HoloLens 2: Teknolojia ya Kufanya Kazi na Ana kwa Ana na Mtu Asiyeonekana

Yes Sophia ni matokeo ya AI.

She is in Saudi Arabia. Am I correct? Last time I checked she was in Saudi.

Nimeona pia robots kama Sophia wapo wengi tu sasa hivi.

And Japan is lead the way.

Pia simu hizi tunazotumia ni AI.

Na jambo lakushangaza sana AI devices/robots zinafikia uwezo wa kujifunza yenyewe.

Will this pose danger to humanity?

Baadhi wanaona ni hatari na wengine wanaona ni maendeleo tu.

Mimi naungana na kundi la pili.

Few years back I read about nanotechnology and how it revolutionize our understanding about the brain.

Sasa hivi kuna uwezekano ku-download taarifa toka kwenye brain yako.

This is interesting.

Ni kiasi cha muda tu kabla haya yote kuwezekana kwa hakika.
Hata hii app mpya inayozua gumzo ya Faceapp ni AI.
 
Mkuu iPhone na sakata la Huawei ni vitu viwili Tofauti.

iPhone ananunua modem Toka Qualcomm, even hio 5G ya kwenye simu kwa iPhone itatoka kwa Qualcomm, na Huawei nae pia ananunua modem kwa Qualcomm. Hivyo Hata Huawei Hana 5G kwenye upande wa simu, na sio 5G tu Hata 4G, 3G etc. Kwenye 5G upande wa simu asilimia Kama 90 Atleast ya royalties inamilikiwa na Nokia, Ericson na Qualcomm.

5G inayozungumziwa na inayoleta tabu ni mitambo, hii wanayofunga kina Vodacom, Airtel etc ile minara ya simu na miundombinu mengine.

Hii mitambo makampuni Kama Huawei wanawauzia mitandao ya simu na wao wanaseti mtumiaji wa mwisho aweze kutumia, Wao Kama marekani Wana Hofu wakimuachia mchina aseti hii mitambo watadukuliwa.

Jambo baya zaidi ni kwamba Marekani Hana alternative ya Kampuni ya Nyumbani yenye uwezo wa kutengeneza 3G/4G/5G hivyo inabidi kivyovyote achague kampuni ya Kigeni.
Umefafanua vyema mkuu! Salute!
 
Hata hii app mpya inayozua gumzo ya Faceapp ni AI.
Nilikuwa silijui hili mkuu, ingawa nimesoma mahali kwamba ukiidownload unakuwa vulnerable sana, taarifa zako zote zinatumwa kwa third party kwa hiyo kudukuliwa njenje! Hongera mliotumia na mnaoendelea kutumia FaceApp! haya mambo ya teknolojia unapaswa kuwa makini sana!
 
Mkuu iPhone na sakata la Huawei ni vitu viwili Tofauti.

iPhone ananunua modem Toka Qualcomm, even hio 5G ya kwenye simu kwa iPhone itatoka kwa Qualcomm, na Huawei nae pia ananunua modem kwa Qualcomm. Hivyo Hata Huawei Hana 5G kwenye upande wa simu, na sio 5G tu Hata 4G, 3G etc. Kwenye 5G upande wa simu asilimia Kama 90 Atleast ya royalties inamilikiwa na Nokia, Ericson na Qualcomm.

5G inayozungumziwa na inayoleta tabu ni mitambo, hii wanayofunga kina Vodacom, Airtel etc ile minara ya simu na miundombinu mengine.

Hii mitambo makampuni Kama Huawei wanawauzia mitandao ya simu na wao wanaseti mtumiaji wa mwisho aweze kutumia, Wao Kama marekani Wana Hofu wakimuachia mchina aseti hii mitambo watadukuliwa.

Jambo baya zaidi ni kwamba Marekani Hana alternative ya Kampuni ya Nyumbani yenye uwezo wa kutengeneza 3G/4G/5G hivyo inabidi kivyovyote achague kampuni ya Kigeni.
Nilisikia Verizon wameanza kufunga mitambo ya 5G, kwenye baadhi ya majimbo huko USA... Hivi hiyo Verizon ni kampuni ya nchi gani.!?
 
Hata hii app mpya inayozua gumzo ya Faceapp ni AI.

Kabisa hiyo App ni AI.

Na mara nyingi app za namna hii zinalenga kukusanya taarifa za watumiaji na kuziuza.

It is a big money Industry.

Digital advertisers/businesses wapo tayari kutoa kiasi chochote cha pesa kununua taarifa za potential customers.

Hata kama kwenye privacy policy watasema taarifa zako ni salama lakini hawataacha kuuza taarifa.

Facebook kwa mfano walipata kashfa ya kuuza taarifa za watumiaji wao kipindi cha uchaguzi wa US.

Miaka hii ya high tech mambo ya watu wengi yapo wazi tu. Japo hatufahamu hivyo.

Facebook au Google wanafahamu mambo yanahohusu tabia yako kuliko marafikia na familia.

Kifupi tupo exposed sana kwa walioshikilia miundombinu ya teknolojia.
 
Yesu akichelewa kuja tutashuhudia maajabu ya technology.

4 Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.

Danieli 12 :4
 
napenda na natamani sana kusoma na kuwa nguli ktk mambo ya technology ila ndo umri ushaenda na mambo ni mengi muda mchache
 
Kweli mkuu na hii ndiyo vita kubwa kati ya China na Marekani (Huawei vs iPhone) ambayo watu wengi hawaijui, wa kwanza kuingiana 5G ndiye mshindi katika mapinduzi haya, Huawei walipanga wawe wa kwanza, Marekani akaona 'usinitanie wewe', akawatingisha! 5G ni zaidi ya mapinduzi!
Duuuh ebwana nilikuwa sijui kumbe ndo sababu hiyo
Hahaha
 
Miaka 50 ijayo kama bado dunia itakuwa ingali salama, wanadamu watashuhudia technology ya ajabu sana.

Na hata kizazi cha kipindi hicho wataicheka sana hii tech tunayoishangaa sasa hivi.

“Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.”
— Danieli 12:4 (Biblia Takatifu)

Sent from my cupboard using mug
 
Kabla sijarudi kwa MAVUMBI nilikotoka, nachotamani ni ipatikane Teknolojia ya kurekodi Ndoto na iweze kutazamwa kwenye Uhalisia wake, kila mtu ataangalia movie zake mwenyewe na wale wenye ndoto kali kali watauza zao na kupata hela😁😁 yaani hapo kila mtu atakuwa Mwigizaji bila kamera, director wala nani....
 
Vipi mkuu hii yako bado haijavumbuliwa?
 
View attachment 1156332
Wakati teknolojia ya simu za mkononi zenye uwezo wa ‘touch screens’ ikiingia, kila mtu alikuwa akistaajabu kwamba utaweza vipi kubofya simu ambayo haina ‘buttons?’ yaani uguse tu kioo halafu mambo yawe yanaenda kama unavyotaka? Ilionekana kama ni kitu kisichowezekana.

Lakini sasa imeshakuwa kitu cha kawaida kabisa, kiasi kwamba simu zenye ‘buttons’ au vitufe vya kubonyeza, zinaonekana kupitwa na wakati, kila kitu ni ‘touch’!

Teknolojia hiyo imehama, hivi sasa siyo simu tu zenye touch screens, kuna laptop za kisasa ambazo kila kitu kinafanyika kwa kugusa kioo tu, lakini pia kuna televisheni za majumbani zenye touch screen.

Sasa kwa sababu ‘touch screens’ siyo kitu cha ajabu tena, wanasayansi wameendelea kuumiza vichwa kuja na kitu kikubwa zaidi na hapo ndipo ilipogunduliwa teknolojia iitwayo HoloLens.

Hii ni kama ‘touch screens’ tu lakini tofauti yake, wakati kwenye ‘touch screens’ ukilazimika kugusa kioo cha kifaa unachotumia, kwenye HoloLens, unavaa miwani yenye teknolojia kubwa ya kugeuza kila unachokiona kupitia miwani hiyo, kuwa touch screen.

Twende taratibu, yaani ni hivi; unavaa miwani maalum iliyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu, halafu ukiitazama miwani hiyo, eneo lote unaloliona mbele yako linakuwa ni ‘screen’, na jinsi ilivyotengenezwa kimaajabu, japokuwa unaivaa machoni, bado unaweza ‘ku-touch’ kwa mikono yako kila kinachoonekana kwenye screen.

Yaani unapoivaa, halafu mtu ambaye hajavaa miwani hiyo akikutazama, anaweza asielewe unafanya nini, au akahisi pengine umechanganyikiwa na ndiyo maana inashauriwa kwamba unatakiwa kuivaa ukiwa ndani ya chumba kilichotulia.

Sasa kwenye matumizi yake ndiyo utachoka! Miwani hii ina matumizi makubwa na mazito yanayoweza kukushangaza. Kazi yake kubwa ya kwanza, ni kukuunganisha na watu waliopo sehemu mbalimbali duniani kwa wakati mmoja, mnaweza kuunganishwa watu wawili, watatu au hata kumi ambao mpo sehemu tofauti duniani, wote mkajiona kama mpo ndani ya chumba kimoja.
View attachment 1156333
Unapounganishwa, unamuona mwenzako aliyevaa miwani kama yako, akiwa pembeni yako hata kama wewe upo Dar es Salaam na yeye yupo Washington DC, teknolojia inawaleta pamoja, tena sio kwa picha za kawaida, bali zenye kiwango cha 3D.

Kisha baada ya kuunganishwa, wote mnaweza kuanza kujadiliana kuhusu kitu kimoja, kutegemeana na muongoza mjadala anataka mjadili kuhusu nini. Kwa mfano, yawezekana mgonjwa yupo Dar es Salaam, anaumwa sana lakini madaktari wa hapa hawana uwezo, kwa hiyo wanawaunganisha madaktari waliopo China, India na Ujerumani.

Kwa wakati mmoja, wote watakuwa na uwezo wa kumtazama mgonjwa, kuchunguza taarifa zake za kina na kutoa ushauri wa nini kifanyike, tena siyo ushauri wa maneno tu, ushauri wa picha za video kuhusu nini kifanyike na kwa wakati gani! Wote watakuwa ni kama wapo wodini wakimtazama mgonjwa.

Sasa unaweza kuona kwamba ni mambo ambayo yapo mbali sana na yatachelewa kutekelezeka lakini kwa taarifa yako, teknolojia ya HoloLens, tayari ilishaanza kufanya kazi na sasa, Kampuni ya Microsoft imezindua toleo jipya la teknolojia hiyo, HoloLens 2 ambayo tofauti na toleo la mwanzo la majaribio, hii imeboreshwa maradufu.

Miwani hiyo, inatarajiwa kuanza kuuzwa kwa bei ya dola za Kimarekani 3,500 ambazo ni sawa na takribani shilingi milioni 8 za Kitanzania ikiwa na uwezo wa kuunganishwa na Wi-Fi, kwa hiyo cha msingi ni kuhakikisha mahali ulipo kuna intaneti yenye kasi, hilo likifanikiwa basi dunia nzima inakuwa machoni mwako, si kiganjani tena!
Sahihisho hologram siyo hololens .

Hologram -hololens .

Stand to be corrected
 
Back
Top Bottom