Hollywood Stars ambao pia ni Marubani (Pilots)

I_manyota

Member
Aug 15, 2012
48
44
Hollywood ni makazi pendwa sana ya watu maarufu huko Marekani na sio kuwa maarufu, na hata kwa matajiri mbali mbali duniani Hollywood it's a place to live na hasa Beverly Hills. Na hapa naomba tuwekane sawa kabla sijatoa hiyo list, maana najua kichwani mwako unawaza movie tu baada ya kuona nimetaja Hollywood 😂 😂 .
Sasa iko hivi ni kweli hollywood umaarufu wake umetokana na mambo ya sinema na waigizaji maarufu wengi tangu kipindi hicho walikua wakiishi maeneo hayo ili kuraisisha kazi zao pindi wanapoitajika. Story ya Hollywood ni ndefu na leo sio siku yake, sasa nataka nikwambie jambo moja unaposkia Hollywood star sijui celeb usikalili basi lazima awe muigizaji hapana Hollywood kwa sasa wanaishi watu maarufu wa kila namna japo watu waigizaji na watu wanajihusisha na mambo ya TV wengi wanaishi huko sababu ndio kitovu cha hiyo sekta studionyingi nakubwa duniani ziko huko ma director wakubwa wanaishi huko sricpt writers wakubwa wapo huko kila takataka iko huko.
Yote kwa yote lazima uwe na pesa kuishi mitaa yao. Kwahiyo usishangae mwanamitindo akaitwa Hollywood celeb, as long as unaishi hiyo mitaa that's it. Twendeni sasa

1. HARRISON FORD
Hakuna asimyemjua huyu mzee wa Indian Jones, Star wars na ileee ya Air-force One ambayo wengi wetu ilikua movie pendwa sana kipindi hicho. Na mzee alishawahi kupata na ajari.
Harrison_ford_pilot-2.jpg
141030090621-harrison-ford-2001-exlarge-169.jpg



2. JOHN TRAVOLTA
Huyu bwana mkubwa mimi ndio muigizaji wangu bora wa muda wote, John hajawahi kuniangusha yani kama ningekuwa kwenye hayo mambo ya sanaa ya uigizaje basi huyu ndio angekua role model wangu. John kafanya kufuru maana amejenga na kiwanja cha ndege kabisa nyumbani kwake. Moja ya ndege alizowahi kurusha ni Boeing 707
1e1fa8f8b4db990b422987fb47a2300c.jpg
main-qimg-3c4cf99c83be71d7b72a8c9b970a1283.jpg
d4f64b47ec3b22decdc5e1927e349225.jpg
john travolta plane.jpg


3.GISELE BUNDCHEN
Mwanamitido huyu kutoka hollywood , anapiga mpunga kama hana akili nzuri, amewahi kuwa katika list ya wanamitindo wanaolipwa pesa nyingi duniani pia aliwahi kushika namba 16 ya matajiri wanawake duniani. Mrembo huyu kutoka Brazil pa ameigiza movie kadhaa kadhaa
Na mara yake ya kwanza kujifunza urubani alikua na mimba, ila Gisele yeye ni chopper tu.
.
gisele-bundchen-today-square-180909_41669f624a6f58b115b875b367832ca8.jpg


4.TOM CRUISE
Mzee wa Top Gun, Mission Impossible, Jack Reacher nk, huyu mzee nae alinogewa na urubanai baada ya kurekodi movie ya top gun miaka hyo ya 80's akaona isiwe tabu akaenda kujifunza urubani na mwaka 1995 akawa amepata leseni yake kwa mara ya kwanza. Tom na urubani damu damu.

851077300.jpg
30E35A2300000578-0-image-a-2_1454964923462.jpg


5. MORGAN FREEMAN
Mzee tangu enzi hizo akiwa jeshini miaka ya 60's Morgan alikua akipenda urubani akaona isiwe tabu akajiunga na kozi ya urubani mambo yakajipa
.
morgan-freeman-biography-filmography1.jpg
Morgan_Freeman-Acoso_sexual-Harvey_Weinstein-Hollywood-Cine_309732160_79173876_1024x576.jpg



6. ANGELINA JOLIE
Muigizaji wangu bora wa kike wa muda wote Angelina Jolie ex-wife wa Brad Pitt mtoto wa Jon Voight yule mzee wa kwenye Anaconda ileee ya Ice cube na J lo. Star mwenye vituko vya aina yake, hii kichwa unaambiwa ishawahi kulana na bro wake anyways sio leo😂😂, yeye mwaka 2004 ndio alianza urubani.
91441__jolie_l.jpg
angelina jolie da42.jpg
Angelina-Jolie.jpg


Asanteni
 

Attachments

  • bruce_dickinson_1335876029_crop_440x259.jpg
    bruce_dickinson_1335876029_crop_440x259.jpg
    18.1 KB · Views: 9
Tom cruise
Jolie
Na the magician mzee freeman
love them sana sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom