Holiday INN Hatunayo tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Holiday INN Hatunayo tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkora, Jun 2, 2008.

 1. M

  Mkora JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  holiday inn dar hatunayo tena
  Meneja Mkuu wa hoteli ya Southern Sun Dar Adam Fuller akifungua shampeni kuashiria uzinduzi rasmi wa hoteli hiyo uliofanyika leo mchana. kufuatia uzinduzi huo jina la hoteli ya Holiday Inn iliyopo barabara/mtaa ya Garden limezikwa rasmi leo. pembeni ni baadhi ya wafanyakazi wa hoteli hiyo wakishuhudia uzinduzi huo


  Wadau Naomba kuwasilisha
  i) Hao waliopitisha hiki kipengele cha tax holiday kuna makosa kuturudisha mshahara wetu.
  ii) Hivi wansheria wanchi nyingine wamesomea wapi ikiwa wanfanya mazuri kwa nchi zao
  iii) Kifanyike nini kuhusu haya mambo ambayo ni ya aibu kubwa sana kwenye specialization ya sheria na uwekezaji
  iv) Hivi ule uzalendo wetu umeenda wapi? isitoshe hawa wanaofanya haya mambo kama sikosei hata suti walinunuliwa walipokuwa wanaenda kusoma nje
  v) Je na sisi itakuwaje tuliojisomesha kwa kubaba box ikiwa hao waliolipiwa kila kitu wanafanya haya mambo
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kwa serikali ya ki-ZECOMEDY ulitegemea wafanye nini??
  Mwananchi wanaomjua wao ni mbunge na si vinginevyo
   
 3. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wazee hali mbaya..
   
 4. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,658
  Likes Received: 2,464
  Trophy Points: 280
  Five year tax holiday...yalianza na Sheraton-Royal Palm-Movenpick, sasa yamehamia tena kwa Holiday Inn-Southern Sun...next sijui wapi...kina Mramba hao na matax holiday yao...
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sheria zote zilizopitishwa wakati wa Mwanasheria Mkuu, Andrew Chenge, kama mshauri wa Sheria nchini, zipitiwe upya!
   
 6. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Jamani naomba niwaelewesheni, haina maana kua Holiday Inn imebadilisha. Jina la SOUTHERN SUN HOTELS (TANZANIA) LIMITED wakiwa na VAT Numbner 10014009R lilikuwepo tangu mwanzo. Holiday Inn ilikua kama Brand name tu, yaani jina la kibishara tu na sio la kampuni kama lilivyosajiliwa kwa Msajili wa Makampuni. Kwa mfano, Tigo ni brand name lakini Jina la Kampuni ni MIC Tanzania Ltd, siku wakiamua kuua Tigo na kuita MIC Tanzania Ltd haina maana kua wamebadilisha jina bali wamebadilisha Brand Name au jina la bidhaa yao au biashara/huduma. Kwa Hiyo hasi AKA ya SOUTHERN SUN HOTELS (TANZANIA) LIMITED ilikua Holiday Inn.

  Kama haijaeleweka hapo itabidi ulipie ili uende masomo ya ziada kwa ufafanuzi zaidi
   
 7. S

  Sam JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2008
  Joined: Jun 6, 2006
  Messages: 416
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama information zako ni za kweli ninashukuru kwa ufafanuzi!
   
 8. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Holiday Inn wanafungua hoteli pale zamani ilipokuwepo Mawenzi,Lakini Holiday Inn hio haina uhusiano na hio iliyobadilisha jina
   
 9. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #9
  Jun 2, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Wabunge waliopitisha hizi sheria si wapo, kama tumeweza kumzomea Mkapa barabarani, kwa nini na wao wasizomewe hadi watakapobadilisha hizi sheria?

  On the hand, pengine tutaanza kuamka na kujua kazi za wabunge. Maana kwa muda mrefu tumedanganywa kwamba kazi ya mbunge ni kuleta maji, kugawaia wananchi wake unga wa mahindi wakati wa njaa. Matokeo yake tumepeleka wafanyabiashara na wajasiria mali bungeni wenye uwezo wa kuleta maji na kugawa unga lakini hawajui kazi zao na walipoenda bungeni wakapitisha kwa mbwembwe kila kitu kilichowasilishwa na Chenge. Sasa kwa utaratibu huo hao wabunge wangeweza kweli kuchambua issues zilizowasilishwa na na Chenge wa Havard?

  Kuna haja pia ya kuhakikisha kisheria kuwa wale wasaidizi wa wabunge wanakuwa na basic competence. Sasa hawa jamaa wanaajiri ndugu zao ambao wengi wao hata library index, achana na google, hawajui na hawawasaidii wabunge kuwa na informed opinion kabla ya kupitisha miswaada ya sheria kwa mbwembwe na jeuri ya chama!
   
 10. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kuna hoteli nyingine mpya kabisa hapa Dar inamiliziwa kujengwa na inaitwa Holiday Inn, kwa hiyo inawezekana kabisa ikawa ni jengo tu ndio wamehama na kuhamia pengine. Hoteli hiyo ipo karibu kabisa na Posta Mpya !
   
 11. M

  Mbangaizaji Senior Member

  #11
  Jun 2, 2008
  Joined: Jul 23, 2007
  Messages: 121
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Wakuu,

  Naomba nimuunge mkono Mkombozi na kumshukuru kwa maelezo mazuri. Holiday Inn ni franchise kama unavyoona MacDonalds, Steers etc. Southern Sun ndo initially iliyokuwa na franchise ya Holiday Inn na baada ya Holiday Inn kuissue same Franchise kwa Eclipse Hotel Ltd(Zamani Mawenzi na ndio new owners wa Jangwani Sea Breeze nasikia hata hii wanataka kuifanya Holiday Inn Resort). Southern Sun nathani hawakufurahia ndo wakaamua kurudia jina lao halisi. In any case payments zote zao huwa zinatumia jina la Southern Sun, hawana account hata ya jina la Holiday Inn.
  Vile vile Holiday Inn wanazo criteria zingine zaid kwa mfano unaweza ukaona Holiday Inn, Holiday Inn Beach Resort na hata Holiday Inn Express. Ni franchise tu na huwa hata wanasupervise ujenzi, etc ili ukifika kiwango wanakupa franchise a unalipia loyalt ya kutumia jina lao. Nadhani kama Uingereza huko kuna ma Holiday Inn mengi tu na wala si za mtu mmoja.
   
 12. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mkombozi maelezo yako sijaelea nitalipia kama ukitaka nilipie lakini na zile sheraton royal palm na nyingine naomba maelezo yake
   
 13. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2008
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  ALIYEUMWA NA NYOKA BWANA HATA UNYASI ATAKIMBIA..."KWELI JEURI HUMPUMBAZA MWENYE HEKIMA, NA RUSHWA HUUHARIBU UFAHAMU:Mithali 7:7
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kuna uhakika wowote wa tukio hili kwamba ilikuwa just a brand name na sasa wamerudia kule kule ? Wazungu wanatumaliza jamani hadi leo kuna mambo ya tax holiday bado ? Kama yako basi ukweli ni kwamba wale wameishia na wamekuja wale wale na jina jpya .
   
 15. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huo mstari haupo!
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Vinara wa huu mchezo walikuwa, Mramba, Idd Simba, Sumaye, na Yona!
   
 17. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kuna wakati jambazi likiingia nyumbani likaua strangers halafu lisiondoke na kitu waendesha mashitaka huwa wanajiuliza, huyu jambazi nia yake ilikuwa nini hasa? Kwamba, jambazi nalo ni binadamu na lina kichwa.

  Unadhani hawa kina Mramba, Simba, Sumaye, na Yona nia yao nini kuwachorea michoro wazungu wa Sheraton na Movenpick wakwepe tax kwa sheria za kubadili majina?

  Hawa Wazee hawana ndugu masikini bushi kwao huko Hanang na Ilala na Uchagani huko mpaka wasaidie kushika miguu wakati Wazungu wana repu nchi yetu?
   
 18. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Omulangi, Bible does not tell that, instead Prov. 7:7 written "I saw among the simple, I noticed among the young men, a youth who lacked judgement." NIV. translation yako siyo sahihi.
   
 19. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #19
  Jun 3, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na bado baadaye itaitwa Eclipse hotel. Wabunge wetu wenyewe ni vihiyo tusitegemee kutufanyia chochote
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ufafanuzi kwamba hiyo ni change ya brand name ni kweli, lakini wasiwasi ni wangu ni kuwa kutokana na ufisadi ulioenea hapa kwetu, kuna uwezekano viongozi wetu wakatumia nafasi hiyo, kula deal na wazungu na kuondoa rekodi za zamzni ili waanze upya. This can be done if they dont play thei parts
   
Loading...