sana kwa wengi kuwa kama sisi kufika hapa tulipo mengi tumepita na kukutana nayo yote tumeweza kupambana nayo na kuyashinda bado tuko ngangari bado tunapendana na bado kila mmoja hajaonyesha nia yoyote ya kumchoka mwenzake .

  Nimekuwa nasoma magazeti mtaani na kusoma mitandao mbali mbali ya kiswahili , nimeona maajabu sana , sikuhizi vijana kama sisi kama ni mwanaume basi anapotafuta mchumba utakuta pale ameweka kipengele cha LIMAMA LENYE UWEZO kama ni mwanamke basi naye anataka LIBABA LENYE UWEZO limpangie nyumba na kumpa pesa za matumizi namambo kama hayo .

  Ninapoona matangazo kama hayo nikijiangalia mimi mwenyewe nikikuangalia wewe nikiangalia na wengine najiuliza vijana wamekubwa na nini sasa hivi wapi tunaenda kwanini vijana wamefikia hatua hiyo ya kubadili mwelekeo wa kizazi hichi kabisa , maajabu ni kwamba wengi wanaosema wanataka MIJIMAMA unakuta ina Visichana vyao viwanafunzi majumbani na mitaani hii mijimama a mijibaba inatoa hela halafu inapelekwa kuhudumia wengine .

  Mijibaba hii na mi mama hii ndio inachangia kwa kiasi kikubwa katika kusambaza mgonjwa ya zinaa kwa mabinti hawa , vijana hawa halafu wanawakimbia pale ambapo unakuta kijana amezidiwa na magonjwa na shida zingine za dunia , kwasababu michezo hii inakuwa ni ya siri kubwa unapoaanza kuumwa basi na yule jibaba au jibaba linakimbia halitaki kusikia chochote kuhusu wewe

  Kwa kusema hayo hapo juu , nakumbuka siku moja nilikuwa napita mitaani , mtu na mpenzi wake wakawa wanagombana huyu mwanamke akamwambia yule kijana kwamba yeye ni sawa na Nguo nzuri iliyopo dukani inauzwa kwahiyo mtu mwingine akiwa na dau kubwa anaweza kununua nguo hiyo na ikawa yake akawa anaitumia , huyu dada hakujua kitu kingine kwamba nguo pia inavaliwa yule aliyenunua anaichoka au inaweza kuchanika au ikazeeka akaiacha NDIO MAPENZI YAO HAO

  Pia kuna wakati wengine wakawa wanagombana mara yule dada akamwambia mwanaume MIMI NAFANYA UMALAYA NDIO NAKUPA HELA YA KULA WEWE USINITISHE , mambo kama haya ndio yanayochangia ukuaji wa hao majimama na majibaba kwa sababu hawana shida wao wanahangaikia familia zao wanataka vijana kwa ajili ya starehe muda mwingi .


  Hata hivyo ni haki ya kila binadamu kuamua kile anachotaka yeye lakini watu wawe wanaangalia adhari za muda mrefu kwao wakiamua kuchukuwa maamuzi hayo

  Honey

  Nimekuwa nakupenda sana toka siku ya kwanza nimeanza kujuana na wewe , nikaendelea kukupenda , kushirikiana na wewe kwa hali na mali mpaka hapa tulipofika sasa hivi , tafadhali kama unaona kuna chochote kinakutatiza nijulishe kwa njia yoyote ambayo wewe unaona inafaa kama unaogopa kuniambia basi unaweza kutumia rafiki zangu au ndugu zangu au unaweza kunitumia Email kama hivi uwe muwazi na uonyeshe ukomavu wa akili na mawazo yako yapanuke zaidi .

  Basi tuendelee kuwa waaminifu , wasikivu , wavumilivu na wenye kutakiana maisha mema na mazuri , Ahsante sana kwa kuendelea kuniunga mkono na kuendelea kuwa na mimi mpaka dakika hii ninapoandika ujumbe huu , sina zawadi ya kukupa lakini nakuahidi upendo wa dhati ambao siwezi kuupima kwa chochote kile .

  Hayo ndio yangu kwa leo na weekend hii ,Nakutakia Weekend njema na maisha mema , utakapopata email hii naomba unijibu hata kwa mistari 2 tu ukipata nafasi najua wewe ni mvivu sana wa kuandika lakini jitahidi utajifunza kidogo kidogo mpaka kuwa mzoefu .

  Wasalimie wote Hapo ulipo

  Mpaka wakati mwingine tena
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  very creative don't u think?

   
 3. HOPECOMFORT

  HOPECOMFORT JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 2,784
  Likes Received: 3,519
  Trophy Points: 280
  Nimm eeee.Thanx sana honey kwa ujumbe mzito utakao nifanya nitabasamu cku nzima.Lkn honey mi cpendi kumshirikisha mtu mwingine maswala yetu bwana,siunajua binadamu wengine walivyo? Kwa lolote baya au zuri nitaku face mwenyewe. Gd day honey.
   
 4. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Shy,long time no see,karibu tena.
   
 5. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Yaani utadhani ndo mpenzi wangu kaniambia.... We have long time relatnship nw. 8Years Si mchezo

  Never cheated on Each other

  Thanks shy
   
 6. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Shy, asante sana sikujua kama unanipenda hivyo :bounce:
   
 7. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,671
  Trophy Points: 280
  Mapenzi au ni njaa ya kupendwa?
   
Loading...