Homa ikipungua kuna haya ya kufikirisha Ndugu Lissu

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
1. Sasa ule umbali haupo tena. Ukitukana au kudhalilisha au kusema uongo umbali kati ya kituo cha polisi na mhusika utakuwa umepungua mno.

2. Sasa ile kinga kuwa polisi wangeendelea na uchunguzi bila mhusika mkuu kuwepo sasa imeondoka. Sasa mtihani uko kwake. Atatakiwa atoe ushirikiano na polisi. La kwanza ni kuisaidia polisi ijue alipo dereva. Pili ni kuisaidia polisi ijue ilikuwaje risasi zipige mguu wa kulia badala ya kushoto.

3. Kesi zinazomkabili ni nyingi hasa ukizingatia tunaelekea kwenye kampeni.

4. Kuna tuhuma atatakiwa azitolee ushahidi. Tuhuma kama Magufuli na Serekali yake wanahusika na yeye kupigwa risasi, Magufuli hawezi kuandika hata sentence moja kwa kiingereza, n.k. Ni muda muafaka kujiandaa na ushahidi.

5. Ndani ya chama chake kuna mgombea mwenye fedha. Leo wachache wanamuita raisi lakini hawa sio "wajumbe"! Ajiandae kupambana na tajiri ilhali yeye alikuwa anaomba michango ya wazamiaji.

6. Ikiwa atanyinwa bendera na akakosa ubunge inampasa ajiandalie namna ya kusukuma gurudumu la maisha. Uwakili asiutegemee sana ajifunze kwa Fatuma.

7. Ajiulize sana je aliokuwa akidhani watamuunga mkono kutokea nje ni kweli walikuwa naye? Kitendo cha yeye kudai wamemuahidi kumsindikiza na akarudi na sanduku kiwe funzo kwake. Hakuna mdharau kwao anayethaminika ugenini. Watacheka na kunywa nawe ila mioyoni mwao umeshuka thamani mno.

8. Ajiulize sana katika hali ya ulemavu atamudu shuruba za kukamatwa, kulala gerezani na kushinda mahakamani?

9. Ajiulize mno bila kigugumizi hivi inawezekana Oktoba JPM aende Chato yeye aende Ikulu? Saa ingine njozi ndefu zina madhara yake. Asilewe walevi kumuita "raisi, raisi"! Mrema aliitwa sana cheo hiki hata kuzidi yeye.

10. Ikiwa chadema watampa bendera Nyalandu itampasa ajihoji je chadema ni nyumba salama kwake au aanze?

11. Kwa yeye kurudi nchini bila kusindikizwa ingawa aliihadaa dunia hayuko salama haoni kuwa dunia leo imemjua uongo wake? Hivi wangemsindikiza halafu wakute vile angewaambia nini? Hivi haoni serekali imecheza na hoja yake kwa uhodari mkubwa? Leo aliyepoteza ni yeye sio Serikali.

12. Ajihoji imekuwaje karudi licha ya serikali kupuuza ombi lake la kuhakikishiwa Ulinzi na usalama wake kana kwamba uhai na usalama wake ni special? Haoni kajifedhehesha kurudi bila kutimiziwa alichoomba?

Nimalizie kwa kumshauri huu sio wakati yeye kuanza siasa uchwara. Watoto waliumia sana baba ulioikatalia Ubeljiji. Ni muda ukae nao.

Itakuwa sio sawa ukaanza kuwa wa kulala Segerea. Jitahidi ulale nyumbani. Ningependa upewe bendera lakini uamuzi ni wa wale wachaga. Ila tafadhali jaribu kuacha kunyoa kiduku. Tanzania sio Korea Kaskazini. Utajikosesha kura kama utapewa bendera.

Kila la heri
 
Lissu Ni miongoni mwa wanasiasa wasio na hekima pamoja na busara ndani yake..

Kitaalamu tunasema; "Ni miongoni mwa wanaume walio na hormones za kike ndani Yao(Yani mdomo Sana)"

Pongezi kwa Mwanasiasa Nguli na mwenye hekima na busara Mh. Freeman Mbowe.
 
Hivi ukisimama mbele ya kioo unaona tashwira gani?
Basi ujue hicho kituko ukionacho mbele yako ni binadamu asiyetumia akili kufikiri mambo ya maana wala kuchambua ukweli bali box tupu
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom