Homa ya Degedege Ni Nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Homa ya Degedege Ni Nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by ZionTZ, Jun 15, 2012.

 1. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Degedege Ni Nini?

  Ni hali ya ghafla ya kutingishika kwa mwili mzima au miguu na mikono, ambayo husababishwa na kukakamaa kwa misuli ya mwili. Hali hii uhusishwa na magonjwa ya ubongo kama kifafa, vichocheo vya kwenye damu kama upungufu wa sukari(hypoglycemia), upungufu wa oxygen(hypoxia), kushuka kwa shinikizo la damu(hypotension) na maambukizi na homa ya degedege.

  Homa ni Nini?

  Ni hali ya kawaida ya mwili kujikinga na maambukizi. Na kwa watoto hutokea pale joto la mwili linapokuwa zaidi ya nyuzi 38 za sentigredi.


  Homa ya Degedege Ni Nini?

  Ni degedege linalotokea kwa watoto ghafla likiambatana na homa kali iliyotokana na kuongezeka haraka kwa joto la mwili. Ugonjwa huu utokea kwa wastani wa asilimia nne (4%) ya watoto walio kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano. Watoto wengi ambao hupatwa na ugonjwa huu huwa haiwapelekei baadae kuwa na matatizo ya kudumu kama kupata ugonjwa wa kifafa, niasilimia tatu (3%) tu ambao wanaweza baadae kupata ugonjwa wa kifafa.
  Mmoja kati ya watoto watatu anbao wamewahi kuwa na homa ya degedege wanaweza wakapatwa tena na tatizo hili.baabhi ya watoto wanaweza wasipatwe kabisa na tatizo hili au wakapatwa mara moja tu kwa maisha yao yote. Lakini hauna jinsi ya kutabiri ni mtoto yupi ambaye anaweza kupatwa na shambulio hili.


  Homa ya Degedege Hutokea kwa Watoto Gani?

  Watoto wanaweza kurithi tabia hii ya kuumwa homa ya degedege kutoka kwa wazazi wao. Kama mama au baba aliwahi kuumwa ugonjwa huu basi mtoto ana asilimia 10-20 zaidi ya kuumwa ugonjwa huu hukilinganisha na yule ambaye wazazi wake hawakuwai kuumwa ugonjwa huu.

  Homa isababishwayo na maabukizi yoyote yale kama virus, bakteria na parasite

  Dalili za Homa ya Degedege ni Zipi?


  • Shambulio la ugonjwa huu likijitokeza mtototo uanza na kupotewa na fahamu na muda mfupi baadae mwili, miguu na mikono uanza kukakamaa na kurudisha kichwa nyuma, baada ya hayo miguu na mikono uanza kujitikisa.
  • Kushindwa kupumua na kutokwa na mapovu mdomoni
  • Macho kugeukia nyuma na kuonekana kwa sehemu nyeupe ya jicho
  • Shambulio huisha baada ya muda mfupi mara nyingi chini ya dakika tano
  • Baada ya shambulio mtoto hupitiwa na usingizi mzito kama takribani dakika 30 hadi saa nzima.
  • Akizinduka anaweza kushindwa hata kukutambua na akawa atamani kitu chochote kwa muda huo.

  Nini cha Kufanya Mtoto anapopatwa na Shambulio


  • Tulia na usichanganyikiwe
  • Ondoa vitu vya hatari karibu na mtoto na muweke sehemu ya usalama kama sakafuni.
  • Usijaribu kuweka kitu chochote mdomoni kwa mtoto hata vidole vyako.
  • Angalia muda wa shambulio kuanza hadi litakapo isha ili umueleze daktari.
  • Baada ya shambulio kuisha mlaze mtoto kwa upande na usimuamshe muache apumzike.
  • Shambulio la homa ya degedege sio kifafa na mtoto hapati maumivu yoyote wakati wa shambulio kwa hiyo usimpe dawa yoyote ile.
  • Baada ya hayo mpeleke mtoto kwenye zahanati, kituo cha afya au hospitali ya karibu kwa matibabu zaidi ya mtoto.
   
 2. M

  Masuke JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2013
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Heshima yako mkuu!

  Homa ya degedege inaweza kusababisha matatizo ya kuona pamoja na kusikia? Nauliza hivyo kwa sababu kuna mtoto wa ndugu yangu alipatwa na degedege lakini baadaye amekuwa na hayo matatizo, umri wake ni miaka miwili na hiyo hali amekuwa nayo kwa muda wa miezi miwili sasa. Nini inaweza kuwa chanzo hasa cha kutoona wala kusikia? Na tiba yake ni ipi na je kama atapatiwa tiba upo uwezekano wa kurudisha uwezo wake wa kuona pamoja na kusikia?

  Jamani madaktari wa hapa JF njoni msaidie, MziziMkavu, Riwa na wengine wote wenye ufahamu wa tatizo hili mtoe nasaha zenu.
   
 3. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2013
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  asante sana kaka
   
 4. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Habari Wadau,

  Leo asubuhi nimejikuta katika wakati mgumu pengine kuliko siku yoyote ile,Nilikuwa nimekaa na mtoto wangu akawa ananiambia baba macho yanauma,mara kichwa kinaniuma nikamgusa akawa amechemka sana mwili,nikamwambia tulia nikupeleke hospitali

  Tukaendelea kupiga stor na utani mwingi,ghafla akakamaa kama mti huku akitetemeka sana,nikamwita jina akawa haitiki tena, nikamkumbatia,Nilichanganyiwa sana,Ndipo nikamkimbiza hospital lakini ametibiwa.

  Nimeona si vibaya kuwashirikisha magumu yangu ya leo
   
 5. naumbu

  naumbu JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2013
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 3,314
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Pole sana!ni malaria makali hayo,mimi yalinitokea mwanangu alianza geuza macho ghafla wakat nacheza naye usku so naelewa what you went through
   
 6. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante Mkuu Lakini tumepima malaria hana kapewa dozi ya kunywa na Sindano ambazo ni anti-malaria.
   
 7. N

  Ngolombwe JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2013
  Joined: Mar 9, 2013
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri pia kuangalia kichwa chake huenda alipata tatizo la kuanguka akiwa mdogo na hizo ni athari zake. Apimwe vizuri
   
 8. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2013
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Dah pole sana. Mimi wangu bado mdogo kabisa ni kujipanga likitokea tatizo kama hilo.
   
 9. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2013
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ilikuwa inaelekea kwenye degedege
   
 10. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2013
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nahisi atakuwa wakiume,
   
 11. lowale

  lowale Senior Member

  #11
  Oct 27, 2013
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  pole sana mpendwa kweli hiyo hali ni ngumu sana .degedege hutokana na homa kali ikipanda kuzidi 40 huwa ubongo unapata short. na hapo ndipo degedege hutokea.
  Je alipoteza fahamu kwa muda wa dk ngapi?
  mwanao ana umri gani?
  je umepewa dawa gani?
  je uko mkoa gani?
  nipe majibu ya haya maswali ndipo nitakushauri la kufanya
   
 12. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hujakosea ni wa Kiume!
   
 13. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2013
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Pole mkuu Domy!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ilimchukua kama dakika kumi kupata fahamu..! Ana miaka mitatu,niko Mbeya,Dawa nilizopewa ziko mbali kidogo nimetoka nyumbani,
   
 15. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante kwa ushauri Mkuu!
   
 17. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante Mkuu,ukiwa na mtoto mdogo jitahidi sana kulala na pesa kidogo ndani!
   
 18. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2013
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  pole sana
  nakushauri siku zote uwe na paracetamol za kushusha homa za kuweka matakoni pindi uonapo mwanao ana joto kali
  pia jenga tabia ya kumpima homa uwe na thermometer nyumbani mwako,
  mtoto akilalamika anaumwa usipuuze hata kidogo.
  housegirl mwelekeze pia awe makini akimwona ana joto hachezi ampe paracetal ya kunywa.
   
 19. md4doctor2000

  md4doctor2000 JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2013
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 740
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Pole sana mkuu. Hiyo ni degedege (convulsions or fits) due to high fever. Anything which cause high fever in children can cause convulsions. It can be malaria (commonest cause in TZ) or any other disease which can cause high fever.

  Convulsion is one of the danger sign. Whenever it occurs...immediate take your child to the hospital!
   
 20. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2013
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante Kiongozi,Nitazingatia ushauri wako....
   
Loading...